Dada yetu anaishi na Virusi vya UKIMWI, tumwambie ukweli mchumba wake?

Fuatilia kama hawajavuana chupi umwambie bhana.
 
Kama unajali kweli kama unavyodai, usikubali haya yatokee.
Lakini sio wewe unayepaswa kumweleza huyo jamaa!
La kufanya ni uzungumze kwa marefu na mapana na huyo dada juu ya analotaka kulifanya.

Mweleze haki ya jamaa kujua hali yake ya kiafya na umwambie ni jukumu lake kama mate/partner wake kumwambia hayo.

Mwambie kama hatomwambia kuhusu hali yake ya afya, utamwambia wewe.
Sasa kama huyo dada ana akili timamu hatokubali mtu mwingine kumwelezea mchumbake hali yake ya afya. Atamwambia.

Hakikisha anamwambia kabla hawajaoana.
Sasa utakuwa umeua ndege wawili kwa jiwe moja.
 
Nakumbuka maneno ya Alhaji Mwinyi (Mzee wa Ruksa) "Ndugu Watanzania huu ugonjwa umekaa pabaya, tena pabaya sana"
 




Fanya kama kutoa nasaha tuu ya ki utu uzima@wasisisitize wasisahau kwenda ku chek afya Zao@kupitia apo nazan utapata defenc mechanism hata yakija kubumbuluka badaye
 
Kisheria hakuna ndoa inayofungwa bila vipimo vya daktari so itajulikana na km wataamua kuoana pia inawezekana.
kwa kweli mkuu wakapime kabla ya ndoa, ila wasiwasi ni kama ameanza tendo la ndoa kabla ya ndoa-hapo uaminifu wake kwenye ulokole wake utakuwa umepungua na atajutia.hatuwezi kusema ni wa kawaida, LAZIMA UKWELI USEMWE
 
hivomnaoana tuu kienyeji kisa niniau eti ni walokole ndio mnaaminiana....kulaleki hakuna utaratibu wa kuoana kienyeji kansanixo huyo jamaa naye ntamshangaa akitakaresi na huyo dada naye muuaji tu hana utu
 
Siku hizi si hauozeshwi mpaka uwe na cheti cha kupimwa HIV?

Uungwana ni kuambiana ukweli.

Huyo dada'ko kama anamficha huyo mchumba bado hajaokoka kama unavyodai, anajidanganya tu.

Pengine na mchezo kisha mpa. Si mnasema siku hizi hamuoani mpaka mlane kwanza!

Kuokoka kiukweli ni kujisalimisha kwa Mwenyeezi Mungu aka Kusilimu, vinginevyo ni uongo tu.
 
ahaaa hapa nam mtaani kuna dogo kazaliwa nao kila siku anabadilisha wavulana
 
Nadhani hela mlizokula ni chache kuliko mtakazopewa baada ya kumwambia mtu ukweli na kuokoa ndoto zake kufutika!Hofu yangu ni kama kweli bado hajapewa mzigo kavukavu maana hapo sioni element za ulokole kabisaa, ni full matamanio!Ukishindwa kumwambia nitumie namba za jamaa PM na jina la dada yako nikusaidie kuwaweka sawa
 
Safi sana!Wewe unastahili dhima ya hata kupewa udiwani aisee
 

Mwambie kijana wa watu, na dada yako oia kuwa anachofanya ni dhambi na mshahara wake ni mauti.
 
ushauri wangu ni kua tatizo la dada yako ni lake na ni maisha yake na huyo mchumba wake. si jukumu lako wewe kuingilia mambo yasiyokuhusu. Jali maisha yako na waache waendelee. Jiweke kwenye nafasi ya dada yako, halafu dada yako angeenda kusema kwa mchumba wako status yako, how would you feel.... Kama ni lazima usaidie, jitahidi kumuongoza dada yako a built ujasiri wa kumwambia mchumba wake yeye mwenyewe na sio wewe ndio uwe msemaji. Ukimwi sio ugojwa kama cancer na diabetes bali ni mfumo kubadilika mwilini. wewe mwenye kiherehere unaweza ukaondoka duniani kwa jambo dogo sana ukawaacha wakaendelea kuishi miaka mingini 20 na watoto wenye afya tele. achana na hii kitu, its too personal. nyinyi kama familia endeleeni na maandalizi ya harusi wala msizungumzie hili jambo maana si lenu bali ni la dada yenu, atajua mwenyewe jinsi ya kulitatua kwa mchumba wake. kwanini uumie moyoni kwa jambo ambalo si lako. binadamu tuna mambo ya ajabu sana. Kabla hawajaamua kuoana ilikua ni jukumu lao wenyewe kuamua kwenda kucheki afya zao maana mwisho wa siku ni kwa maisha mazuri, sasa kama hawakufikiria hilo wewe nini wa kutaka kuropoka. incase unamwambia halafu asikuamini akakuona unamfanyia roho mbaya hasa kwa kuhisi unaharibu kwa vile ni ndugu wa kambo, utajisikiaje? kama si aibu iliyokithiri. waache na maisha yao, na wewe endelea na ya kwako.
 
hapo kazi bure vijana wengi hawawez kutangaza ndoa km hawaja onjana.ila unatakiwa umwambie hata kw indirect way hivi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…