Kete Ngumu
JF-Expert Member
- Nov 21, 2014
- 6,656
- 6,886
Wapime kwanza kabla ya kufunga ndoa
Mkuu hapo hakuna problem.
Kaa kimya.
Kwa Kifupi CANCER na KISUKARI ndio hatari zaidi....pia hauambukizi.
si kweli; ndoa nyingi tu zinafungwa bila vipimo. inategemea ni kanisa gani, ila makanisa menge hakuna hii condition.Kisheria hakuna ndoa inayofungwa bila vipimo vya daktari so itajulikana na km wataamua kuoana pia inawezekana.
Sijampotosha soma vizuri comments zangu. kama anaona ni vyema mchumba akajua, basi wa kusema ni dada yake na si yeye kama kama. ajaribu kum convince dada yake aweze kuongea na mchumba wake kuhusu status yake kama uwezo huo anao. kama dada hataki, basi akae mbali. kua na ukimwi haimaanishi unakufa kesho. dunia ya leo asojua ukimwi ni nani. watu walipanic siku za nyuma valikua hawaujua vizuri. sasa hivi hata wenye virusi wanazaa tena very healthy kids kupita wewe unayejiona una afya njema.
Hayo yao wenyewe hayakuhusu yaache kama yalivo.
Habari zenu wana Jf,
Nina mdogo wangu wa kike baba mmoja ila mama ndio tofauti, mzee alikua na wake wawili.Huyu binti alikua akifanya biashara za kusafiri kwenda Kampala na nairobi kwa miaka mingi, ni mdogo wangu wa nne kuzaliwa, tupo Tisa kwa hao mama wawili, ila mama zetu hawapo duniani, mzee ndio bado yupo katika hizi safari za kibiashara bahati mbaya akapata ugonjwa huu wa kisasa, aliugua sana hapo katikati, nadhani ilikua 2006-2009.
Baadae akapona akainuka kabisa kutoka kitandani lakini akaambiwa asiache dawa za kurefusha maisha, tukamzuia kuendelea na hizo business za kusafiri, akaokoka na bado anaabudu hadi sasa, amenona hasa, amekua kipande cha mtu.Simzungumzi vibaya Dada yangu, ila kwa kweli amekua na wowowo lenye kumvutia mwanaume yeyote yule.
Nadhani ni katika muonekano huo ndipo akajitokeza mlokole mwenzie huko kanisani kwao kutaka kumuoa, huyo jamaa kachanganyikiwa na yuko resi mno, ameshaniletea barua nami nikaipokea pamoja na wenzangu, baadae tukamtajia mshenga wake mahari nayo akalipa na tulishaila, tuligawana makaka, nae binti tukampa kidogo.
Sisi hatujaanza utaratibu wa vikao ila wao upande wa jamaa walikaa vikao viwili tayari, wakati wote huu mimi nilidhani dada alishamweleza status yake huyu mchumba, na pengine nikadhani wote wana status hiyo hiyo ya HIV positive wameamua ku team up kuunda familia, kumbe sivyo huyu jamaa hajui chochote kuhusu hali ya huyu dada yangu.
Kuna dada yetu mkubwa aliempeleka kanisani huyu binti na wanasali pamoja, juzi alimuuliza muolewaji kama amemwambia mchumba hali yake, akajibu hajamwambia, anaogopa akimwambia atakosa ndoa, na yeye anahitaji kuwa na familia yake kama mwanamke, na kwamba yeye mwenyewe haachiwe jambo hilo atalimaliza mwenyewe, na kwamba tusimwambie mchumba chochote.
Roho yangu inanisuta sana kushiriki jambo hili, hasa ukichukulia kuwa nyumba na mji wangu ndio unaochukuliwa kama nyumbani kwao na bibi harusi, na tupo karibu sana kimawasiliano na huyo jamaa.Mfano ni juzi tu kanitumia laki mbili akisema ni ya chai.
Pia ni msomi mwenye carrier yake na future inayoeleweka, hivyo nafsi inanisuta, wenzangu wanadai afya za maharusi sio kazi yetu, kwamba sie kazi yetu ni kusherekea tu, kwamba ni miaka sasa hatujawa na harusi tunachangia watu tu
Wadau, nahitaji msaada wa mawazo
Au na mimi nipotezee tu watajuana wenyewe?
What is for the rest of your life means. For me it can be 3 yrs.
kwa hiyo kama kuwa na ukimwi hakumaanishi kufa leo au kesho ndo sababu ya maana ya kumfanya mtu anyamaze jamaa akaupewe tu kwa kuwa hatakufa leo au kesho??? athari za vvu unaziona kwenye kifo tu huzioni kwenye sex ambayo ndo kiungo cha ndoa, wala kwenye uzazi ambao ndo lengo la ndoa, wala kwenye gharama na muda wa matibabu. Jamaa aambiwe tu. haya mambo unayoyasema hapa hata huyo bwana arusi mtarajiwa anayajua kwa hiyo ataamua mwenyewe.
ukivunja sheria kwa nia ya kuokoa maisha hauhukumiwi. uhai wa mtu una thamani. unasema dada mtu aendelee kushawishiwa amwambie mchumba mwenyewe, na akikataa kaka mtu ajitoe kwenye mchakato!! akijitoa kwenye mchakato itafuta akilini mwake kuwa alikuwa anajua ila akanyamaza kwa kuwa haolewi yeye? kama muoaji atamuona shemeji yake kuwa ni muongo na fisadi kuna shida gani? zitakuwa ndo gharama zake za kusema ukweli. hatakuwa amepoteza kitu zaidi ya guilty aliyo nayo sahivi.
Hivi ule utaratibu wa walokole kupelekwa na mzee wa kanisa kupima afya na mimba kabla ya ndoa haupo kwenye makanisa mengine? Mimi nakumbuka mke wangu (wakati huo mchumba) alipmwa ujauzito mbele ya mjumbe aliyeteuliwa na kanisa..na baadaye mimi na yeye tulipelekwa hospitali na mjumbe wa kanisa kupimwa maambukizi ya HIV.
Kama kanisani kwao hawana huo utaratibu, na kama kweli hajamfahamisha itakuwa busara kama ukihakikisha jamaa amepata taarifa. Ingekuwa vema kama dada yako angesema mwenyewe, ila yaelekea ameipania ndoa hasa wala hawezi kusema. Hata hivyo sioni kama kutakuwa na ndoa yenye afya baada ya jamaa kugundua kuwa ameoa mwathirika ambaye kwa makusudi kabisa ameamua kuwa kimya na kumwambukiza ugonjwa huo. Kuna hatari ndoa ikavunjika mapema sana na jamaa kuchanganyikiwa au hata kujidhuru.
Yawezekana dada yako anataka tu hadhi ya kuwa na ndoa, kwa maana kwamba hata ikivunjika baada ya siku 2 angalau na yeye atakuwa ameimbiwa "anameremeta", otherwise, sioni ndoa ya kudumu katika mazingira yenye usiri wenye nia ovu kama hiyo.
Kama unaogopa kumwambia shemejio moja kwa moja, tengeneza mazingira ya kijasusi uhakikishe anapata "anonymous message" kumtahadharisha na kusisitiza amwombe mwenzie wakapimwe afya zao kwa ujumla. Kwa vyovyote vile, reaction itakayofuatia baada ya pendekezo hilo itatosha ku-solve kesi hiyo.
ushauri wangu ni kua tatizo la dada yako ni lake na ni maisha yake na huyo mchumba wake. si jukumu lako wewe kuingilia mambo yasiyokuhusu. Jali maisha yako na waache waendelee. Jiweke kwenye nafasi ya dada yako, halafu dada yako angeenda kusema kwa mchumba wako status yako, how would you feel.... Kama ni lazima usaidie, jitahidi kumuongoza dada yako a built ujasiri wa kumwambia mchumba wake yeye mwenyewe na sio wewe ndio uwe msemaji. Ukimwi sio ugojwa kama cancer na diabetes bali ni mfumo kubadilika mwilini. wewe mwenye kiherehere unaweza ukaondoka duniani kwa jambo dogo sana ukawaacha wakaendelea kuishi miaka mingini 20 na watoto wenye afya tele. achana na hii kitu, its too personal. nyinyi kama familia endeleeni na maandalizi ya harusi wala msizungumzie hili jambo maana si lenu bali ni la dada yenu, atajua mwenyewe jinsi ya kulitatua kwa mchumba wake. kwanini uumie moyoni kwa jambo ambalo si lako. binadamu tuna mambo ya ajabu sana. Kabla hawajaamua kuoana ilikua ni jukumu lao wenyewe kuamua kwenda kucheki afya zao maana mwisho wa siku ni kwa maisha mazuri, sasa kama hawakufikiria hilo wewe nini wa kutaka kuropoka. incase unamwambia halafu asikuamini akakuona unamfanyia roho mbaya hasa kwa kuhisi unaharibu kwa vile ni ndugu wa kambo, utajisikiaje? kama si aibu iliyokithiri. waache na maisha yao, na wewe endelea na ya kwako.
hata ukimwambia itakua ni kazi bure maana jamaa atakua keshamvua chupi huyo mgonjwa siku nyingi sana.
Kaongea ukweli kiasi fulani.mmhhh...da asia