Dada yetu anaishi na Virusi vya UKIMWI, tumwambie ukweli mchumba wake?

Dada yetu anaishi na Virusi vya UKIMWI, tumwambie ukweli mchumba wake?

Kisheria hakuna ndoa inayofungwa bila vipimo vya daktari so itajulikana na km wataamua kuoana pia inawezekana.
si kweli; ndoa nyingi tu zinafungwa bila vipimo. inategemea ni kanisa gani, ila makanisa menge hakuna hii condition.
 
Sijampotosha soma vizuri comments zangu. kama anaona ni vyema mchumba akajua, basi wa kusema ni dada yake na si yeye kama kama. ajaribu kum convince dada yake aweze kuongea na mchumba wake kuhusu status yake kama uwezo huo anao. kama dada hataki, basi akae mbali. kua na ukimwi haimaanishi unakufa kesho. dunia ya leo asojua ukimwi ni nani. watu walipanic siku za nyuma valikua hawaujua vizuri. sasa hivi hata wenye virusi wanazaa tena very healthy kids kupita wewe unayejiona una afya njema.

kwa hiyo kama kuwa na ukimwi hakumaanishi kufa leo au kesho ndo sababu ya maana ya kumfanya mtu anyamaze jamaa akaupewe tu kwa kuwa hatakufa leo au kesho??? athari za vvu unaziona kwenye kifo tu huzioni kwenye sex ambayo ndo kiungo cha ndoa, wala kwenye uzazi ambao ndo lengo la ndoa, wala kwenye gharama na muda wa matibabu. Jamaa aambiwe tu. haya mambo unayoyasema hapa hata huyo bwana arusi mtarajiwa anayajua kwa hiyo ataamua mwenyewe.

ukivunja sheria kwa nia ya kuokoa maisha hauhukumiwi. uhai wa mtu una thamani. unasema dada mtu aendelee kushawishiwa amwambie mchumba mwenyewe, na akikataa kaka mtu ajitoe kwenye mchakato!! akijitoa kwenye mchakato itafuta akilini mwake kuwa alikuwa anajua ila akanyamaza kwa kuwa haolewi yeye? kama muoaji atamuona shemeji yake kuwa ni muongo na fisadi kuna shida gani? zitakuwa ndo gharama zake za kusema ukweli. hatakuwa amepoteza kitu zaidi ya guilty aliyo nayo sahivi.
 
kama ww ni mwanaume halisi na una roho ya kibinadamu, una maumivu ya kweli fanya lolote ni bora kuwa mkweli na uchukiwe na watu woteeeeeeee,
plz ukoa nafsi ya shemu wako damu yake itakulilia kama ndugu wengine wamesusa ww sema. na mungu abariki tuu. na nina imani kama ni walokole wa kweli naiman hawaja nanihiana nyeti zao.
kazana wala usiogope jiwekee hazina kwa mungu. i wish u the best
 
Hayo yao wenyewe hayakuhusu yaache kama yalivo.

na ww mgonjwa una roho mabay eti hayakuhusu. just take example kama nyumba yao imeungua na yeye yuko karibu hataruhisiwa kwenda kuokoa????? WATU WENGINE SJUI WAKOJE cjui ata una principle gan labda za kunya tyuu.
 
ndugu yangu nimesoma kwa masikitiko sana hii habari yako nachokuomba ni bora uende kumwambia hilo suala kwani akijakugundua wakati amefunga ndoa na huyo ndada yako atawachukia mara 7 kwani ni afadhali uiponye afya ya shemeji yenu mtarajiwa mapema kabla ya majanga kuwepo kuliko kunyamaaza na kuendelea kula hela zake huku mkishekisheki kiaina sio vyema ni bora ajuue mapema labda eyeye mwenyewe ndo akubaliane na hali hiyo huku mkiwa tayari mmeshawmwambia juu ya jambo hilo



Habari zenu wana Jf,

Nina mdogo wangu wa kike baba mmoja ila mama ndio tofauti, mzee alikua na wake wawili.Huyu binti alikua akifanya biashara za kusafiri kwenda Kampala na nairobi kwa miaka mingi, ni mdogo wangu wa nne kuzaliwa, tupo Tisa kwa hao mama wawili, ila mama zetu hawapo duniani, mzee ndio bado yupo katika hizi safari za kibiashara bahati mbaya akapata ugonjwa huu wa kisasa, aliugua sana hapo katikati, nadhani ilikua 2006-2009.

Baadae akapona akainuka kabisa kutoka kitandani lakini akaambiwa asiache dawa za kurefusha maisha, tukamzuia kuendelea na hizo business za kusafiri, akaokoka na bado anaabudu hadi sasa, amenona hasa, amekua kipande cha mtu.Simzungumzi vibaya Dada yangu, ila kwa kweli amekua na wowowo lenye kumvutia mwanaume yeyote yule.

Nadhani ni katika muonekano huo ndipo akajitokeza mlokole mwenzie huko kanisani kwao kutaka kumuoa, huyo jamaa kachanganyikiwa na yuko resi mno, ameshaniletea barua nami nikaipokea pamoja na wenzangu, baadae tukamtajia mshenga wake mahari nayo akalipa na tulishaila, tuligawana makaka, nae binti tukampa kidogo.

Sisi hatujaanza utaratibu wa vikao ila wao upande wa jamaa walikaa vikao viwili tayari, wakati wote huu mimi nilidhani dada alishamweleza status yake huyu mchumba, na pengine nikadhani wote wana status hiyo hiyo ya HIV positive wameamua ku team up kuunda familia, kumbe sivyo huyu jamaa hajui chochote kuhusu hali ya huyu dada yangu.

Kuna dada yetu mkubwa aliempeleka kanisani huyu binti na wanasali pamoja, juzi alimuuliza muolewaji kama amemwambia mchumba hali yake, akajibu hajamwambia, anaogopa akimwambia atakosa ndoa, na yeye anahitaji kuwa na familia yake kama mwanamke, na kwamba yeye mwenyewe haachiwe jambo hilo atalimaliza mwenyewe, na kwamba tusimwambie mchumba chochote.

Roho yangu inanisuta sana kushiriki jambo hili, hasa ukichukulia kuwa nyumba na mji wangu ndio unaochukuliwa kama nyumbani kwao na bibi harusi, na tupo karibu sana kimawasiliano na huyo jamaa.Mfano ni juzi tu kanitumia laki mbili akisema ni ya chai.

Pia ni msomi mwenye carrier yake na future inayoeleweka, hivyo nafsi inanisuta, wenzangu wanadai afya za maharusi sio kazi yetu, kwamba sie kazi yetu ni kusherekea tu, kwamba ni miaka sasa hatujawa na harusi tunachangia watu tu

Wadau, nahitaji msaada wa mawazo

Au na mimi nipotezee tu watajuana wenyewe?
 
yaan hii story imefanya nimuwaze sana demu wangu ambaye ni shemeji yenu

venye alivyonona na kavu nyingi full kuzama mpaka chumvini Daaaaaamn!!
 
hii nchi ndio maana haina maendeleo halafu tunasema tunataka mabadiliko. yatoke wapi ikiwa mtu badala ya kufikiria mambo ya maendeleo au yanayomhusu yeye na yenye kumletelea maendeleo yeye na familia yake kama anayo, yuko busy kupasua kichwa jinsi ya kusambaratisha mahusiano ya watu... aisee... nimechoka kabisa... Haya namtakia kila la heri Baraka tele Navin-Govind katika harakati zake za kuvunja mahusiano ya dada yake ili amuokoe seheje. Asiache kutuletea mrejesho reaction ya dada yake na shemeji yake. maana nahisi dada yake atakua adui yake hadi anaingia kaburini (damu yake) na huyu wa kuja (shemeji) atakua best yake milele maana umemuokoa asife, vile na yeye hutakufa kwa kua hana ukimwi.
kwa hiyo kama kuwa na ukimwi hakumaanishi kufa leo au kesho ndo sababu ya maana ya kumfanya mtu anyamaze jamaa akaupewe tu kwa kuwa hatakufa leo au kesho??? athari za vvu unaziona kwenye kifo tu huzioni kwenye sex ambayo ndo kiungo cha ndoa, wala kwenye uzazi ambao ndo lengo la ndoa, wala kwenye gharama na muda wa matibabu. Jamaa aambiwe tu. haya mambo unayoyasema hapa hata huyo bwana arusi mtarajiwa anayajua kwa hiyo ataamua mwenyewe.

ukivunja sheria kwa nia ya kuokoa maisha hauhukumiwi. uhai wa mtu una thamani. unasema dada mtu aendelee kushawishiwa amwambie mchumba mwenyewe, na akikataa kaka mtu ajitoe kwenye mchakato!! akijitoa kwenye mchakato itafuta akilini mwake kuwa alikuwa anajua ila akanyamaza kwa kuwa haolewi yeye? kama muoaji atamuona shemeji yake kuwa ni muongo na fisadi kuna shida gani? zitakuwa ndo gharama zake za kusema ukweli. hatakuwa amepoteza kitu zaidi ya guilty aliyo nayo sahivi.
 
Bro..kama huyo dada tayari anatumia ARV uwezekano wa kumwambukiza huyo broo ni mdogo mno...ARV hushusha viral load kiasi ambacho kidaktari tunaita undetectable..katika level hiyo wanaweza kuoana wakazaa watoto na kuwalea na jamaa akabaki kuwa negative tu
 
Hivi ule utaratibu wa walokole kupelekwa na mzee wa kanisa kupima afya na mimba kabla ya ndoa haupo kwenye makanisa mengine? Mimi nakumbuka mke wangu (wakati huo mchumba) alipmwa ujauzito mbele ya mjumbe aliyeteuliwa na kanisa..na baadaye mimi na yeye tulipelekwa hospitali na mjumbe wa kanisa kupimwa maambukizi ya HIV.

Kama kanisani kwao hawana huo utaratibu, na kama kweli hajamfahamisha itakuwa busara kama ukihakikisha jamaa amepata taarifa. Ingekuwa vema kama dada yako angesema mwenyewe, ila yaelekea ameipania ndoa hasa wala hawezi kusema. Hata hivyo sioni kama kutakuwa na ndoa yenye afya baada ya jamaa kugundua kuwa ameoa mwathirika ambaye kwa makusudi kabisa ameamua kuwa kimya na kumwambukiza ugonjwa huo. Kuna hatari ndoa ikavunjika mapema sana na jamaa kuchanganyikiwa au hata kujidhuru.

Yawezekana dada yako anataka tu hadhi ya kuwa na ndoa, kwa maana kwamba hata ikivunjika baada ya siku 2 angalau na yeye atakuwa ameimbiwa "anameremeta", otherwise, sioni ndoa ya kudumu katika mazingira yenye usiri wenye nia ovu kama hiyo.

Kama unaogopa kumwambia shemejio moja kwa moja, tengeneza mazingira ya kijasusi uhakikishe anapata "anonymous message" kumtahadharisha na kusisitiza amwombe mwenzie wakapimwe afya zao kwa ujumla. Kwa vyovyote vile, reaction itakayofuatia baada ya pendekezo hilo itatosha ku-solve kesi hiyo.

this is very wise
 
ushauri wangu ni kua tatizo la dada yako ni lake na ni maisha yake na huyo mchumba wake. si jukumu lako wewe kuingilia mambo yasiyokuhusu. Jali maisha yako na waache waendelee. Jiweke kwenye nafasi ya dada yako, halafu dada yako angeenda kusema kwa mchumba wako status yako, how would you feel.... Kama ni lazima usaidie, jitahidi kumuongoza dada yako a built ujasiri wa kumwambia mchumba wake yeye mwenyewe na sio wewe ndio uwe msemaji. Ukimwi sio ugojwa kama cancer na diabetes bali ni mfumo kubadilika mwilini. wewe mwenye kiherehere unaweza ukaondoka duniani kwa jambo dogo sana ukawaacha wakaendelea kuishi miaka mingini 20 na watoto wenye afya tele. achana na hii kitu, its too personal. nyinyi kama familia endeleeni na maandalizi ya harusi wala msizungumzie hili jambo maana si lenu bali ni la dada yenu, atajua mwenyewe jinsi ya kulitatua kwa mchumba wake. kwanini uumie moyoni kwa jambo ambalo si lako. binadamu tuna mambo ya ajabu sana. Kabla hawajaamua kuoana ilikua ni jukumu lao wenyewe kuamua kwenda kucheki afya zao maana mwisho wa siku ni kwa maisha mazuri, sasa kama hawakufikiria hilo wewe nini wa kutaka kuropoka. incase unamwambia halafu asikuamini akakuona unamfanyia roho mbaya hasa kwa kuhisi unaharibu kwa vile ni ndugu wa kambo, utajisikiaje? kama si aibu iliyokithiri. waache na maisha yao, na wewe endelea na ya kwako.

mmhhh...da asia
 
Kama habari hii ni ya kweli basi hata mimi napendekeza huyo mwanaume aambiwe ukweli na ikibidi wakacheck afya zao pamoja.
Lakini pamoja na hayo yote niseme tu Watanzania tulio wengi hatuna ufahamu wa tatizo hili la HIV...kuna watu hawajui tofauti ya ukimwi na HIV. Niseme tu kuwa namshukuru sana mwenyezi Mungu nimeweza kulielewa tatizo hili au ugonjwa huu kutokana na kuwa jirani na watu walio kwenye tatizo hili(siiti ugonjwa maana na mimi nitakuwa kama mlivyo baadhi yenu bali naliita ni tatizo la kawaida tu kama ilivyo malalia au maradhi mengine) kiukweli watanzania asilimia 95 hatuna uelewa na swala hili...tumejazwa hofu na hisia mbaya tu. Ukweli ni kwamba unaweza ishi na VVU kwa mda mrefu sana tena ukiwa kwenye afya njema kabisa iwapo CD4 zako hazipo chini ya 500 au 400 bira kutumia ARV na ukaishi bila hofu yeyote.

Na ikiwa CD4 zako ziko chini ya 400 basi unaweza kuanza kutumia dawa za ARV ambazo zitaendana na mfumo wa mwili wako na ukaishi maisha marefu na yenye furaha ila hakikisha unakula chakula bora,kunywa maji safi na salama na uwe unafanya mazoezi hata mara 3 kwa wiki. Lakini watanzania tuliowengi ni rahisi tuwapo hospital na doctor akakuambia una Cancer au Kisukari ukatoka hapo huku unafurahi lakini ukiambiwa unamaambukizi ya VVU au HIV basi unaanza kulia na kuona hii Dunia siyo yako tena...lakini ungeambiwa una cancer au kisukari basi ungeona hii dunia bado ni ya kwako na hauwezi kufa.
Sisemi kama HIV siyo tatizo ila nasema HIV siyo tatizo kubwa kama ambavyo Wabongo tunavyolichukulia ki hisia za kufirikika. Miaka 20 iliyopita HIV ilikuwa ni kweli hukumu ya Kifo...ila sasa baada ya elimu nyingi na hizi dawa za kila aina sasa HIV siyo hukumu ya kifo tena.

Hebu tujiulize maswali haya: mbona siku hizi yale mabango makubwa makubwa barabarani yahusio HIV au matangazo ya salama condom kwenye mativii na radio mbona hatuyasikii tena?. Ila tuwe makini ni kweli HIV ipo na inaambukiza...ila tusiione HIV kama ni hukumu ya kifo kama miaka 20 iliyopita! Noo!!
 
hata ukimwambia itakua ni kazi bure maana jamaa atakua keshamvua chupi huyo mgonjwa siku nyingi sana.

teh teh t:msela:
Wenzio ni walokole bhaaaanaaaaa hawafanyagi huo mchezo b4 ndoa.
 
Back
Top Bottom