Dada yetu anaishi na Virusi vya UKIMWI, tumwambie ukweli mchumba wake?

Fanya maamuzi magumu,umuokoe huyo jamaa hata km dada yako atakuchukia lkn elewa kuwa mbele ya Mungu upo sahihi.
 
Tena usipoteze muda jamaa yangu,kamwambie leo hii. Kama unaogopa mwambie mtu mwingine mpigieni hata simu kwa kutumia simu ya mtu mwingine. Jiulize je ingekuwa ni wewe? Usipomwambia utakuwa umeshiriki moja kwa moja kuchinja mtu. Tena wewe ndio zambi yako itakuwa juu ya wengine wote,ksbb una uelewa tofauti na hao. Ukimwambia thawabu yako ipo
 
Mmmh
 
 
 
Ukisema ni vizuri ila huyo dada hamtaelewana tena.

Halafu huyo muoaji kama yuko huku atakuwa ameshajijua
 
Waachie wenyewe
Ukimwi sikuhizi wakawaida sna
Weweeee....! Usidanganye watu. Usifanye mtu aambukizwe kienyeji hivi. Mimi tu najijua nikiupata leo,kesho tu naweza nikafa. Kuna wengine nyie ni never mind,lakini wengi ni waoga kama mimi
 
Ni rahisi sana cha kufanya. Wewe muulize muoaji katika maongezi je mmepima? Mwambie Ni vizuri sana mchukue hatua ya kwanza mkapime pamoja. Kama umeshindwa kwa huyo mwambie hata Mchungaji wake atakaewafungisha ndoa. Muombe awashinikize kwamza wakapime pamoja kabla ya chochote.

Hapo utakuwa umefanya kwa nafasi yako. Vinginevyo usipotanya hivyo hivyo itakutesa hiyoaisha yako yote. Wewe tulia waza chukua nafasi ya huyo kijana. Piga picha hiyo.
Japo huyo muoaji nae mzembe kweli utajitwishaje kiholela hivyo bila kupima kwanza?
 
Fikisha taarifa kwa mchungaji wao, iwe ni taarifa ya siri, na mchungaji atambue niaa njema uliyonayo, ili kwa utaratibu sahihi taarifa imfikie shemeji yako matarajiwa kwa njia nzuri na isiyo na emotional damge.

Makanisani wana utaratibu wa kuhakikisha afya za wanandoa, watajua njia sahihi ya kuzungumza nao kwa kabla ya ndo yao. Hapo utakuwa umemsaidia shemeji yako na dada yako.
 
=
Thread ni ya 2015. Mleta mada kama bado yuko hapa JF, alete mrejesho kulindaje.
 
Mnaingilia business za watu wazima zisizowahusu, waacheni wamalizane wenyewe na 99% chance jamaa kishakula kavu, na ukimwi sio murder watu wanaishi maisha ya kawaida mpaka wanazeeka, kama ni lazima sana ongea na dada yako lakini sio jamaa
 
Hayo maswala ya magonjwa na mahusiano ni very private, na kitaalam mtu anayetumia dawa vizuri hawezi kuambukiza inategemea na viral load, mtu mwenye virusi ana haki na uwezo wa kuingia kwenye mahusiano kama mtu mwingine, na akazaa mtoto negative na asimuambukize mtu mwenza
 
Mm dada yangu anakula Dozi na.kunajamaa kamuoa hivyohivyo ilibidi niulize jamaa anajua status ya sister wanasema anajua eeehhh kumbe kinawamba wanajilipua tu!! Jamaa aambeie ukweli harafu aamue mwenyewe
 
Leo ni 2024 tupe mrejesho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…