Dada zangu jitazameni upya, thamani yenu ni kubwa

Dada zangu jitazameni upya, thamani yenu ni kubwa

Mimi nisiwe mnafiki , na enjoy sanaaa nikiona mrembo kajaliwa kapiga dress tight ya mpira, au mini skirt fulani au skin jeans! Yaani naburudika sana endeleeni kutubariki keep flaunting what God gave u..
 
Well said... But kila kukicha mnasema wadada wa watu tu nyie wakaka mbna hamjisem whil mna mapungufu meng.... Mtuwacheeee
 
Wemimiaid... But kila kukicha mnasema wadada wa watu tu nyie wakaka mbna hamjisem whil mna mapungufu meng.... Mtuwacheeee
Thamani yenu ni kubwa kwenye jamii, pasipokuwepo mimi bila uwepo wenu. Itunzeni thamani yenu
 
Thanks again ibra87

Pumzika kwa amani swahiba.
 
Thamani yenu ni kubwa kwenye jamii, pasipokuwepo mimi bila uwepo wenu. Itunzeni thamani yenu
Umeondoka ukiwaachia mama na dada zetu nasaha thabiti.

Pumzika kwa Amani Ibra87
 
Nimejikuta nawaza nitaacha kitu gani kwenye kurasa zangu au post zangu kwenye mitandao ya kijamii nitakapokufa. Facebook page yangu itakuwa na post gani? Instagram, Twitter na mitandao mingine!! Michango yangu na threads zangu humu JF zitakuwaje?


Je sitatamani kumuomba malaika dakika chache za angalau kuedit baadhi ya vitu? Maana nadhani kila kitu kitabakia kama kilivyo, ikiwa ni aibu ndugu au watoto wangu watalazimika kukabiliana nayo; na kama ni mambo ya hekima basi watafurahi na kujifunza.

Ingewezekana kungekuwa na button mtu unabonyeza unapokufa inazima profile zako zote kwenye social network!!

Just thinking and typing!!
 
Wasalaam wanajukwa..

Ni kipindi kirefu sijajitokeza hapa kuandika kitu chochote kinachohusu mapenzi, uhusiano na urafiki. Sio kwamba nilikuwa siingii na kusoma, la hasha, nilikuwa nikiingia nakusoma kama kawaida na kuchangia kwa uchache sana. Ndugu zangu sitaki kuongelea kilichonitokea mwishoni mwa mwaka uliopita kwa kuwa ilikuwa ni mipango ya Mwenyezi Mungu. Nimeshukuru, nimeinuka na pia najaribu kutembea tena. Kwa hili nasema Ahsante Mungu.

Ndugu zangu wanajamii wenzangu, nipo hapa leo kuzungumza na dada zangu, mama zangu, shangazi na hata wadogo zangu. Ni ukweli usiopingika kwamba nyie ni mama zetu, shangazi zetu na dada zetu.

Ni ukweli usiofichika kwamba mnathamani kubwa kwenye jamii yetu kuliko hata sisi wanaume. Licha ya thamani kubwa mlionayo na ile tunayoendelea kuwapa lakini mmekuwa watu wa ajabu sana.

Dada zangu na mama zangu, maungo yenu yanathamani sana, nguo zenu za ndani zinathamani sana. Shanga zenu na hata tight zenu zinathamani sana. Hazipaswi kuonekana machoni mwetu, hazipaswi kuonekana hata kwa watoto wadogo. Lakini hili ni tofauti kwenu.

Unamkuta mama mwenye miaka hamsini amevaa gauni la mpira linalouchora mwili wake na kusababisha mpaka hata mistari ya nguo kuonekana. Una mkuta mdada amevaa nguo fupi mpaka magotini huku ndani akiwa hana chupi au kama anachupi ile ya mikanda (bikini)

Harafu kibaya zaidi, licha ya kujua nguo mnazovaa ni fupi, lakini mnajilazimisha kukaa huku mmeichanua miguu yenu. Wengine unakuta urembo wa kiunoni umetokeza lakini bila kuijali thamani yake, bila kujali jamii inavyomchukulia, anatembea bila kujistiri.

Dada zangu thamani yenu ni kubwa sana kwa jamii yetu. Ni mwanaume gani ambaye atakupenda kwa kukukuta ukitembea uchi mtaani. Ni mwanaume gani atakayekupenda wakati amekukuta ukiwa nusu kahaba?

Ni wakati wa kubadilika, ni wakati wa kujitambua ili muonekane ni wanawake wa kweli. Ukimkalia uchi mwanaume sio sababu ya kukuoa. Ndio maana wengine huwapa mimba na kukimbia sana kisha mnabaki wenyewe mkilea watoto na kupewa majina ya ajabu (single mothers).

Jaribuni kubadilika mama zangu, jaribu kubadilika shangazi zangu, jaribuni kubadilika dada zangu.

JITAZAMENI UPYA THAMANI YENU NI KUBWA SANA KWA JAMII.

Naomba kuwasilisha
Rip
 
Back
Top Bottom