Dada Zetu/Mashemeji: Mnaachika kwasababu ya Wana/Washkaji wa Mabwana zenu

Rorscharch

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2013
Posts
1,435
Reaction score
3,120
Mabinti, Madada na Mishangazi... Sikilizeni Kidogo

Siku hizi mtu akikutambulisha kwa washikaji wake, usijidanganye kwamba kila mmoja atakushangilia. Hasa ukikosa kisura cha kuvutia, macho yao ni kama CCTV — wanakuchunguza juu hadi chini, kisha maneno yao nyuma ya pazia ni ya kashfa tupu.

Juzi kati, jamaa mmoja kamleta demu wake kwa washikaji. Alivyoondoka tu, mmoja wao akasema:
"Yaani mimi mzuri kuliko hata demu wako... bora hata ungenitongoza mimi!"

Sasa tafakari hapo. Huyo jamaa alimpenda demu wake kweli, lakini washkaji wakaanza kumdhalilisha kwa sababu mpenzi wake si ‘miss’ wa Instagram. Madongo ya hila yakaanza:

"Mbona huyu hakufai?"
"Ulimtoa wapi?"
"Yaani umejishushia hadhi bro!"
" Unatembea na Nungunungu?"

Na mara nyingine, kwa presha hiyo hiyo ya maneno, jamaa anaanza kukupotezea. Si kwa sababu hakupendi — la hasha! Ni kwa sababu washkaji wake hawajaona ‘brand’ wanayoamini inafaa kutambulishwa.

Ukweli?
Kama mwanaume anakutambulisha bila hofu, jua huyo anakuthamini zaidi ya sura. Na kama washikaji wake wanamchoma nyuma yako, ni wao wana shida — si wewe.

Kwa hiyo dada, usiwe na wasiwasi kama walivyokuwa wanagawa urembo huko mbinguni wewe ulichelewa kwenye foleni basi ujue Kuna wanaume nao walifanya makosa kama Yako
 
Uzi wa Zanzibar!
 
Back
Top Bottom