kilaboy
Senior Member
- Dec 11, 2011
- 150
- 97
Habari zenu wana jamvi, ni matumaini yangu kuwa nyote mu wazima.
Ninakuja hapa kwanza kakutoa shukrani kwa wadau mbalimbali ambao hutoa michango yao ya kitabibu ambayo imekua msaada mkubwa sana kwangu.
Pili leo nikiwa katika pita pita zangu nimekutana na muuza madafu akiwa na ndimu kwa pembeni.
Baada ya kuagiza dafu akaniuliza vipi kiongozi unahitaji kwa ajili ya kutibu UTI?
Hapo ikabidi nimdadisi zaidi anamaanisha nini?
Ndipo akanieleza kua ili uweze kutibu ugojwa huo bila dawa za hospitali basi unatakiwa ule madafu mawili kwa siku na kila dafu unalikamulia ndimu moja, na dozi hii unaitumia kwa muda wa siku tatu hadi saba.
Sasa wanajamvi ninakuja kwenu ili tupeane uzoefu na kama kuna mwenye ufahamu juu ya hili.
Naomba kuwasilisha.
Sent using Jamii Forums mobile app