The dumb Professor
JF-Expert Member
- Dec 10, 2023
- 852
- 1,978
Hawayuu wasomi wenzangu,
Leo katika harakati zangu za hapa na pale za kutafuta mkate wa siku wakati natoka kufundisha subtopic ya quantum tunneling pale UD.
Nikadandia daladala moja ya kwenda Mbezi, ilikuwa imeshona mno na kulikuwa na kafoleni kimtindo. Mimi nlikosa siti nkawa nimenin'ginia mlangoni.
Nikajiangalia kwa urefu wangu na suti niliovaa haifai kusimama wakati kuna malofa tu wamekaa. Nkamcheki jamaa mmoja alokaa nikamwambia aniachie siti nimpe elfu 10.
Jamaa akagoma akaona kama namfanyia dharau, nikamwambia kavipi basi nakupa 20K jamaa bado akakaza. Nikapanda dau nikamwabia basi nakupa 30k jamaa amekaza tu.
Si akaanza kupayuka daladala nzima na kunishushua kuwa nina dharau eti yeye ana hela ana uwezo wa kuninunua mimi na ukoo wetu wote, anasema eti ana uwezo wa kuinunua daladala yote na abiria wote mpaka dereva tukashuka.
Katika hayo maongezi yake nikamsoma lafudhi jamaa ni wa kanda ya shomile.
Dah hawa jamaa kumbe ndo wana dharau hivi. dah kumbe hawasingiziwi mazee.
Ikabidi tu nishuke pale kwa aibu kabla ya kituo changu maana sio kwa kushushuliwa vile.