Dah, ila ndoto zingine; sasa kuota unakula chakula juu ya choo ndo nini tena hiki?!!!!!

WhoWeBe

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2022
Posts
2,299
Reaction score
4,282
Imenitokea hivi punde tu. Nilijikuta napata chakula juu ya ukuta wa choo kilichowazi. Ajabu ni kuwa chakula chenyewe nimenunua kwa mama n'tilie anayeuzia nyumbani kwake na hapo juu ya choo ndipo nilipojikuta nimechagua kukaa.

Yaani nimeamka ghafla hapa, hata sielewi. Hata habari za makolo KUTOLEWA MBALI HUKO nimezisahau kwa muda.
 
Maana ya ndoto hii ni kuwa una/utapata hasara kwa shughuli unayofanya. Au pia unafanya kazi bure wanasema kuweka maji kwenye gunia. Angalia shughuli na mipango yako na uwe makini ikiwezekana sitisha mipango yako ya hivi karibuni hadi utakapojiridhisha kuwa upo sawa ndio uendelee.
 
Choo ni jela mkuu

Kule hawanyimi watu chakula
 
Usile kwa mama lishe wanaweka mpaka kinyesi kwa maelekezo ya mganga

Na wewe ni mteja
 
Daresaalam kuna kipindupindu
maana yake utapata kipindupindu
 
Inakadiliwa Binadamu kwa usiku mmoja uota ndoto zipatazo elfu 1000 tofauti tofauti ila huwezi kuzikumbuka zote maana zinakuwa ni fupi nyingine mara nyingi unakumbuka ndoto ya mwisho mara uliposhtuka toka usingizini.

Kifupi ni kwa kwamba akili ya binadamu inakuwa active sana ukiwa umelala kuliko ukiwa macho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…