Dah! Tembea uyaone, sikujua barabara za Kenya zimeboreshwa kiasi hiki

Dah! Tembea uyaone, sikujua barabara za Kenya zimeboreshwa kiasi hiki

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Mgala muue, haki umpe! Jameni aliyekua rais wa Kenya bwana Uhuru Kenyatta hata kama ana mapungufu mengine lakini kwenye hili nampa hongera za dhati. Nina miaka mingi sijasafiri, ila jana nimekatiza kutokea gatuzi za Magharibi hadi Nairobi, barabara zimetanuliwa na kuboreshwa aki ya nani mpaka raha tu yaani, nilijikuta nashangaa kote kote, halafu unafika mjini na kupepea juu ya Expressway. Nimejikuta mshamba kwenye hii nchi.

Halafu Wakenya wamewekeza pembezoni kote, nimeona majengo yanaibuka kila mahali, mbona hii nchi kama inaserebuka vile, tuendelee vivi hivi, muheshimiwa daktari Ruto nakurai uendeleze haya yote na kuyadumisha.... shukrani sana.
 
Back
Top Bottom