Dah. . .wanawake wengine bana!!!

Dah. . .wanawake wengine bana!!!

hilo ni onyo kwa kina canta na wale wote ambao hawajaolewa..

Ndetichia like this

Ndetichia embu na nyie muwe mnachukua muda kujua mwanamke mnaetaka kumfanya mke ni wa aina gani msije mkalazwa nje/njaa.
 
Lizzy tegemea kutokuchangiwa siku ukioa/kuolewa au utakuwa tayari umeoa/olewa?

Nichangiwe ya kazi gani?
Hiyo harusi itaendana na uwezo tulionao mimi, mwenzangu na familia zetu. Kama ni wa chai na maandazi, basi ndicho watakachoambulia waalikwa, kama ni kulisha pilau watu 20 basi wataalikwa hao tu.
 
Last edited by a moderator:
Lizzy safi sana maneno yako ukweli mtupu.
 
I will be right back, namvaibret boss kwa hisani ya gfsonwin.
 
hahahaha lizzy ni kweli kabisa wanawake wengi tunachangia hayo mambo,hata kama hana kazi but alipaswa kuridhika na kile alichojitahidi mwenzie kukileta nyumbani,kwa mwanamke mwenye akili angepikia hata kuni ama kukopa mkaa kwa siri ili kum2nzia mumewe heshima sio kumnyima chakula alichokitolea jasho.ningekua namjua huyo baba ningemtafutia dogo dogo lol

Mie wa kwangu hanipi chochote, hata gari yake nkitaka kupanda lazima niweke mafuta kwanza, lakini NAMPENDA tuu, tena sana. Na nikipika chakula kitamu, lazima yeye ale wa kwanza, lol. What a loving wife i am, tehe.
 
Sasa wiki iliyopita alimuomba mumewe pesa ya mkaa, mume akawa hana. Alichofanya ni kwamba amemnyima chakula (anachonunua huyo huyo mume) mpaka leo hii. Yani "kwa eaha na shida (siku hizi inabidi mchungaji akisema . . . . na shida waseme "INATEGEMEA NI ZIPI" badala ya "NDIO NAKUBALI" za kinafiki) aliyotamka imekosa matendo.

.

sasa kama aliomba mkaa ili aweze kumpikia huyo mume wake na mume amekataa kuleta mkaa sa apikie kutumia nini?? hapo naona fair game
 
kweli ndio maana nyumba ndogo haziwezi kupigwa stop, wanaume embu fungueni macho sio mteswe halafu mseme mnavumilia ndoa
 
..........
Ahhhhh wanaume wengine mna kazi kweli aisee. . .nawapa pole wote mnaokaribia kupewa vichaa na wake/wapenzi wenu.

hivi ndoa yaweza kumfanya mtu achizike eenh?
kweli Mungu tusaidie makapera na waseja lol
 
1. Je ni kweli huyo mume alikua hana pesa? (2.) hakuna mazingira yoyote aliyoyaonyesha kuwa alifanya kusudi kumnyima mkewe hela mf. Kaja nyumbani kalewa? (3) hiyo ni mara ya kwanza kushindwa kumpa mkewe hela ya matumizi?
 
Kwa wale ambao bado hawajaolewa hua hawaishi kuonyesha na kuelezea namna gani wanaume walivyo wabaya hata kufanya swala zima la kuingia ndoani kuwa gumu. Walioolewa hawaishi kulalama namna waume zao walivyo wabaya ndoani hata kuona ndoa zao hazina furaha. Ila wote wanasahau kwamba kwa kiasi kikubwa wengi hua wanachangia ubaya wauonao kwa wanaume kama ambavyo wanaume huchangia ubaya (sio wote) wauonao kwa wanawake.

Kuna dada kaolewa miaka minne(4) iliyopita, na harusi yake ndo harusi pekee ambayo mimi nimewahi kuhidhuria mpaka leo hii. . .

Sina shaka kwamba alikubali mwenyewe kuolewa na siku ile aliifurahia maana alionekana mwenye furaha muda wote. Miaka minne baadae wamejaaliwa mtoto wa kike na maisha yao ni ya kawaida. Sasa wiki iliyopita alimuomba mumewe pesa ya mkaa, mume akawa hana. Alichofanya ni kwamba amemnyima chakula (anachonunua huyo huyo mume) mpaka leo hii. Yani "kwa eaha na shida (siku hizi inabidi mchungaji akisema . . . . na shida waseme "INATEGEMEA NI ZIPI" badala ya "NDIO NAKUBALI" za kinafiki) aliyotamka imekosa matendo.

Sasa mwanamke kama huyu, mume akimbadilikia au akimmwaga atamlaumu nani?Nae ataweza kusimama mahali na kusema wanaume ni watu wabaya? Kwanini asifanye shughuli ndogo ndogo nae awe anasaidia akiona mume mambo hayajamuendea vizuri sana kwenye shughuli zake?

Ahhhhh wanaume wengine mna kazi kweli aisee. . .nawapa pole wote mnaokaribia kupewa vichaa na wake/wapenzi wenu.

Yaani usipokuwa mvumilivu unaweza kumtimua fasta,mimi ishanitokea pesa ipo,mahitaji yapo ndani! kughafirika kidogo,haiingii jikoni kupika.siku nyingine kusuka mpaka usiku mkali asijue hakuna wa kupika nyumbani(msichana wa kazi hakuwepo).nikajiuliza alijua nitakula nywele? ni kweli wakati mwingine wake zetu hufanya vitu vya ajabu,uki react anakuona mbaya
 
1. Je ni kweli huyo mume alikua hana pesa? (2.) hakuna mazingira yoyote aliyoyaonyesha kuwa alifanya kusudi kumnyima mkewe hela mf. Kaja nyumbani kalewa? (3) hiyo ni mara ya kwanza kushindwa kumpa mkewe hela ya matumizi?
vyote hivyo havijalisi unyimwe chakula khaaaa!
 
Yaani usipokuwa mvumilivu unaweza kumtimua fasta,mimi ishanitokea pesa ipo,mahitaji yapo ndani! kughafirika kidogo,haiingii jikoni kupika.siku nyingine kusuka mpaka usiku mkali asijue hakuna wa kupika nyumbani(msichana wa kazi hakuwepo).nikajiuliza alijua nitakula nywele? ni kweli wakati mwingine wake zetu hufanya vitu vya ajabu,uki react anakuona mbaya
ungefukuzia mbali, aende
akaolewe na msusi
 
Lizzy mydia, mwanamke kumuadhibu mumewe kwa kosa ambalo liko nje ya uwezo wake (hana kipato cha kumtosheleza) ni upungufu wa akili kichwani na upendo moyoni. Kama hana anataka akaibe? Na huyo mwanamke hana maarifa ya kufanya akapata mkaa?? hapa ndipo ule usemi mwa mwanamke mpumbavu huibomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe.

Ingawa story yako iko shallow hujatweleza ilikuwaje mpaka mume akashindwa kutoa pesa ya mkaa kwa ajili ya familia yake na je kweli hana uwezo na akili za kuhakikisha kuwa anatimiza majukumu yake kama mume na baba? hasa kwa kuprovide chakula kitu ambacho ni jukumu kubwa kwa familia yake??
 
Mie wa kwangu hanipi chochote, hata gari yake nkitaka kupanda lazima niweke mafuta kwanza, lakini NAMPENDA tuu, tena sana. Na nikipika chakula kitamu, lazima yeye ale wa kwanza, lol. What a loving wife i am, tehe.
Aiseee!!
Kweli ndoa ndoano.
 
sasa kama aliomba mkaa ili aweze kumpikia huyo mume wake na mume amekataa kuleta mkaa sa apikie kutumia nini?? hapo naona fair game
Hicho anachopika na kula yeye anapikia mawe?
 
Back
Top Bottom