Ni vitu vidogo lakini naweza kumuacha wifi yenu
Tunatoka kazini njiani anakwambia leo nimechoka tukae sehemu tununue chakula tule.nikamjibu si vyema tuna kwetu kila siku tule mahotelini(jana yake tumekaa sehemu na kula kisha tukaenda home),tununue tu mboga(mkuu wa meza ) tukasonge na ugali tule,akakubali kumbe alikubali shingo upande.Tukafika sehemu ya kununua mboga nikamwambia mimi nimebanwa nakimbia chooni(choo cha sehemu husika) shika hii hela tangulia kwenye nyama,akakataa akasema kama ni hivyo tuondoke(nafikiri alimaanisha tukae tule pale hivyo hakukubali toka awali),ok nikatii kauli tukaondoka,tulipofika nyumbani akaa kidogo akaingia kulala,nikamfuata vipi kulikoni? akasema hatopika amechoka!kuna msichana ambaye baadhi ya siku huwa anamuagiza kupika,lakini hakumuagiza akaingia tu kulala.nilipomwambia kuhusu kupika akasema huo ni mfumo dume,nikamwambia kama ulikuwa unajua hata kusonga ugali hautaweza sababu umechoka si ungemuagiza msichana apike leo jioni toka hata ukiwa kazini?je ni jukumu langu baba kumwambia msichana apike?wewe si jukumu lako? anasema tungeweza kununua chipsi tule sio lazima msichana apike naye anachoka(kweli ana kazi nyingi ila kumsemea kwamba anachoka mimi inanishangaza). Hivi kupika mwanamke ni jukumu ama ni jambo unaloamua tu ukitaka unapika,ukitaka haupiki? msichana wa kazi akiondoka hauta pika nyumbani itakuwa ni mwendo wa kula hotelini?Je vitabu vyetu vya dini vinasemaje? Nakaribisha maoni yenu hili ni jambo dogo pengine lisilo weza sababisha watu kuachana ila jinsi anvyo li handle ni dhahiri hajui majukumu yake kama mke!Najua wanawake mnaofanya kazi ni wengi je huwa mnazihudumia vipi nyumba zenu?