Dakika 30 za PLO Lumumba zaimaliza NASA ya Odinga mahakamani, wanasheria wa Tanzania jifunzeni kwake jamaa huyu

Nimeamini hakuna Professor anaweza kuwa mtendaji mzuri Lumumba na uprofessor wake ameonekana bogus kufuatia hukumu ya kutengua ushindi wa Kenyatta. Hapa nchini kuna umuhimu wa serikali kuwaacha hawa professors wafundishe vyuo vikuu.
ukishakuwa profesa tu huwa akili inabadilika, unakuwa hauna akili kama za watu wengine.
 
Tatizo letu huwa hatuelewi viashiria vya kuwa mtu ameongea pointi au ucheshi, ukiwa unaongea na watu halafu wakacheka haimaanishi kuwa umeongea kitu cha muhimu na hasa sehemu kama Mahakamani au Kanisani kwenye mahubiri. Nilitarajia kama Lumumba angeongea hoja nzito basi mawakili na wanasheria wenzake wangekuwa wanatingisha vichwa na hiyo ndiyo ingekuwa kiashiria cha uzito wa hoja, lakini walicheka kumaanisha kwamba maneno yake hayakuwa na msingi bali ni burudani ndani ya mahakama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…