masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 18,207
- 13,839
Katika kipindi cha Dakika 45 jioni hii Ndg J Ndugai kwa kweli amenikosha sana.
Amesema yale ambayo wana CCM wengi wanaogopa kusema hadharani, Na amelisema suala la serikali tatu ndani ya muungano bila woga wala kujificha ficha.
Na kuna wakati mwandishi wa habari Selemani Seminyu alionekana akishangaa shgaa kutokana na msimamo huo wa Ndugai.
Ndugai amesema kazi iliyofanywa na wazee wetu hawa Warioba,Salim A Salim na hata kina Palamagamba Kabudi na Prof Baregu na kina Mvungi, wamejitahidi sana kuzunguka nchi nzima kupata maoni ya wananchi katika suala la aina ya muungano wetu.
Kwa hiyo , Ndugai kasema, pendekeo la serikali tatu lina uhalali wake kwa vile miundo mingine inaonekana kutofaa kwa sasa, nakwa vyovyote serikali moja au zile zile mbili hazikubaliki kabisa na wenzetu Wazanzibari.
Sasa hivi kuna bunge la wawakilishi Zanzibar na akasema ni wakati muafaka kuwa na bunge la Tanganyika sasa, na baadaye mfumo mpya wa serikali ya tatu ya muungano.
Binafsi mimi naona ni mawazo ambayo hata wana CCM wa Tanganyika wanayaunga mkono.
Hongera Ndg J Ndugai kwa kutokuwa mnafiki.