Dakika 45: Job Ndugai asisitiza wananchi wafikirie uwezekano wa serikali tatu.


Mkuu hata mimi nilimcheki Ndungai kwenye kipindi cha dk 45 kwa kweli kwa hilo la serikali tatu alinikosha sana. Hakumumunya kama wenzake wa chama chake ambao ukiongelea serikali tatu kuna baadhi mapovu yanawatoka mpaka wanafikiria kuchakachua hicho kipengele. Pamoja na hayo kuna maeneo alikuwa anamumunya maneno kidogo mathalani kuhusu nizamu bungeni na uzalendo eti akasema baadhi ya wabunge si wazalendo wanaleta fujo bungeni na kauacha kutetea maslahi ya taifa. Sasa nikajiuliza hivi hao wanaosemekana walikuwa wakileta fujo si ndo walikuwa wakitetea maslahi ya taifa afu wakaonekana waleta fujo?. Mbali na hilo nilikerwa au huwa nakereka sana na hutu mtangazaji anayeitwa Seleman Semunyu...hafai kwa kipindi kama hicho.....kwanza anaonekana mwoga!...anatetemeka.....si jasiri wakuuliza....Anamuachia sana mzungumzaji hata pale unapohisi mzungumzaji kaongea pumba..kiasi cha kuhitaji kuulizwa kitu atoe ufafanuzi...lakini kwa semunyu hilo halipo!!! tena mara nyingine maswali yake huonekana kama kakaririshwa na watu fulani...yaani kaambiwa ukaulize hivi....na vile! Shame on Him....ITV wafikirie kumwambia a Improve au watafute mtu mwingine kama Rainfred Masako....ndio kipindi kitapendeza.....vinginevyo kitazidi kuwa doroooo!
 
kwa hilo ameongea ukweli ulio moyoni, nina mpongeza na kuunga mkono
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…