Dakika arobaini (40) za Bernard Morrison, Lomalisa mutambala na Shabani Djuma zinatosha kabisa kuwateketeza waarabu (USM Alger) Nyumbani kwao

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Winga msumbufu, winga machachari namba kumi na moja Bernard Morrison (Toto tundu) kutokana na skills zake za kuchezea mpira ndani ya box la mpinzani hakika akipewa dakika arobaini (40) zinamtosha kabisa kufanya maajabu mbele ya waarabu na kuwaacha wakilia kwa machozi ya uchungu.

Beki namba mbili (2) Djuma Shabani kupanda na kushuka pamoja na Kloss zake upigaji wa mpira katika lango la mpinzani Kama ataaminiwa na kocha Nabi dakika arobaini tu zinamtosha kufanya Jambo la msingi na kuleta positive results kwa wanayanga.

Beki namba tatu( 3) Lomalisa mutambala anastahili kupata dakika arobaini (40) za Nabi, ujuzi wa kumwaga majalo ndani ya box la mshambuliaji hakika italeta manufaa kwenye kikosi Cha Nabi endapo atapewa dakika arobaini na Nabi.

Twende Algeria, twende kwa nguvu zote.
 
mwarabu first half atapigwa chuma 0-2,second half 1-1 so FT 1-3......agg 3-4,then baada ya kipenga cha mwisho mashabiki wao wataingia uwanjani kutufanyia vurugu nzito ila kuhusu kombe ndo itakuwa too late.Jumapili asubuhi kutakuwa na habari za vifo vingi sana vya makolo kujiua..REMUNTALEM!!
 
Hizi kelele zenu ndo zilisababisha tuwatumie mvua. Na Jumamosi tunawaletea mvua ya mawe, walengwa ni wachezaji wa Yanga.
 
Mvua inanyesha hapo ulipo? Sio kwa utopolo huo
 
Hata ARV wanasema ni dawa za matumaini
 
Unafikiri Nabi ni mjinga kuliko wewe hadi awaanzishe benchi hao unaowataja? Anajua udhaifu wao. Lomalisa na Djuma wanaruhusu mashambulizi langoni kwa Yanga, hata Mwinyi Zahera alishasema ni wazito kurudi na kwamba wakikutana na mawinga wenye kasi, Yanga inapigwa mabao kadhaa mapema kabisa. Morrison hasaidii kushuka kukaba, na kila akijaribu anafanya faulo inayoongeza hatari langoni. Nabi huyu wa kulinda lango hawezi kuwaanzisha hao katika mechi anayohitaji magoli yasiongezeke
 
Hata kwa kutumia wachawi kutoka Nigeria. Mtu mwenye akili timamu anajua kabisa kuwa mechi iliishia kwa Mkapa, kule ni kwenda kutimiza tu wajibu kwa kutekeleza sheria za CAF.

Hata wakiweka re-match mara 20 Yanga ya sasa haiwezi kuchukuwa point kwa Algers, hata kwa uchawi wa majini. Anyway, kujifarij kwa mgonjwa nayo ni tiba kisaikolojia. Kila la heri Wananchi. Niko paleeeeeee trh 3/6/2023 saa 4:00 usiku.
 
Kama vile waarabu wao hawana kikosi au wataingia watatu uwanjani
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]yaan utadhan hizo dkk 40 ni za yanga pekee yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…