Dakika ya 70 yanga 3 simba 0

Dakika ya 70 yanga 3 simba 0

manchoso

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2011
Posts
1,605
Reaction score
2,055
Mechi hii imechezwa jana majira ya saa 11 alfajir

mechi ilianza kwa kasi na toka mwanzo mwa mchezo Yanga ilitaka kuonyesha umwamba wake mbele ya simba na wakajipatia goli la mapema dakika ya 2 kupitia kwa Bernad Morrison.llilkuwa moja ya magoli matamu kabisa kushuhudiwa ndani ya uwanja wa taifa kwani alianza kutambaa na mpira kwenye chaki na akaingia nao ndani ya box kwa kasi ya swala na kumchambua manula na kuwaacha mabeki wa simba wameduwaa, -0baada ya kuingia goli walilalamika kuwa wakati anatambaa na mpira ulikuwa umeshatoka lakin refa alishaweka kati

hazikupita dakika nyingi ndani ya dakika ya 8 Morrison aliwaliza tena simba kwa goli la pili amabalo lilifanana sana na lile goli la kwanza baada ya kuwafunga tela mabek wa simba akaingia nayo kwenye box na kumtungua manula.baada ya hapo kukawa na kosa za hapa na pale ila kiukweli simba walizidiwa sana na yanga kila idara, kidogo mchezaji alieonyesha uhai ni yule kahata na hata kuna muvu moja alijaribu kuwatoka mabek wa yanga ila alipigwa tackling na mchezaji mmoja wa yanga ambae alionekana ni mdogo sana ila ye sio feitoto, sizani hata kafikisha hata miaka kum kwa umrii kwa kweli nilimuona ni mdogo mno jina lake simjui sura yake ni ngen la nilijua ni kawaida yanga kuibua yoso mahiri walipita pia kina silvatus ibrahim vijana wadogo waliokuwa wakipiga mpira ulioenda shule

Hadi aftertime mbili bila, wakati wa mapumziko nilienda jukwaa la simba nikawa nabadilishana mawazo na mjomba angu shabiki wa simba alietoka morogoro kuja kushuhudia timu yake alikuwa na huzuni sana ila akaniambia wametuachia kwa vile eti washachukua ubingwa, niliwaona pia marafiki zangu kina amos sikuwa najua amos ni mshabiki wa timu gani lakin kwa jinsi alivyonuna nilijua atakuwa simba sababu yanga wote walikuwa na furaha.pia nilijaribu kuangaza bila mafanikio kama ningeweza kumuona yule mzee wa utopolo lakin watu uwanjani walikuwa wengi sana sikuweza kumuona

wakati wa mampumziko nilikaa nikatafakari haya magoli yote mawili yamepitia upande wa kulia wa huyu beki shomari kapombe nikawa najiuliza kapombe leo ana nini?ndo huyu kweli mrithi wa nsajigwa? hakuwa mchezon kabisa kuna wakati alipigwa kibaiskel akaanguka kama gunia la mkaa, mashabiki wa yanga walishangilia sana lile tukio ila mimi lilinihuzunisha

kipindi cha pili kilianza pia kwa kasi huku yanga wakiendelea kulisakama lango la simba amabao hawakuwepo mchezoni kabisaaa na kwenye dakika ya 56 morrison alipenyezewa pasi safi akabaki yeye na manula lakin alipiga shuti kubwa likapaa hewani, pamoja na kukosa hilo goli morrison leo alionyesha uwezo mkubwa ambao ulimshangaza kila mtu alikuwa akiifanya beki ya simba anavyotaka alinikumbusha usiku ule zizzou alivyowatesa wabrazil pale frankfurt au siku ile fernando redondo alipowanyanyasa manchester kwa pasi za kisigino pale uingereza, morrison leo alikuwa na vitu vyote chenga za redondo,akili ya zizzou,stamina ya roberto carlos na akienda hewani alikuwa akipiga vichwa mithili ya jurgen klinsman kwa kweli ilikuwa ni burudani leo kumtazama morrison

kwenye dakika ya 70 nchimbi alimtoka beki wa simba ule ule upande wa kapombe na kupiga shuti kali iliyomshinda aishi manula na kuiandikia yanga goli la tatu, goli hili lilinistua nikapiga kelele nyingi hadi nikaamsha majirani kumbe bhana nilikuwa ndotoni

Ndoto ya leo ilikuwa taamu sana tena nimejilaumu sana kwa nini hili goli la tatu nimepiga kelele sana hadi usingizi ukakata nikaamka ningerelax nadhan ningejionea magoli meng leo tukimtandika mnyama.

NB
Kuna imani inanijia Usiku wa leo ntaota nipo peponi, nimekuwa nikiwaza sana raha za peponi ambazo jicho wala sikio la binadamu haliwahi kuona wala kusikia!!!!Namuomba Mungu anisaidie niote nipo janatul firdaus pepo ya juu kabisa nikiwa na Mitume na watu wema usiku wa leo pia sitashiba sana nisije nikavimbiwa nikashindwa kula vitamu vitamu vya pepon.
 
Haaaa haaa haaaa,nimecheka sana ndoto zako mkuu, kuhusu Mbinguni usiwe na haraka sana, hata ukiishi sana hautaishi miaka 100 toka sasa utakufa tu na kuenda peponi, cha muhimu we angalia tu matendo yako yawe mema na hata mawazo yako yawe mazuri,mawazo ya kiboyaboya huleta ndoto za kiboya kama uliyoota.Acha kuwaza ushubwada utaenda mbinguni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizo ndoto zako ni ishara kwamba kirusi COVID-19 hakitakuacha salama. Anza kuandaa wosia na taratibu za mirathi.
aaah covid kitu gan bhana nimekuwa nikitafuna vitunguu swaum kwa mwaka wa tatu sasa kila siku asubuhi
naamin vitunguu swaumu ni kinga na tiiba ya maradhi mengi
 
Haaaa haaa haaaa,nimecheka sana ndoto zako mkuu, kuhusu Mbinguni usiwe na haraka sana, hata ukiishi sana hautaishi miaka 100 toka sasa utakufa tu na kuenda peponi, cha muhimu we angalia tu matendo yako yawe mema na hata mawazo yako yawe mazuri,mawazo ya kiboyaboya huleta ndoto za kiboya kama uliyoota.Acha kuwaza ushubwada utaenda mbinguni

Sent using Jamii Forums mobile app
ni kweli mkuu inabidi niache ushubwada mbinguni raha aiseee
 
aaah covid kitu gan bhana nimekuwa nikitafuna vitunguu swaum kwa mwaka wa tatu sasa kila siku asubuhi
naamin vitunguu swaumu ni kinga na tiiba ya maradhi mengi
Kumbe corona inaweza kudunda mbele ya kitunguu swaumu eeeh? Ngoja na mimi nianze dozi hiyo.
 
Utopolo kwa kujichekesha

♡♤Life belongs to all who struggle for it♤♡♧
 
Utopolo kwa kujichekesha

♡♤Life belongs to all who struggle for it♤♡♧
hakuna cha utopolo
ndo tushawapiga tatu na burudan nimepata yaaan had raha

yanga baba lao
 
Hii team tokea viongozi hadi mashabiki wana kasoro
Yanga sijui mna matatizo gani, kuanzia mashabiki mpaka uongozi wenu ni upuuzi mtupu.

Sent using Jamii Forums mobile app
tatizo lenu mshazoea ushindi wa miamala afu mnajiona mko juuuu kumbe hamna kitu

huu ni ukweli mchungu ila mkubali mna historia mbaya sana ya kubebwa

yanga ni chama la wastarabu kuanzia viongoz had mashabiki mkibebwa wala hatuvunji viti, tunarudi majumban kwetu tunajifariji namna hii huku mkonon tumeshika tumeshika kikombe cha gahawa
 
89679426_526284518060200_174279520289458046_n.jpg


Mzee wangu aliwahi kunambia
Mwanangu jitahid sana isije siku wanao wakalala na njaa, hata kama huna kitu mambo yakienda mlama vamia hata shamba la watu beba ndizi wapelekee watoto wako wakale, baade ndo utajua huo msala unasolve vipi
Jiandae kwa kupigwa au kudaiwa ila wanao watakuwa wameshashiba

Hayo maelezo ya chini hayana uhusiano wowote na hiyo picha nimemkumbuka tu mzee wangu na wosia wake wa kindezi
 
Hahahaaa. Lol
hawa majirani wana shida sana 🙂 🙂 yaani wanatuonea wivu hata tukiota ndoto nzuri nzuri

na kwa taarifa yao leo nimeota naiangalia saaana mbingu
hiyo ni dalili siku si nyingi ntaota niko mbinguni kabisa
 
Back
Top Bottom