Wakuu
Ama hakika ubunge unatafutwa kwa nguvu zote, tangu 2020 baada ya kuwa wamechaguliwa hatukuwahi sikia wala kuona mikikimikiki ya wabunge majimboni kama ilivyo sasa. Mfano mzuri ni huyu Erick Shigongo, huu muda unatumiwa kulaghai wananchi ili wachaguliwe tena then wanapotea mazima miaka mitano tena. Tusikubaliiii
===
Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo ameweka umeme kwenye zahanati ya Kisiwa cha Soswa iliyopo katika jimbo hilo na kumaliza kero ya muda mrefu ya wanawake kujifungua kwa msaada wa mwanga wa tochi, iliyokuwa ikiwakabili wananchi hao.
Hatua hiyo imepongezwa na wananchi wa Kisiwa cha Soswa ambapo wamesema kuwa ni hatua kubwa ya maendeleo kwenye kisiwa hicho yaliyofanywa na Mbunge Shigongo.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Shigongo amesema hatua hiyo ni mwendelezo wa kutimiza ahadi alizowaahidi wananchi wakati anaomba ridhaa ya kuwatumia.
View attachment 3384659View attachment 3384663