Daktari ahukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kwa kubaka wagonjwa 229

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Mahakama ya Ufaransa imemhukumu kifungo cha miaka 20 jela Joel Le Scouarnec ambaye ni Daktari bingwa wa upasuaji ambaye alikiri Kuwanyanyasa kingono wagonjwa na kubaka wagonjwa 229, wengi wao wakiwa watoto, kwa zaidi ya miongo miwili.

Kesi hiyo iliyodumu kwa miezi mitatu ya Joel Le Scouarnec, mwenye umri wa miaka 74, imefichua ukubwa wa uhalifu wake na mateso ya waathiriwa lakini pia imezusha maswali kwa nini juhudi zaidi hazikufanywa mapema ili kumzuia.

Amepatikana na hatia ya kuwadhulumu kingono na kuwabaka wagonjwa 229 katika kliniki yake mjini Vannes.

Le Scouarnec, mmoja wa wanyanyasaji wakubwa wa kingono waliopatikana na hatia katika historia ya Ufaransa, alikuwa tayari gerezani baada ya kuhukumiwa mwaka 2020 adhabu ya miaka 15 kwa kuwabaka na kuwadhalilisha kingono watoto wanne, wakiwemo wapwa zake wawili.

Hukumu ya miaka 20 jela kwa uhalifu mkubwa wa ubakaji iliyotolewa na hakimu mfawidhi Aude Buresi ndiyo ya juu zaidi ambayo inaweza kutolewa nchini Ufaransa kwa shtaka la ubakaji uliokithiri, ambapo hukumu hazijumuishwi pamoja kwa kila kosa alilofanya.

Le Scouarnec hatakuwa na haki ya kuomba kuondoka jela kabla ya kifungo chake kukamilika, hadi atakapotumikia theluthi mbili ya hukumu yake ambayo ni sawa na miaka 13.
 
229 wengi sana, at74 plus 20 kifungo ngumu sana ! Utalima ulichokipanda
 
Afu muwage na Akili mnatabia ya kuona Kobaz na bikra wao 72 wengiiiii

sasa uyo yupo apa apa Duniani na wanawake 229 toa 72 = 157 acha kuchezea kiumbe wa kiume..!!!!!!!! Yule Batazar 400. toa 72 = 328 ongeza wale awajapiga picha ya video . MWANAUME Jembe. Hatari
 
Mahakama ya Ufaransa imemhukumu kifungo cha miaka 20 jela Joel Le Scouarnec ambaye ni Daktari bingwa wa upasuaji ambaye alikiri Kuwanyanyasa kingono wagonjwa na kubaka wagonjwa 229, wengi wao wakiwa watoto, kwa zaidi ya miongo miwili.

Kesi hiyo iliyodumu kwa miezi mitatu ya Joel Le Scouarnec, mwenye umri wa miaka 74, imefichua ukubwa wa uhalifu wake na mateso ya waathiriwa lakini pia imezusha maswali kwa nini juhudi zaidi hazikufanywa mapema ili kumzuia.

Amepatikana na hatia ya kuwadhulumu kingono na kuwabaka wagonjwa 229 katika kliniki yake mjini Vannes.

Le Scouarnec, mmoja wa wanyanyasaji wakubwa wa kingono waliopatikana na hatia katika historia ya Ufaransa, alikuwa tayari gerezani baada ya kuhukumiwa mwaka 2020 adhabu ya miaka 15 kwa kuwabaka na kuwadhalilisha kingono watoto wanne, wakiwemo wapwa zake wawili.

Hukumu ya miaka 20 jela kwa uhalifu mkubwa wa ubakaji iliyotolewa na hakimu mfawidhi Aude Buresi ndiyo ya juu zaidi ambayo inaweza kutolewa nchini Ufaransa kwa shtaka la ubakaji uliokithiri, ambapo hukumu hazijumuishwi pamoja kwa kila kosa alilofanya.

Le Scouarnec hatakuwa na haki ya kuomba kuondoka jela kabla ya kifungo chake kukamilika, hadi atakapotumikia theluthi mbili ya hukumu yake ambayo ni sawa na miaka 13.
Miaka 13 kwa mwenye umri wa miaka 73 si ni kifungo cha maisha hicho?
 
Duh, jela miaka 20.
Na kama hajatubu, adhabu ya moto wa milele inamngojea.
Hao waliobakwa wangesoma ushuhuda wangu kabla, nafikiri wangepata ujasiri wa kukemea pepo la uzinzi limtoke daktari huyo. Please share ushuhuda huu kwa wasichana/wanawake wajue jinsi ya kufanya wanapokutana na madaktari wazinzi:
 
Kwanini asitubu na washamlegeza makali yake!?
 
Back
Top Bottom