Daktari: Ajali za bodaboda zimeongeza wagonjwa wa kifafa

Daktari: Ajali za bodaboda zimeongeza wagonjwa wa kifafa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
AJALI za bodaboda zinachangia ugonjwa wa kifafa kwa waathirika wa ajali hizo kutokana na majeraha kwenye kichwa ambayo yanaathiri ubongo, imeelezwa.

Hayo yamebainishwa na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Mfumo wa Fahamu na Ubongo kwa watoto, Dk Edward Kija wakati akizungumza katika kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na Televisheni ya Taifa (TBC).

Dk Kija alibainisha kuwa ugonjwa wa kifafa unatokana na athari katika ubongo unaosababisha uwepo wa changamoto ya kuwasiliana na viungo vya mwili.

Alisema ajali ikitokea na dereva au abiria au wote kwa pamoja wakagonga vichwa chini inakuwa rahisi zaidi kwa ubongo wao kuathirika na kusababisha kifafa.

“Imekuwa ni kawaida kwa madereva wa bodaboda au abiria kutumia usafiri huo bila ya kuvaa kofia ngumu huku wengine wakipanda mishikaki huku wakienda kwa mwendo wa kasi,” alisema.

“Hapo kama ajali ikitokea wakagonga vichwa chini, watu hawa wanaweza kuathirika zaidi yaani baada ya kuishia tu kuumia viungo vyao basi watajikuta wakipata hata kifafa, sasa ni muda kwa watumiaji wa bodaboda kuvaa kofia ngumu ili wasije kupata kifafa ajali ikitokea.”

Akizungumzia hali ya sasa ya ugonjwa huo ilivyo hapa nchini, Dk Kija alibainisha kuwa Wilaya ya Mahenge mkoani Morogoro ndiyo inaongoza kwa kuwa na wagonjwa wengi ambapo watu 30 kati ya 100 wanaumwa kifafa.

Kwa takwimu za nchi nzima alisema zinaonesha kwamba kwa kila watu 100, watatu ndio wenye tatizo la kifafa.

Alisema ugonjwa huo unasababishwa na vitu vingi ikiwemo shinikizo la damu kupanda hasa kwa wajawazito huku akiwasihi kujenga utamaduni wa kwenda kliniki kufanya vipimo vya mara kwa mara.

Dk Kija pia amewataka wazazi kuhakikisha wanawalinda watoto dhidi ya ugonjwa wa malaria sugu kwa kuwa inaweza pia kusababisha kifafa.

Pia ameitaka jamii pindi ikimuona mgonjwa wa kifafa ameanguka kuhakikisha anageuzwa ili alalie upande wa kushoto na siyo kumweka kijiko au fimbo mdomoni kama wengi ambavyo wamekuwa wakifanya kwa kuwa kwa kufanya hivyo wanasababisha mgonjwa kushindwa kupumua vizuri na anaweza kufa.

HabariLeo
 
AJALI za bodaboda zinachangia ugonjwa wa kifafa kwa waathirika wa ajali hizo kutokana na majeraha kwenye kichwa ambayo yanaathiri ubongo, imeelezwa.

Hayo yamebainishwa na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Mfumo wa Fahamu na Ubongo kwa watoto, Dk Edward Kija wakati akizungumza katika
Mara kifafa kinachangiwa na kula kitimoto, mara bodaboda..!!!! Dah..!!! Mnatakaje sasa?
 
AJALI za bodaboda zinachangia ugonjwa wa kifafa kwa waathirika wa ajali hizo kutokana na majeraha kwenye kichwa ambayo yanaathiri ubongo, imeelezwa.

Hayo yamebainishwa na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Mfumo wa Fahamu na Ubongo kwa watoto, Dk Edward Kija wakati akizungumza katika
Ahsante
 
Juzi Hapa Pia Kuna Daktari Alisema Hata Nyama Ya Nguruwe Kumeongeza Idadi Ya Watu Wenye Kifafa.

Hapa Itakuwa Ni Ugumu Wa Miasha Tu Ndio Umeongeza Idadi Ya Watu Wenye Ugonjwa Wa Kifafa.[emoji23]
 
Kuna mwamba kashusha meli nzima ya helmet,
NB vaa helmet muda wote upandapo pikipiki, kwani bodi ni mwili wako
 
Back
Top Bottom