Daktari alifanya nikampoteza mchumba wangu Mercy

Let's go..............

Tukiwa tupo geto kwa Mercy ile jpili tukawa tunapitia pitia researches na baadae tukaanza kujisomea somea kwa disc.
Baada ya kuchoka basi tukawa tunapiga piga stors.
Niliamua kumuliza Mercy juu ya ile likizo fupi kwamba ataenda homa au atabaki, Mercy alinambia kwamba kwao wamekwambia aende wamemmiss lakini pia nayeye amewamiss.
Nilikubaliana naye nikasema haina shida yeye ataenda lakini mimi nitabaki maana kilikizo ni kifupi sana. Bado Mercy hakuweza kunambia chochote kuhusu Dokta na mimi pia niliamua kujikaza nisimsemeshe chochote kuhusu Dokta.

Nilimuaga Mercy nikarudi zangu geto, nipo njiani narud kwangu nikapokea cm ya Mercy fek akaniuliza nipo wapi nikamdanganya nipo kwa Mercy maana anaujinga wa kutokea mageto kwangu sometimes tena bila hata taarifa, alikuwa anapenda kuja kwangu hasa boom lilipokuwa likiisha ili aje kugongea vichenji vya msosi.
Akanambia anashida ya kuonana na mimi na ni very urgent, nikampuuza nikajisemea Hana lolote anataka kuniweka 18 nimle.

Basi nikampa ahadi kwamba wakati nitakapokuwa natoka kwa Mercy basi nitapita kwake ila sitaingia magetoni tutakutana nje.
Nikaona kuna haja ya kumsikiliza pengine atakuwa na jambo la maana. Nilifika mageton kwangu nikavunga kama nusu saa then nikamchek nikamwambia nipo njiani nakuja atoke nje maana kwake hapakuwa mbali sana na kwangu.
Nilivofika karibu na kwake nikamkuta nje, alikuwa kipens cha filla, chini open shoes na juu alivaa t-shirt na kikot cha jeans.
Tukasalimiana tena pale nikamuliza vipi kuna issue gani, akanambia kwamba anajua mimi ni mwanaume nina uwezo wa kupokea kitu chochote regardless uzito wake na nikakimudu.
Nikamwambia aendelee asiwe na shaka, Mercy fek hakuwa na muda wa kupoteza akaanza kufunguka akasema ndugu yangu kidem chako kinakusalit na Dokta. Hapa moyo ulilipuka lakini nilivokumbuka maneno yake kwamba mimi ni mwanaume inabid nikaze bas nikaona nikipanic ataniona mrembo.
Nikakaza nikamuliza unauhakika na umejuaje?

Akanijibu wewe niamini Mercy anakusalit na Dokta, nilimsihi sana athibitishe. Akanambia ukweli kwamba alitafuta namna nyingne ya kujikonekt na Dokta maana alipatwa na tamaa baada yakuona Dokta ni mwepes kutoa pesa. Alinambia kwamba alienda mpka hospital aka act kwamba anasumbuliwa na jino, na walikuwa wanachat mpka Whatsapp na Dokta akawa kashamtumia Mercy fek picha kwahyo ikawa rahisi kumfaham yule Dokta.

Akanambia alipokutana na Dokta pale hospital akamuomba namba na akaanza kuwasiliana naye kwa namba nyengine kabisa.

Aligunduaje Mercy wangu anawasiliana na Dokta ilikuwa hivi.

Mercy fek alipoanza mawasiliano na Dokta kama nilivowambia huyu ni malaya hivo haikuchukua muda akajiingiza mwenyewe kwenye laini. Anasema kuna siku walitoka out na Dokta na walipokuepo huko viwanja Dokta alikuwa anaenda sana toilet na cm alikuwa anaacha pale mezani kwahiyo Mercy fek alikuwa anachungulia chungulia. Sasa katika kuchungulia akaona mesej imeingia na namba ilikuwa haijaseviwa na namba ya Mercy anaijua akanambia Ile mesej alikuwa kaituma Mercy mesej ilisomeka "baby where are you now mbona kimya"".


Seeee you............

===
Muendelezo soma Daktari alifanya nikampoteza mchumba wangu Mercy
 
Hii thread Tunatakiwa kuishia kuisoma hapa. Hebu kabadilishe jina la thread sasa.
 
Duuh!!
 
Mrs DR Mambo Jambo anafaidi sanaaa….
 
Wapotezee watu wana stress za maisha
 
HONGERENI WANANCHI.
Tuendeleee..............

Nilimuliza anauhakika ile namba ni ya Mercy wangu? Akajibu kwamba asilimia 100 ni ya Mercy na hakuwa na haja ya kunidanganya kunivuruga kichwa.
Basi nikamwambia inatosha na tukaagana nikasepa zangu home. To be honest siwez kuelezea maumivu ambayo niliyapata baada ya kugundua kile kitu japo sikuwa nimethibitisna mwenyewe kwa macho yangu lakini yaliniingia sana.

Nakumbuka siku hii nilitoka machoz kwasabb ya mapenzi (wakunitukana anitukane tu ila wanaoyajua mapenz wanaelewa namanisha nini).

Pamoja na maumivu haya sikutaka kabisa Mercy agundue kwamba kuna vitu nimejua kuhusu yeye na Dokta. Usiku huu ulikuwa ni mref sana na wamateso mengi mno. Kabla ya kulala Mercy alinichek kunitakia usiku mwema tukaagana.
Hapa nikaja kugundua kwamba watu wapole na wasio waongeaji sana hawa ni watu wa vitendo zaid maana Mercy kuna siku niliwambia kwamba alinambia maneno haya "nikichoka namimi nikaanza mambo yasiyofaa usije shangaa".

Japo Mercy hakuwa na haki ya kunikasirikia wala kunifikiria vibaya kwasabb sikuwahi kumsalit.

Nilivokumbuka haya maneno basi nikaanza kuona kila dalili ya ndoto zangu na Mercy zinaenda kufa. Nilijikaza nikalala na uzuri kesho yake kulikuwa na mtihani mmoja tu na ulikuwa ni jioni kwahiyo nikajipa imani nitasoma kesho asubuhi mpka mchana.

Kesho yake nikaamka nikapiga piga msuli kwa kuunga unga hivo hivo ili kujiandaa na mtihani. Mercy alinipigia tukaongea akanambia niende chai tayar nikamwambia sawa naenda. Nikajiandaa then baiki yangu mpka kwa Mercy.
Tulikunywa chai lakini akili yangu ilikuwa ishasinyaa kabisa haina muamko kabisa. Mercy akaniuliza kama nipo sawa nikamwambia nipo poa. Akanambia hapana kuna kitu hakipo sawa ebu niambie, hapa nilimgusia kidogo japo sio direct nikamuliza hivi Mercy unanipenda kweli? Mercy akajibu ndio tena sana, nikamuliza tena haunisalit? Akanijibu unadhani kila mmoja yupo kama wewe ulivo?

Basi stor ikaisha pale lakini nikaona kabisa kwa kiasi flan imemuingia japo amevunga lakini ujumbe ushafika.
Mercy akanambia baby usiwe na wasiwasi nakupenda na siwez kukusaliti kama hauamini basi sina cha kufanya kikafanya uamini Zaid. Nilikuwa nishajiapiza kutokujiweka karibu na cm ya Mercy tena kwahyo sikupata nguvu za kuchukua cm ya Mercy hata kama tukiwa tunasoma nilijitahidi kama ni notes au past papers niwe nazo katika cm yangu.
Basi ilifika mchana tukasema tujisogeze skul ili tukadiscuss na wengine katika kufinal touch kabla ya kuingia kwenye mtihani. Nikampakiza katika baik tukala road moka chuo.

Nilishangaa kwanzia muda ule nimeuliza Mercy yake maswali kuhusu kunipenda na kunisaliti Mercy aliongea sana upendo na kunijali (nahisi alifanya hivi ili kuniweka sana na nisimfikirie vibaya).
Mercy alibarika akaanza kusuprize na vizawad (boxer, perfume, viatu, majeans, n.k). Namimi nikawa napokea tu lakini moyoni nikawa najua kabisa zile pesa ni from Dokta mtu mbaya.

Tulifanya UE ikaisha nakumbuka ilikuwa j5, na kesho yake Mercy akawa anaratiba ya kwenda kwao. Nilimsindikiza mpaka stand nikahakikisha anapanda bus kabisa mpak gari iliposepa namimi ndo nikasepa.
Tukawa tunachat nikamtakia safar njema na nikamwambia awe makini. Mimi nilipanda boda nikarudi magetoni sikuwa na muda wa kupoteza town ukizingatia nilikuwa sipo sawa.

Nilifikiria kumtafuta Mercy feki nile naye mission anithibitishie kwamba kweli Mercy ananisalit na Dokta.
Lakini nikajiona kwamba nitakuwa mtumwa wa mapenzi na hisia nikaamua kupiga chini ule mpango. Likizo ilikuwa ni week moja na kama siku mbili hivi. Basi maisha yaliendelea na kwa Ile wiki nilikuwa na pika mara moja moja sana magetoni kwan sambamba na muda mwingi kuwa tunapika na kula kwa Mercy mimi pia nilikuwa na jiko na baadhi ya vyombo kwahyo nikanunua baadhi ya mahitaji nikawa najipikia kagetoni.

Nikiwa magetoni nasikiliza mziki nikapata wazo la kuanza kwenda chuoni kuchukua mazoez ya mpira wa miguu ili angalau niwe natoa yale mawazo kuhusu Mercy na Dokta.

See you.............

===
Muendelezo soma Daktari alifanya nikampoteza mchumba wangu Mercy
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…