Daktari alifanya nikampoteza mchumba wangu Mercy

Mueleze,wajuba tushajua
 
Tuendeleee.......

Mwanzoni mwa mwaka wa pili (2020 mwez wa11) tuliona mimi na Mercy tutafute vyumba mtaani tutoke hostel za chuo. Mimi nilifanyie field mkoa huohuo ambao kwahyo skuwa mbali na mazingira ambayo tulikuwa tunatakiwa kutafuta vyumba. Basi ilivobak kama weeks 2 tufungue nikaanza kufuta rooms nilihakgaika lakini nikabahatisha room katika mjengo flan mzur tu nikalipa kod kabisa ya miez sita tsh 240, 40/month. Mfukoni nilibakiwa na kama 580k maana nilikuwa na pesa ya field na home walinitumia kwasabb niliwaambia mwaka wa pili na wa3 hatutakiwi kukaa hostel tena. Nikatafuta kitanda na godoro used kwa wahitim, nikanunua jiko na mazaga mengine baadhi kwa kuanza life.

Nakumbuka ilibaki kama 160k nikapiga hesabu tukifungua tutapewa boom kwahyo hiyo 160k nikaamua kuifutia cha kufanya basi nikamchek Mercy kuhusu chumba kwanza akanambia pesa anayo mimi nimtafutie chumba Cha 50k isiwe chini au juu ya hapo. Mwanaume nikaanza kusavula kitaa kutafuta room nikapata room moja kali sana ilikuwa mtaa wa tatu kutoka mtaani kwangu.

Niliwaambia kimo na Mercy hatukuhusudu sana ngono ndo maana na vyumba tulitafuta kila mtu chake. Basi Mercy nakumbuka alinitumia 800k, yani pesa kwao haikuwa shida maana hata mkopo aliambiwa na babaake asiombe lakini aliniomba ushaur akasema anataka aombe kificho kwao wasijue ili awe na pesa za kutosha lakini mimi nilimkatalia nikamwambia watakuja kugundua halafu utapata shida akavunga.

Ile 800k aliweka katika acc yangu ya benk nikaenda kuichomoa nikalipa 300k ya miezi sita, nikanunua kabati la nguo na la jikoni, nikanunua sembe ya kilo tano, mchel, vyombo na mazaga zaga mengine ya kula plus sabufa ndogo maana alikuwa anapendelea sana mziki. Nilipofanya zile mambo ilibaki kama 95k nikamwambia akanambia nikate 30k nitumie halafu 65k atanikuta nayo. Nikafanya vile na mimi mfukoni nilikuwa na kama 120+35 nikawa na 155k.

Niliona kutoa pesa ya daladala kila siku buku kwenda chuoni ingenicost ikabid nitafute kibaiskel flan cha kukitumia. Mimi sikuwa brothermen bishoo kwamba ningeona soo kutumia baiskel. Nilipata baiskel flan ya kiaina yenye kiti cha kukalia nyuma. Basi week Ile ikakata ya pili ikakata j 3 tukafungua chuo, siku hiyo hiyo ndo ilikuwa siku ya Mercy kurudi chuo. Alifika saa3 usiku nikaenda kumpokea kama kawaida tulimisiana sana (asee nyie mapenzi matamu wakikutana wanaopendana).

Basi tukapita kuna sehemu walikuwa wanachoma nyama mfukoni nilikuwa na vijisent vimebak nikamnunulia nyama na bavaria akajishindilia tukawahi magetoni. Siku ile kwakweli kwasabb tulikuwa tumemisiana sana ilibidi alale kwangu kwahiyo tulikubaliana akalala kwangu nikajilia vyangu tulienjoy sana kwasabb tulikuwa na hisia kwa kila mmoja wetu tena zile true feelings.

Kesho yake tulikuwa na vipindi asubuhi saa tatu kwahiyo tuliamka tukajiandaa kwenda chuo nilimpandisha katika baiskel yangu japo mwanzo aligoma eti nitamuangusha lakini alikubali nikampandisha tukateleza kwenda skuli. Njiani wanafunzi wenzetu walikuwa wanatushangaa wengi wao hasa madem walitamani sana (wanawake wanapenda vitu vya kijinga jinga sana) namimi nikaamua kupitiliza mpka venue nikafinya break nje pembeni kidogo na venue Mercy akashuka nikapak baiki tukaingia venue.

Vipindi vilipoisha tukarudi kitaa na baiki yetu tukapitia room kwa Mercy akaiona alipenda kwahiyo tukaenda kwangu kusanya vya Mercy tukahamishia kwake.

Maisha ya nje ya chuo yakaaanza...........

==
Muendelezo soma Daktari alifanya nikampoteza mchumba wangu Mercy
 
Quetzal
 
Mbona kama kisirani mzee
 
..
 
[emoji28][emoji28][emoji28]
 
Tuendeleee.....

Kumbuka hiyo ilikuwa mwaka wa 2 mwanzoni.

Nakumbusha tena mimi na Mercy hatukupenda sana ngono kwahiyo tulikuwa tunakutana mara chache sana kwa semester tulikuwa tunaweza kukutana hata mara moja au mbili tu kwahiyo hatukuwa watu wa kugegedana sana.

Ratiba yangu kila siku ilikuwa ni kumpitia mpenz wangu na baik yangu kwenda chuo.

Niliwambia kwamba wanawake ni watu wa ajabu sana wanapenda vitu vya kijinga kijinga.
Ile baik iliniletea madem wengi mpka mwaka wa 3 yani walikuwa wanamuonea wivu Mercy kubebwa kwenye baik. Wengine walithubutu kunitongoza kabisa kisa ile lifestyle yangu na Mercy. Kulikuwa na pisi moja tulikuwa tunasoma nayo inaitwa Nurati ilinisumbua sana mpka Mercy akajua wakaznguana na kiukweli tulivokuwa tunapendana sikuweza kumsaliti mpenzi wangu.

Ile semester ya kwanza mwaka wa 2 tuliamua kushona sare ya vitenge mimi na Mercy hii ndo iliwamaliza kabisa wanafunzi wenzetu mpak wakawa wakituona wanasema et wanatupenda tusije kugombana n wengine wakawa wanatula kisogo walikuwa hawapendi sisi kupendana vile.

Mimi na Mercy tulikuwa tunapiga hesabu ya chakula na maji na mahitaj mengine kila mwez yani mfano tulikuwa tukipata hesabu inakuja labda laki 2.5 au mbili basi mimi nilikuwa natoa 2/3 yeye 1/3 mimi ndo nilipendekeza hivi ili kuweka heshima kama mwanaume. Tulikuwa tunapiga pamoja hasa kwake ili kupunguza bajet.

Tuliishi maisha mazuri sana na tuliahidiana kuona mimi na Mercy wangu lakini mwisho wa siku nikaamini ule msemo kwamba YA MUNGU NI MENGI na MIPANGO YAKE NI TOFAUTI NA MATAKWA YETU.

Let's meet badae kidogo.......

==
Muendelezo soma Daktari alifanya nikampoteza mchumba wangu Mercy
 
Changamka Mkuu, muda hautoshi uzi uwe mrefu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…