Tuendeleee.........
Baada ya kumfikisha Mercy hospital tulienda reception tukapata namba ya foleni, hapa maumivu yalikuepo lakini kwa mbali kwahiyo aliweza kuvumilia foleni. Katika foleni palikuwa na mtu mmoja tu ambaye alikuwa anaenda kutolea jino. Tulikaa almost kama dakika 45 yule mtu akawa katoka. Dokta alituruhusu tuingie ofisini kwake tukaingia akatuhoji kidogo kisha akatusubirisha kidogo alitokwa akaenda sehem skujua alienda kufanya nini lakini hakuchelewa. Niliamuliwa kutoka nje akabak Mercy huko ndani na dokta kwa ajili ya kutolewa lile jino.
Ilichukuwa kama nusu saa hivi akawa kamaliza Mercy alitoka akiwa kashikilia shavu lake. Nilipomuona nilipatwa na huruma sana nikamchukua taratibu tukaenlekea dirisha la dawa tukapewa dawa za kutuliza maumivu then tukapotea zetu. Siku ile iliisha kwa tabu sana maana alikuwa anapata maumivu mpenz wangu. Nilimchukulia maji ya barid akawa anakunywa taratibu mwenyewe akawa anasema aliweka maji ya barid mdomon anapata ahueni.
Siku ile nililala kwa Mercy, ilipofika saa 4 usiku cm ya Mercy ikaita nikampa akanambia nipokee maana Mercy alikuwa ananiruhusu kupokea cm zake na hata kujibu mesej kama alikuwa yupo bize. Nilipopokea nikasikia sauti ya kidume na yeye aliposikia saut yangu akauliza mgonjwa anaendeleaje nikamwambia anaendelea vizur lakini nikamuliza yeye ni nani akajibu ni Dokta alomtoa Mercy jino. Basi nikaona fresh tu ni kawaida Dokta kumjulia hali mgonjwa. Basi baada ya kumaliza maongezi tukatakiana usiku mwema basi ikaisha hivo.
Ikawa asubuhi tukaamka na alikuwa tyr ana nafuu kwahyo nikajiandaa nikaenda kwangu kuchukua baiki nikaja kumpitia Mercy kwenda chuo. Niliendesha mdogo mdogo ili asiumie mpenz wangu maana maumivu ya jino nasikia so poa. Tufika chuo tukaingia class tukahudhuria pindi likaosha tukatoka kupata tea ila Mercy aliagiza juice ya barid ya matunda tukamaliza tukasubr vipindi vingine.
Tulipokuwa tunasbr kipindi kingine cm ya Mercy ikaita alikuwa ni yule Dokta basi wakaongea madai yake ni kumjulia hali. Walipomaliza nikaanza kuhisi kunakitu Dokta anakitaka kutoka kwa Mercy. Nilimsanua Mercy ila akanambia niwe mpole hawez kunisaliti na anajielewa.
Hapo sikuwa na mishe mishe ya kuniingizia pesa tena maana zile cm nilikuja kuachana nazo niliona natumia muda na nguvu nyingi hafu hakuwa na maokoto ya kutisha. Sasa nikajiona kabisa kwamba naanza kuwa boya maana vipesa vya ice cream na yoghurt za kustukiza kwa Mercy zilianza kupunguza.
Vipindi viliisha tukarudi home, Mercy alipika tukala. Ile najiandaa nisepe Dokta kapiga tena sas nikamwambia Mercy naomba niipokee mimi akakubali nikapokea. Alivosikia saut yangu alifade up kidogo akauliza hali ya mgonjwa tu bas akakata cm. Nikamwambia tena Mercy awe makini asije kuvuruga ndoto zetu zikaja kufia njiani. Mercy alionesha kumpotezea na kumuona Hana maana yule Dokta.
Nikasepa, kesho yake nikampitia tuakenda chuo. Sasa nilikuwa nahitaj namba ya mshikaj flan Mercy alikuwa nayo kwahiyo nikachukua cm ya Mercy ili nichukue namba. Ile nimeishika tu ghafla ikaingia mesej "huyo dogo anaenipokelea cm zangu kakupa nini mbona unakua kama so mtoto wa mjini". Wazee hii text ilinikata sana nikapigwa na butwaa kwa muda kidogo Mercy alivonitazama aligundua kunakitu hakipo sawa akaiwahi ile cm lakini nikaikwepesha kidogo nikaifuta kwanza Ile mesej ndo nikampa cm.
See you there..........
===
Muendelezo soma
Daktari alifanya nikampoteza mchumba wangu Mercy