Tuendeleee.......
Mwanzoni mwa mwaka wa pili (2020 mwez wa11) tuliona mimi na Mercy tutafute vyumba mtaani tutoke hostel za chuo. Mimi nilifanyie field mkoa huohuo ambao kwahyo skuwa mbali na mazingira ambayo tulikuwa tunatakiwa kutafuta vyumba. Basi ilivobak kama weeks 2 tufungue nikaanza kufuta rooms nilihakgaika lakini nikabahatisha room katika mjengo flan mzur tu nikalipa kod kabisa ya miez sita tsh 240, 40/month. Mfukoni nilibakiwa na kama 580k maana nilikuwa na pesa ya field na home walinitumia kwasabb niliwaambia mwaka wa pili na wa3 hatutakiwi kukaa hostel tena. Nikatafuta kitanda na godoro used kwa wahitim, nikanunua jiko na mazaga mengine baadhi kwa kuanza life.
Nakumbuka ilibaki kama 160k nikapiga hesabu tukifungua tutapewa boom kwahyo hiyo 160k nikaamua kuifutia cha kufanya basi nikamchek Mercy kuhusu chumba kwanza akanambia pesa anayo mimi nimtafutie chumba Cha 50k isiwe chini au juu ya hapo. Mwanaume nikaanza kusavula kitaa kutafuta room nikapata room moja kali sana ilikuwa mtaa wa tatu kutoka mtaani kwangu.
Niliwaambia kimo na Mercy hatukuhusudu sana ngono ndo maana na vyumba tulitafuta kila mtu chake. Basi Mercy nakumbuka alinitumia 800k, yani pesa kwao haikuwa shida maana hata mkopo aliambiwa na babaake asiombe lakini aliniomba ushaur akasema anataka aombe kificho kwao wasijue ili awe na pesa za kutosha lakini mimi nilimkatalia nikamwambia watakuja kugundua halafu utapata shida akavunga.
Ile 800k aliweka katika acc yangu ya benk nikaenda kuichomoa nikalipa 300k ya miezi sita, nikanunua kabati la nguo na la jikoni, nikanunua sembe ya kilo tano, mchel, vyombo na mazaga zaga mengine ya kula plus sabufa ndogo maana alikuwa anapendelea sana mziki. Nilipofanya zile mambo ilibaki kama 95k nikamwambia akanambia nikate 30k nitumie halafu 65k atanikuta nayo. Nikafanya vile na mimi mfukoni nilikuwa na kama 120+35 nikawa na 155k.
Niliona kutoa pesa ya daladala kila siku buku kwenda chuoni ingenicost ikabid nitafute kibaiskel flan cha kukitumia. Mimi sikuwa brothermen bishoo kwamba ningeona soo kutumia baiskel. Nilipata baiskel flan ya kiaina yenye kiti cha kukalia nyuma. Basi week Ile ikakata ya pili ikakata j 3 tukafungua chuo, siku hiyo hiyo ndo ilikuwa siku ya Mercy kurudi chuo. Alifika saa3 usiku nikaenda kumpokea kama kawaida tulimisiana sana (asee nyie mapenzi matamu wakikutana wanaopendana).
Basi tukapita kuna sehemu walikuwa wanachoma nyama mfukoni nilikuwa na vijisent vimebak nikamnunulia nyama na bavaria akajishindilia tukawahi magetoni. Siku ile kwakweli kwasabb tulikuwa tumemisiana sana ilibidi alale kwangu kwahiyo tulikubaliana akalala kwangu nikajilia vyangu tulienjoy sana kwasabb tulikuwa na hisia kwa kila mmoja wetu tena zile true feelings.
Kesho yake tulikuwa na vipindi asubuhi saa tatu kwahiyo tuliamka tukajiandaa kwenda chuo nilimpandisha katika baiskel yangu japo mwanzo aligoma eti nitamuangusha lakini alikubali nikampandisha tukateleza kwenda skuli. Njiani wanafunzi wenzetu walikuwa wanatushangaa wengi wao hasa madem walitamani sana (wanawake wanapenda vitu vya kijinga jinga sana) namimi nikaamua kupitiliza mpka venue nikafinya break nje pembeni kidogo na venue Mercy akashuka nikapak baiki tukaingia venue.
Vipindi vilipoisha tukarudi kitaa na baiki yetu tukapitia room kwa Mercy akaiona alipenda kwahiyo tukaenda kwangu kusanya vya Mercy tukahamishia kwake.
Maisha ya nje ya chuo yakaaanza...........