Tuendeleee........
Maisha yalisonga nikiwa nipo kwa Mbwambo lakini nilikuwa narud magetoni kufata nguo na vitu vingine incase. NAMSHUKURU SANA Mbwambo alinisaidia sana.
Ngoja nimwambie kitu, Mbwambo kuna kipindi mwaka wa pili aliandamwa sana na sup ilibak kidogo adisco, Sasa aliniomba wakat wa kusapua ukifika basi niwe naye around ili niwe nampiga piga msasa. Baada ya field niliahirisha kwenda home kwaajili pia ya Mbwambo, tulikuwa tunakesha wote nampiga msasa na hatimaye akachomoa zote hii mwenyewe sikuamini yani jamaa alifuta sap zote alikuwa nazo tano ( sem2+sem3).
Nahisi hiki kitu ndo kilimfanya nayeye anisaidie na kuniona wa maana kwake. MERCY kuletwa na Dokta chuoni ikawa ni kawaida. Mimi huku hali ilizidi kuwa mbaya wanafunzi wenzangu walikua wote lakini Mercy hakujali hili.
Mbwambo alinishauri nitafute dem angalau wa kuniliwaza, nilimuona kama anaongea ujinga nikawa namjibu "kama Mercy wangu kabadirika kawa hivi basi hakuna dem mwingine nitakuja kumuamini".
Mbwambo akanambia "huyu dem naye kushauri umtafute sio kwa ajili ya kumpenda awe mpenz wako bali unasukuma naye time tu semester ikate tumalizie chuo". Haya maneno yalinifundisha kitu.
Baadae nikaja kumsikiliza Mbwambo lakini nikawa bado naathiriwa na ujinga wa Mercy, hakika nilikonda sana, nilikuwa natokwa na jasho sio polepole.
Nikaanza kufikiria ni nani nimvute awe bebe yangu kwa muda, nikawaza Mercy fek nikaona hapana ataniona kama mtu ninayetanga tanga baada ya kuachwa na Mercy kwasababu ni mtu aliyekuwa anajua kilichokuwa kikiendelea mwanzo mwsho.
Nilikuja kumpata dem mmoja anayeitwa "Merry" hii ni real name.
Huyu alikuwa ni mtu wa singida. Marry alikuwa ni first year, niliamua kwenda first year ili iwe ngum kwa dem wangu mpya kufaham story yangu na hata kama atakuja kuifaham basi iwe tyr nishamuweka under utawala wangu kwahyo haitakuwa na shida sana.
Nilikuwa na huyu Merry lakini nikawa najisemea kama Mercy atarudi Merry anaoigwa chini fasta tu maana Mercy alikuwa ananafasi ya kioekee katika moyo wangu.
Ndugu zangu huyu Merry ni binti mwembama, mrefu, mweupe na nywere zake zakiaina flan nadhani ni mtu wa singida lakini kamix na wairaq.
Merry alikuwa ananipa penzi as if alikuja kwangu kwa lengo la kunitibia yake maumivu kutoka kwa Mercy.
Merry alikuwa ananipa mapenz ya moto na ya dhat yani kama dozi hakunibania kama Mercy alivokuwa ananifanyia. Namimi nikaenda na tempo yake ikawa ni mwendobwa show tu yani nilikuwa nikimwambia nipo geto dakika chache tu namuona huyu hapa, nilianza kupata afadhar lakini ile hali ya kutokwa na jasho ilikuwa bado inaendelea na kukonda kukawa palepale kumbe nilikuwa nimepata shida mpka kwenye moyo sikuwa najua.
Ile semester ya mwisho ilikuwa ngum sana lakini nafikiri ingekuwa ngumu Zaid kama ningekuwa sina akina Mbwambo na Merry dem wangu wa first year.
Merry alikuwa ananijali sana na nikaanza kumpenda lakini bado Mercy still alikuwa anarotate katika mind yangu na muda wote nilikuwa namuwaza kwakweli.
Siku zilienda maisha yakasogea semester ikawa inakaribia mwishoni. Hapo Sasa mawasiliano na Mercy hayakuwepo kabisa na nikawa namuona tu venue, kitaa basi.
Kuna siku niliumia sana, ilikuwa ni weekend nimeenda town, nilikuwa alone nlienda crdb town kutoa pesa maana ATM ya kule chuoni ilipata shida kidogo kwahyo ikanibid niende town. Nilivokuwa navuka barabara ili niingie bank nikamuona Mercy na Dokta wanatoka kwenye duka la vipodoz lilikuwa mkabala na bank. Wao hawakuniona, ile kitu iliniuma sana nikatamani nimchek kwenye cm japo nimwambie nimemmiss lakini nikaona ni upuuzi nitampa point tatu za bure.
Kidume nikajikaza hilo jambo likapita nikazoea, kuna siku tena nikawaona wanatoka alipokuwa anakaa Mercy walikuwa katika gari wanaishirizia zao mtaani. Nikiona mengi nilivumilia lakini baadae nikaja kuoma nguvu ya kukaa kimya.
Ulikuwa imebak kama mwez hivi tuingie UE ya mwisho tumalize chuo, siku hiyo nikaona mesej ya Recho rafkiake Mercy. Alinichek akanambia Mercy ni kama hayupo sawa anaonekana kazinguana na Dokta wake.
Nikamwambia asante kwa taarifa lakin asiwe ananambia habari za Mercy kwasbb nilikuwa nikisikia jina lake moyo ulikuwa unalipuka kama nimepigwa na shot ya umeme wa grid ya taifa.
Sio kusikia jina tu hata nilipokiwa nikimuona nilikuwa nalipukwa sana na moyo. Hii hali ilikuwa inanisababisha natokwa sana na jasho na nakuwa na hasira sana zisizo na maana.
See you......