Daktari alifanya nikampoteza mchumba wangu Mercy

Daktari alifanya nikampoteza mchumba wangu Mercy

nilimtreat kama malaya tuu
Hata Kuna mmoja nilimtokea nikamla siku iyo iyo akaja mtu wake wa muda mrefu mno tokea mkoani kwao alimfundisha olevo na walizaa mtt Sasa demu hakuniwekega wazi. Siku iyo iyo usiku saa Saba akamfuata jamaa yake. Nikaamua kumuona Kama Malaya maisha Ni mpira kwa vile alikuwa ananipa k nakula mpaka nashiba na muda wowote nikiihitaji naye alinipenda ,yaani alikuwa anautamani muhongo anadai yaani Kama haupo kwenye mpira sijui utakuwaje. Tumekuja kuachana Ile kirafiki baada ya kumaliza chuo ndio namfungukia naye anafunguka,nikamwambia ungesema akaniambia kuwa nilikuulizaga Kama waweza oa mwenye mtt ukakataa kumbe alikuwa ananicheki ,alinipenda namie nilimpenda.yaani Ni demu pekee niliyemla ambaye aliniambia ana shida ya 16500 nikampatia ,yaani hapo ilikuwa no dozi baada ya kula usiku Ni dozi ndio tunaenda prepo na uzuri hostel kwao walikuwa wawili tu.
 
Ladies and gentlemen,

Ukiona umeshindwa ku-deal na mpenzi wako achana naye.

Usijishughulishe na wanaomzuzua.

Utajiaibisha tu.
Of course, na point nyingine niliyoiona kwa bwana mdogo DeMostAdmired na mpenzi wake ni kwamba walikuwa hawana gap kati yao, yaan wako sawa, wote walikuwa wanasoma chuo kimoja, same year, same course, maisha sawa japokuwa jamaa ashatuambia demu alikuwa wakishua, ni mbaya sana kulingana kila kitu na demu, hatakama anakupenda kuna muda utafika mwanamke atakuwa anahitaji mwanaume anayemzidi vitu.

Ili kuwe na mvuto baina ya mwanaume na mwanaume lazima kuwepo na gap, sio lazima liwe la kiuchumi, linaweza kuwa la kidarasa, umri, knowledge, elimu etc
 
Tuendeleee........

Nipo zangu geto siku hiyo naona mesej ya Mercy "nimepata hiyo sup kwasababu yako". Kiukweli sikuwa na ham ya kujibu hata ile text ya Mercy huwezi amini nilikuwa nina hasira naye sana japo kupata kwake sup iliniuma.

Baadae nikaona hapana ngoja nimjibu, niliandika short text "pole, utaichomoa usiwaze". Mercy hakujibu tena.
Kulikuwa na baadhi ya nguo zangu kwa Mercy nikaona nazipataje maana nikama nilikuwa tyr nishaachwa.
Nikaona nizipotezee tu maana hazikuwa nyingi na za maana kivile. Niliona Mercy ile sup kwa kiasi flan ingempunguzia kasi na atajirud kwangu kumbe nilikuwa najidanganya.

Kuna siku nilikuwa katika baiki nasepa chuo njian ilinipita gari na nikahisi ni gari ya Dokta, nilikuwa nimekaribia kufika chuo. Niliona ile gar imesimama akatoka Mercy akasepa na gar ikageuzwa ikaondoka.
Siku hii nilijiona kama kuishi kwangu duniani ni adhabu kubwa, niliona ulimwengu umenielemea, nilichanganyikiwa sana na machozi yalinilenga.
Nilipofika venue nikamkuta Mercy yupo na wenzake wanapiga stors, niliwasalimia then nikasonga zangu kutafuta place nikae.

Kuna huyo dem tulikuwa tunasoma wote anaitwa Sozi, Sozi alikuwa ni mmoja ya walokuwa wananikubali sana na alifanya kila njia niwe naye katika mahusiano lakini nilikuwa nishazama kwa Mercy. Pale nilipoenda kukaa nilimkuta Sozi na madem wengine kama watatu kulikuwa na nafasi kama ya watu wawili ilikuwa imebak, Sozi aliponiona akaniita kwa bashasha akanambia niende kukaa naye eti kaniwekea seat.

Namimi sikukataa nikaenda, nilivofika wakalopoka "hey handsome njoo ukae hapa jamani tumekuwekea seat" hili bench kilikuwa hatua mbili mbele ya bench alokuwa amekaa Mercy. Nilipofika Sozi akanambia "handsome karibu, you are so handsome hivi unalijua hilo lakini?" Niliona kama ananizingua tu nikamzuga zuga tutaendelea kula stor.
Yale maneno ya Sozi yalifika alipokuwa amekaa Mercy na wenzake kwani mmoja wa marafiki wa Mercy yule Recho nilimsikia akisema "handsome wako kachukuliwa huko" nikawa makini kusikia Mercy angejibu nini lakini aliguna tu. (Mercy siyo talkative).

Sozi alianza kunilipua akasema saiv siwaelew wewe na Mercy mbona kama hampo sawa, nikamjibu achana na hayo mambo tupiga stor zingine. Sozi akacheka akanambia "nilokupa nafas ukachezea saiz tungekuwa tunaenjoy zetu, of course Sozi alikuwa ananipenda lakini sikutaka kuwa naye kwasabb ni mtu wa maneno mengi na mimi sipend dem wa hivo yan tusingedum.

Kile kitendo cha akina Sozi kuniweka seat na kunikaribisha kwa bashasha kilimfanya nijiamini kwa kiasi flan nikaona kumbe ninathamani kwa watu, nikaona Mercy kuniacha nisijione sina thamani nikamalizia kuwaza na kale kamsemo "ukinidelet wengine wananidowload"

Lecturer aliingia tukapiga pind then tukasepa, siku ile hatukuwa na vipindi vingi. Tulivotoka Mercy aliikiwa na gar akasepa. Hii hali nilijidanganya kwamba nishaizoea kumbe ilikuwa inaniumiza taratibu.

Washkaji walikuwa wananicheka sana kwasbb Mercy alikuwa anafanya kama kunikomoa na sikuwahi kudhani kama Mercy angefikia kufanya mambo ya kikatili vile kwangu kwasabb alikuwa ni dem mpole na mstaarabu sana.

Hali ile ya kudharirishwa na Mercy ilikuwa inaniharibu akili taratibu. Nilikuwa najiona kama nabadirika taratibu taratibu lakini nikawa siyatilii maanani yale mabadiriko.
Usiku nilikuwa natokwa sana na jasho, nikaanza kuwa mtu muongeaji sana, nikaanza kukonda Zaid na Zaid, nikaanza kuacha nywere zinakua mpka zinapitiliza yani kifupi nikaanza kuona kama naenda kuwa chizi lakini mimi nikawa najiona kawaida tu. Nilianza kuwachukia wanawake pia, nikawa nahasira nao tofauti na mwanzo.

Rafiki yangu Mbwambo alinigundua kwamba naenda kuharibikiwa, kuna siku alinifata akanambia anahitaji kuongea namimi nakumbuka ilikuwa tupo chuo kwahiyo tukapanga baada ya vipindi tutaongea wakat tunarud kitaa maana Mbwambo pia alihamia kitaa.

Njiani Mbwambo alinambia kwamba anaona sipo sawa na nahitaji nipate mtu wa karibu kwa kampani na uangalizi, nilimkatalia lakini akanisihi kwamba atahakikisha anakua namimi benet hatakubali kuiona nazd kuteseka. (Kama wenye shida za afya ya akili wengekuwa wanapata watu kama Mbwambo basi suicide cases zingepungua sana).

Mbwambo alinambia nichakue nihamie kwake au yeye ahamie kwangu, nikamwambia Haina haja lakini alisisitiza tena kwamba "kaka haupo sawa niamini mimi unahitaj kampani". Basi nikakubali nikahamia kwa Mbwambo.

See you......
 
Back
Top Bottom