Daktari alifanya nikampoteza mchumba wangu Mercy

Daktari alifanya nikampoteza mchumba wangu Mercy

Very good story broh naimani ni kweli kabisaa
Hao walokuponda wasamehe bure kamwe usitarajie watu wote wawe upande wako ktk maisha
Honestly nimejifunza kitu hapa na uzee wangu wote huu
Pole kwa uliyopitia naimani utakua umepona
Nipo fit
 
Kwani we unajua alikuwa anasoma course gani na Faculty gani?
Au hujui kama Chemistry pia Chuoni watu wanasoma?

Sijaona Logic yako kusema Ni chai kwa sababu tu DeMostAdmired kataja kuwa alikuwa na mtihani wa chemistry..

Sijui Elimu yako ila naanza kupata Mashaka nayo kwa sbabu your Logical Point of View iko Very Non sequitor
Someni mburudike inasaidia kupoteza muda. Hii ni Chai. Hakuna Chuo ambacho atasoma serious anaenda mpitia msichana mzuri na baiskeli. Labda chuo cha Veta au Ualimu huko Nanjilinji. This is fiction totally.
 
Dem wako hakua na msimamo mkuu.

Sifa zoote ulizompa huko nyuma zimekuja kuharibika hapa. Yaani mpaka anapanga mipango ya kukucheat na uongo kibao, hapo huyo sio wako tena.

Na hilo jambo ulikua na uwezo wa kulizuia ila mapenzi yako ya kifilipino yakafanya ufe kijerumani na tai shingoni.
Unaacha kudeal na dem unaenda kuzozana na dokta, unaona text ya mgegedo unakausha eti hadi uambiwe. Sometimes wanawake hawapendi wanaume waoga waoga, ndo nyie kosa sio lako unaomba msamaha ili pisi isikasirike...

Pole sana dogo, i feel your pain.
Hii ni story ya kutunga ichukulieni hivyo msonge mbele.
 
Ulishawahi kuwa kwenye uhusiano na mtu ambaye mnapendana kwa dhati? Mmeweka mipango ya pamoja na mnapambana kuitimiza. Labda mmeshatambulishana hadi kwa jamii inayowazunguka - ndugu, jamaa na marafiki. Ukiangalia mipango na maisha yako ya baadaye yote imejawa na huyo mtu. Unamuamini kupita kiasi. Pengine hata unawaza bila yeye maisha yako hayana thamani yoyote, hayawezekani.

Halafu ghafla inatokea mwenzako anageuka ghafla, anataka kuondoka. Pengine mmekoseana, mmetofautiana kidogo au sana, na au hata hakuna sababu yoyote ila mwenzio anakuambia safari yake kwenye maisha yako imefikia tamati. Pengine anakueleza upungufu na udhaifu wako, au anaweza asikuelezee. Pengine anakuambia wewe ni mtu mwema sana kuliko yeye, hivyo anaona hastahili kuwa na wewe au akakuambia wewe siyo type yake.

Vyovyote iwavyo; mtu ambaye yupo mbele yako amekuletea ukweli mpya mbele yako ambao unapaswa kuupokea hata kama hautaki au haupendi - anapaswa kuondoka. Wewe haupo tayari kuupokea ukweli huu; Wanasaikolojia wanakuambia ili upate uponyaji wa kweli ni lazima upitie hatua tano zifuatazo:

1. Denial (Kuukataa)
Hii ni hatua ya kwanza kabisa ambapo utaukataa ukweli/uhalisia huo mpya. Unakuwa unawaza hawezi kuniacha tumetoka mbali sana, tumefanya mambo mengi sana pamoja, huwa tunatofautiana tu tunayamaliza, ananipenda sana, ninampenda sana na yeye anajua, hawezi kuniacha na tuna watoto, hawezi kuniacha na pesa zote hizi nilizonazo au urembo huu, hawezi kuniacha kwa anavyonitegemea, n.k.

Mkuu, hakuna cha mmefanya mangapi au mlipendana kiasi gani; hakuna cha mali wala urembo, hakuna cha watoto wala eti wazazi, hakuna cha alishajitambulisha kwenu na au umetoa/kutolewa mahari. Kama ameamua kwenda, ujue tu ndio imetoka hiyo.

Kitu kizuri cha kufanya kwenye hatua hii ni kuanza kujiandaa kuupokea ukweli wowote uliopo mbele yako.

2. Anger (Hasira)
Hii ni hatua inayofuata baada ya ile ya kwanza. Katika hatua hii unakuwa na hasira sana. Unamchukia aliyekuacha na au hata watu au vitu unavyohisi vimesabisha. Hapa ndio unakuwa kwenye hali ya kumchukia mtu ila bado unampenda. Unakuwa unajifariji na maneno kama "anaringa sana ila ndio hivyo ninampenda sina jinsi", "ananifanyia hivi kwa kuwa anajua ninampenda", "pamoja na yote tuliyoyafanya pamoja leo ndio ananifanyia hivi kweli!!?"; mara unausingizia moyo wakati wewe mwenyewe hautaki kusikiliza ubongo unaokuambia ukweli, hahaha...

Hapa unaweza hata kujichukia wewe mwenyewe kwa kumpenda mtu kupitiliza. Unamchukia mhusika kuwa hajali hisia zako, hajali jinsi unavyojitoa kwake, jinsi ulivyomthamini. Unamchukia kuwa amekuchezea tu na sasa umempa mzigo anakukimbia. Unawachukia wanaume au wanawake wote. Unakuwa unapatwa na uchungu mkali na usioelezeka, mara nyingine hata unashinda unalia, unakonda wakati mwenzio anazidi kunenepa, hahaha...

Namna nzuri ya kushughulika na hatua hii ni kulia kwelikweli kama unahisi kulia, kuwashirikisha watu wako wa karibu - ndugu, jamaa na marafiki - ambao unahisi watakuwa na wewe, unaowaamini. Achilia huo uchungu, ndio unapona hivyo.

3. Bargaining/compromising (Kutafuta maelewano)
Baada ya hasira kuwa nyingi, na kutafuta faraja huku na kule utashauriwa na moyo au pengine na watu wako wa karibu kuwa mtayamaliza tu, mkae chini muongee. Basi na wewe unajidanganya eti mtayamaliza kweli. Unamtafuta mwenzio unaanza kumbembeleza mrudiane, asiondoke. Unamshawishi kuwa bila yeye wewe siyo kitu, maisha yako bila yake yatakuwa na ni sawa na gari bila konda, hahaha... Unampenda sana.

Unaweza hata kumkumbusha mambo aliyokuahidi, moments nzuri mlizozipitia, na kwamba wewe ni mwanadamu tu. Hapa ndio watu huomba msamaha hata kama hawakukosa na kutoa ahadi hata wasizoweza kuzitimiza ili tu watu hao wabaki katika maisha yao. Hapa ndio watu wanakuwa tayari hata kutoa mahari wakati waligoma kwa miaka kadhaa, hapa watu ndio huwa tayari hata kutoa mbususu walizozibania kwa miongo kadhaa, hapa watu huwa tayari kufanya chochote ili tu wasiuruhusu uhalisia au ukweli mpya kuchukua nafasi. Ndugu yangu, mtoto wa mtu kama ameamua kwenda hata uahidi kumpa dunia yote hawezi kukuelewa. Kwahiyo hata ufanyaje, mwenzio ameamua kwenda muache tu aende. Ukiachwa achika. Hahaha...

Ndugu, kitu kizuri cha kufanya hapa ni kusikiliza tu ushauri na uzoefu wa watu waliowahi kupitia hali kama hii - ambao watakushauri umuache tu aende.

4. Depression (Msongo wa mawazo)
Baada ya kupambana kadiri uwezavyo, kujishusha mpaka chini kabisa na kufanya kila kitu ndani ya uwezo wako na unaona mambo yamegoma kabisa, ndio unapata msongo wa mawazo. Unajutia hisia na muda uliouwekeza ambao mwisho wa siku umepotea. Ukiwaza namna ulivyojitoa, unapata stress ya kufa mtu. Utawaambia nini watu ambao pengine uliwaoshea? Hahaha... Hapa ndio watu hukasirikia kila mtu.

Hata hivyo habari njema ni kuwa unakaribia kuukubali ukweli. Hivyo njia nzuri ni kuanza tu kujiandaa kuipokea hatua ya tano na ya mwisho.

5. Acceptance (Kuukubali)
Baada ya yote sasa inafikia kipindi mtu unaamua tu kuukubali ukweli - unamuacha aende au unaupokea ukweli. Hapa sasa ndio mtu anaanza kurudia hali yake ya kawaida. Hapa hata walioapa hawatakuja kupenda ndio unaona sasa wanapenda tena. Waliosema wanaume wote ni mbwa ndio hapa wanakuwa tayari kubwekewa na mbwa mwingine tena, hahaha...

Note:
  • Tunapokushauri kuwa utapona baada ya muda na kila kitu kitakuwa sawa, huwa tunamaanisha kukupa muda ili uzipitie hatua hizi vizuri na kwa ukamilifu. Hii ndio maana halisi ya time heals.
  • Tujue kabisa kuwa break up zinaumiza. Hakuna kabisa (au kama ipo ni mara chache sana) kuachana kwa amani. Ukiachwa ni lazima uumie. Hata ndugu zangu Sukuma Gang muda utatuponya na tutaukubali ukweli kuwa hii nchi imerudi kwa wenye nao - wapigaji - baadaya kupitia hatua hizi zote. Hahaha...
Ninawatakia kipindi chema cha Pasaka.. Mlioachwa achikeni. Hahahaa...
 
Yaani alitakiwa awashe moto mpaka Mercy mwenyewe aombe pooo....eti katulia Hadi kamegewa kizembe jamani....Ilitakiwa usiku ule ule alivyoona meseji za lodge amuashe na kibao Cha ujinga pale alipolala mbona kesho yake hata kanisani asingeenda
Nliwaambia hii ni ya kutunga mkabisha. Hakuna uhalisia wa ayasemayo huyu dogo.
 
I bet , huyu jamaa ni msukuma
Kuna wakati mapenzi yanatufanya kama watoto..

Kubali ama usikubali Wote tumepita Situation yake..Inaweza ikawa different Story ila lazma kwemye kichwa ukiiwaza unasema dah na mimi niliwahi kuwa zuzu..

Najua tunayo ila tunazificha na kudhihaki wwngine..

Kila Jambo kwemye maisha yetu tunayopitia ndo hutufanya kuwa imara na mashujaa na hutupa funzo ambalo ni aghalabu sana kurudia makosa hayo..
Na ndo maana wanasema "Past is our teacher.."

Ukimuuliza Kila mtu lazma ana story ambayo hajawahi kumwambia mtu yoyote kuhusu Mapenz hivyo kumcheka kijana wangu DeMostAdmired kwa sababu yeye kaamua kuidhihirisha kwa watu sio sawa
 
Bonge la nyuzi
Watu hawataki kuachika ndo shida iliyopo mpk wanapata vihoro
 
Tuendeleee......

Nilipoa kama maji ya mtungini, hii taarifa ilinivunja moyo kwa mara nyingne tena safari hii nilivunjika kwa kishindo kikubwa. Mercy alinambia nimuache kwanza apumzike maana alikuwa hayupo sawa pia nayeye. Basi nikamuacha nikalala zangu pembeni, baadae nikamuliza kwahyo itakuwaje kuhusu mimba akanambia hajui la kufanya kwa muda ule.

Siku zikasogea, lakini nikajitahidi nisiwe mbali na Mercy ili asije kufeli maana tulikuwa tunakaribia UE ya mwisho.
Ili kumfanya awe na furaha nilimuahidi nitakuwa naye bega kwa bega hata kumuoa nitamuoa hvohvo na mimba yake lakini moyoni nilikuwa najisemea siwez kuoa mtu mwenye mtoto huku baba wa mtoto bado yupo hai huko ni kucheza na moto.

HAPA NILIONA KABISA DOKTA KANIHARIBIA MIPANGO YANGU NA MERCY KWASABABU YULE TAYARI AMESHAOA NA KWA HAKIKA KUMPA MERCY MIMBA ILIKUWA NI MAKUSUDI ILI TU ANIONESHE YEYE NI ZAIDI YANGU. HAYA NDO YALIKUWA MAWAZO YANGU.

Tulifanya UE tukamaliza vizur huku Mercy akiwa anaendelea vzr na ujauzito wake. Tulivomaliza UE tukakaa sasa ili nijue what's next, nilimuliza Mercy anafikiria nini akasema anaona bora aitoe ile mimba ili apate kuishi namimi kwa uhuru.
Hapo tushamaliza chuo tyr tuna kama siku mbili.

Tulikuwa tunamalizia ngwe ya pili ya research tukusanye then tupotee makwetu.

Lile wazo la Mercy kutoa ujauzito sikuliunga mkono nikakataa kabisa nikamwambia ni hatar anaweza hata akapoteza maisha.
Mercy alikataa katu katu akasema ni lazima aitoe kwani alihitaji awe free tuanze maisha.
Mimi nilishindwa kumzuia, lakini sikushiriki katika kuitoa ile mimba. Mercy alifanya yeye kama yeye sikutaka kujiingiza katika hii dhambi.

Mercy alienda hospital ilikuwa ni pale pale mtaani hakwenda town, alienda kwa nurse mmoja akamshaur kwasabb ujauzito bado ni mchanga sana hautasumbua.
Sikujua alimpa madawa gani Mercy alikunywa, siku ile hatukulala maana alikuja kunywea mageton kwake, hali ilibadirika akaanza kuumwa na tumbo mwisho wa siku akanichek na kwa jinsi alivokuwa anaongea alionekana kuzidiwa sana.
Nilienda nikamkuta anagaa gaa chini, nikashindwa nianzie wapi. Nikamuliza shida nini ndo akanambia amemeza madawa ya abortion. Nikamuliza kapewa na nani, nilimuliza ili nijue naanzia wap kumsaidia, alinielekeza yuel nurse nikamfaham. Na hapakuwa mbali na pale nikaona kumpigia cm nitachelewa nikaona niped baiki mpka pale kwenye kidispensari.

Nilimkuta nurse nikamueleza na nikamsihi twende fasta, alichukua madawa dawa flan na vifaa kadhaa tukaongozana mpka kwa Mercy. Tulipofika tulimkuta bado anaugulia maumivu, nilimpa nurse nafas amhudumie Mercy.

Baada ya kama nusu saa akatoka akanambia atakuwa powa ni shida ya kawaida tu, akasema anawahi kwende kituo chake cha kazi. Alinihakikishia kuwa Mercy atakaa sawa kwahyo nikapata faraja maana niliwaza kama Mercy atapata shida zaid mimi nitakua answerable.

Ilipita kama lisaa Mercy akawa kapata nafuu, nikamuliza anahitaj nini akasema yupo sawa. Nilimpa tu maji nikamfatia na chips akapiga then tukalal.
Kesho yake Mercy alinambia kuwa anahisi mimba imekataa kutoka. Nikamuliza kwanini akasema yeye anajua kwaiyo anahisi hivo. Kumbe kweli ile mimba iligoma kutoka na baada ya jaribio kufeli nilimkanya Mercy aache kabisa kuitoa ile mimba.

Tulimalizia research zetu tukakusanya sasa tukawa free kuondoka makwetu. Siku mbili kabla ya kuondoka Mercy alinambia twende kwao akanitambulishe, nilifikiria nikaona Mercy hayupo sawa yupo stressed. Maana ni ngum dem aende kukutambulisha kabla wewe kidume hujaenda kumtambulisha kwao.

Kifupi Mercy alikuwa anahitaj kabisa kuishi na mimi na alikuwa tyr twende kwao akanitambulishe.
Nilimuliza kuhusu Dokta, Mercy alinijibu hatak hata kumsikia lakini still Dokta alikuwa anamaumbua bado Mercy na alikuwa anahitaj kujua ujauzito wake unaendeleaj na alikuwa anamsihi pia asithubutu kuuutoa.


See you.......
 
Wanaume mkichit mmeteleza
Ila mwanamke akichit kadhamiria na hasamehewi kkaaahhh
Haha...

Utofauti wa kibaiyolojia kati ya mwanaume na mwanamke unaathiri utendaji kazi wa akili.

Ndiyo maana inapelekea pia utofauti hata katika suala la ku-cheat.

Huu ni ukweli kwa mujibu wa saikolojia, wala sijaweka hivyo ili kutetea jinsia yangu.
 
Hapa tulienda na Mercy kuzurula ilikuwa ni weekend alinipigia hii picha
Hizi picha dogo una zidownload Tiktok. Acha uongo. Wewe hadithia tu kama stories nyingine usilazimishe ionekane kweli.

picha hii nimeitoa ulikoitoa hiyo yako.

Screenshot_2024-02-25-22-41-59-340_com.google.android.googlequicksearchbox~2.jpg
 
Back
Top Bottom