Tuendeleee......
Nilipoa kama maji ya mtungini, hii taarifa ilinivunja moyo kwa mara nyingne tena safari hii nilivunjika kwa kishindo kikubwa. Mercy alinambia nimuache kwanza apumzike maana alikuwa hayupo sawa pia nayeye. Basi nikamuacha nikalala zangu pembeni, baadae nikamuliza kwahyo itakuwaje kuhusu mimba akanambia hajui la kufanya kwa muda ule.
Siku zikasogea, lakini nikajitahidi nisiwe mbali na Mercy ili asije kufeli maana tulikuwa tunakaribia UE ya mwisho.
Ili kumfanya awe na furaha nilimuahidi nitakuwa naye bega kwa bega hata kumuoa nitamuoa hvohvo na mimba yake lakini moyoni nilikuwa najisemea siwez kuoa mtu mwenye mtoto huku baba wa mtoto bado yupo hai huko ni kucheza na moto.
HAPA NILIONA KABISA DOKTA KANIHARIBIA MIPANGO YANGU NA MERCY KWASABABU YULE TAYARI AMESHAOA NA KWA HAKIKA KUMPA MERCY MIMBA ILIKUWA NI MAKUSUDI ILI TU ANIONESHE YEYE NI ZAIDI YANGU. HAYA NDO YALIKUWA MAWAZO YANGU.
Tulifanya UE tukamaliza vizur huku Mercy akiwa anaendelea vzr na ujauzito wake. Tulivomaliza UE tukakaa sasa ili nijue what's next, nilimuliza Mercy anafikiria nini akasema anaona bora aitoe ile mimba ili apate kuishi namimi kwa uhuru.
Hapo tushamaliza chuo tyr tuna kama siku mbili.
Tulikuwa tunamalizia ngwe ya pili ya research tukusanye then tupotee makwetu.
Lile wazo la Mercy kutoa ujauzito sikuliunga mkono nikakataa kabisa nikamwambia ni hatar anaweza hata akapoteza maisha.
Mercy alikataa katu katu akasema ni lazima aitoe kwani alihitaji awe free tuanze maisha.
Mimi nilishindwa kumzuia, lakini sikushiriki katika kuitoa ile mimba. Mercy alifanya yeye kama yeye sikutaka kujiingiza katika hii dhambi.
Mercy alienda hospital ilikuwa ni pale pale mtaani hakwenda town, alienda kwa nurse mmoja akamshaur kwasabb ujauzito bado ni mchanga sana hautasumbua.
Sikujua alimpa madawa gani Mercy alikunywa, siku ile hatukulala maana alikuja kunywea mageton kwake, hali ilibadirika akaanza kuumwa na tumbo mwisho wa siku akanichek na kwa jinsi alivokuwa anaongea alionekana kuzidiwa sana.
Nilienda nikamkuta anagaa gaa chini, nikashindwa nianzie wapi. Nikamuliza shida nini ndo akanambia amemeza madawa ya abortion. Nikamuliza kapewa na nani, nilimuliza ili nijue naanzia wap kumsaidia, alinielekeza yuel nurse nikamfaham. Na hapakuwa mbali na pale nikaona kumpigia cm nitachelewa nikaona niped baiki mpka pale kwenye kidispensari.
Nilimkuta nurse nikamueleza na nikamsihi twende fasta, alichukua madawa dawa flan na vifaa kadhaa tukaongozana mpka kwa Mercy. Tulipofika tulimkuta bado anaugulia maumivu, nilimpa nurse nafas amhudumie Mercy.
Baada ya kama nusu saa akatoka akanambia atakuwa powa ni shida ya kawaida tu, akasema anawahi kwende kituo chake cha kazi. Alinihakikishia kuwa Mercy atakaa sawa kwahyo nikapata faraja maana niliwaza kama Mercy atapata shida zaid mimi nitakua answerable.
Ilipita kama lisaa Mercy akawa kapata nafuu, nikamuliza anahitaj nini akasema yupo sawa. Nilimpa tu maji nikamfatia na chips akapiga then tukalal.
Kesho yake Mercy alinambia kuwa anahisi mimba imekataa kutoka. Nikamuliza kwanini akasema yeye anajua kwaiyo anahisi hivo. Kumbe kweli ile mimba iligoma kutoka na baada ya jaribio kufeli nilimkanya Mercy aache kabisa kuitoa ile mimba.
Tulimalizia research zetu tukakusanya sasa tukawa free kuondoka makwetu. Siku mbili kabla ya kuondoka Mercy alinambia twende kwao akanitambulishe, nilifikiria nikaona Mercy hayupo sawa yupo stressed. Maana ni ngum dem aende kukutambulisha kabla wewe kidume hujaenda kumtambulisha kwao.
Kifupi Mercy alikuwa anahitaj kabisa kuishi na mimi na alikuwa tyr twende kwao akanitambulishe.
Nilimuliza kuhusu Dokta, Mercy alinijibu hatak hata kumsikia lakini still Dokta alikuwa anamaumbua bado Mercy na alikuwa anahitaj kujua ujauzito wake unaendeleaj na alikuwa anamsihi pia asithubutu kuuutoa.
See you.......