Daktari alifanya nikampoteza mchumba wangu Mercy

Tuendeleee.......

Hapa nikaona kabisa Mercy hakuwa na mapenz na Dokta ila shida ni tamaa za pesa na Dokta alikuwa hana mpango wa kumuoa Mercy ila alihitaji kunikomoa tu. Nilihisi vile baadae baada ya siku moja Dokta kunitumia ujumbe "dogo wanaume tushafanya yetu ole wake hiyo mimba mkaitoe".

Hii text alinitumia siku moja kabla ya Mercy kufanya jaribio la kuitoa ile mimba. Hii text sikumuonesha Mercy niliona kama ntamchanganya tu na Haina maana.

DOKTA ALIMTIA MERCY MIMBA KWA MAKUSUDI NA ALIMLAGHAI KWA PESA ZAKE, HII KITU MERCY MWENYEWE NDO ALINAMBIA.

Niliwaza kama Mercy alikuwa hampendi Dokta ni kwanini alikubali kufanya nae tena kavu siku zake za hatari. Sikupata majibu sahihi nikaamua kuipotezea tu japo niliishia kuamini kuwa pesa ndo ilimshawishi Mercy mpka kubeba mimba.

Swala la Mercy kwenda namimi kwao akanitambulishe sikulikubali niliona Mercy hajafikiria kwa kutuliza akili na pia binafsi sikuwa tayar kuoa mwanamke mwenye mtoto.

SIKU YA KUAGANA NA MERCY ILIKUWA NI MAJONZI SANA.

Nilimsindikiza stand akapanda bus kuelekea kwao. Mimi naye nilibaki kwanza pale town kuna mambo yangu nilikuwa nayafatilia.

Nilikaa kama mwezi hivi ukizingatia hata kodi yangu bado ilikuwa inasoma. Kipindi kile nipo bado pale town niliamua nimtafute Merry, Merry alikuwa tayar kashaondoka kwenda Field alienda mkoa wa dodoma. Nilipomaliza mishe zangu nikapak vitu vyangu nikaondoka nyumbani namimi.

Mawasiliano na Mercy yaliendelea ila upande wangu nilianza kuona Haina tena haja ya kumtafuta mara kwa mara ila yeye alikuwa ananitafuta sana ananisihi nimuoe hata kama bado sijajipanga yeye kwao pesa so shida sana. Aliahidi ataomba pesa ya mtaji tuanze kuzichanga mdogo mdogo ila mimi nikaona kabisa Mercy nikimuoa na tayari kazaa na Dokta nitakua nimejitia kitanzi na kujibuturia kistuli mwenyewe.

Matokeo ya semester ya mwsho yalitoka na mimi na Mercy sote tulifaulu vizur hakukuwa na mtu mwenye kimeo.
Japo nilikuwa bado naumia kumkosa Mercy lawama zangu zote nilizielekezea kwa Dokta na niliahidi kutokuja kumsamehe yule jamaa.

Ilikuwa mwez wa1 mwaka jana Mercy alijifungua mtoto wa kiume na anamuita Johnson, still Mercy ananisisitizia nimuoe lakini bado sioni kama kumuoa Mercy nitakuwa nimefanya jambo la msingi.

Mimi naye hali yangu ya kiafya ilichange ghafla nakumbuka ilikuwa mwez wa 12, 2022 hata graduation sikufanya, nilipatwa na kama kistroke flan yani upande wa kushoto haukuwa sawa. Nilishindwa kutembea, nilipoteza uwezo wa kuongea kwa takriban wiki Moja yani mdomo ulikuwa mzito sana ila nilikuwa natumia maandishi nilipokuwa nahitaji kuongea na mtu.

Nilipelekwa hospital nashukuru Mungu pamoja na madaktari walifanikisha kunipa huduma nikarudi katika hali yangu ya kawaida.
Nilitumia madawa tofaut tofaut ila kuna hiyo moja siwez isahau. Najua kuna wataalam wa afya humu wanaijua vizuri inaitwa "Aten" sijajua kama ndo jina linaishia hapo au linakirefu chake. Hii dawa bhna nakumbuka siku hiyo nilikuwa bado siwez kuongea mtaalam akaagiza ikachukuliwe hii dawa, ni tu vidonge tudogo sana kiumbo, niliambiwa nimeze kamoja tu kwa siku ila mziki wake hii dawa sio wa kitoto.

Hii dawa ukiitumia inakufanya upate ham ya kuongea, inakufanya ujihisi raha yani sinywi na sijawahi kutumia pombe lakini nature ya hii dawa inataka ifanane na tabia ya pombe. Nilikuwa naambiwa nimeze kimoja kwa siku lakini nilikuwa nataman nipige hata tutatu kwasababu yani vilikuwa vinanichangamsha kwanzia kichwani mpka sehem zingine za mwili.

Nilipona kabisa na mpka sasa niko poa.
Mercy naye anaendelea vizuri na mtoto wake na kila siku ananitafuta (hata asubuhi hii kashanitumia text) tunaongea na kuchat saana. Kila siku ananikumbusha kuhusu swala la ndoa na anasisitiza sana nimuoe kwani ananipenda lakini mimi bado sipo tayar kwasababu Mercy tayar anamtoto na sio mtoto tu ila mtoto ni wa Dokta mtu mwenye ROHO mbaya.

NIKIONA KUNA HAJA YA KULETA MREJESHO JUU YA MIMI NA MERCY BASI NITARUDI KUWAPA MREJESHO JUU YA NINI KINAENDELEA LAKINI MIMI BADO SIONI KAMA NINAWEZA KUMUOA MERCY.

Naomba kufunga Uzi wangu kwa kuwashukuru nyote na nawatakia kila lakheri katika safari yenu hapa duniani hasa katika ulimwengu wa mapenzi.

AHSANTENI 🫶🫶🫶.
Kosa siyo la dokta na utamlaumu bure hata kama asingekuwa dokta basi angeliwa na mwanaume mwingine.
Mwanamke asipokukubalia huwezi kuwa naye kimapenzi.
Kijana nishatongoza wengine wakanikubali na wengine wakakataa, na mwanamke akikukataa huwa anakataa vibaya mpk wewe mwenyew humtafuti.
Mercy angekuwa hajibu meseji yoyote ya Dr, huyo dr mwenyewe asingemfuata.
Kibaya usichokijua ni kuwa ndoto kuu ya mwanamke ni
1. Anapenda aolewe na mwanaume mwenye hela
 
Kuna wakati mapenzi yanatufanya kama watoto..

Kubali ama usikubali Wote tumepita Situation yake..Inaweza ikawa different Story ila lazma kwemye kichwa ukiiwaza unasema dah na mimi niliwahi kuwa zuzu..

Najua tunayo ila tunazificha na kudhihaki wwngine..

Kila Jambo kwemye maisha yetu tunayopitia ndo hutufanya kuwa imara na mashujaa na hutupa funzo ambalo ni aghalabu sana kurudia makosa hayo..
Na ndo maana wanasema "Past is our teacher.."

Ukimuuliza Kila mtu lazma ana story ambayo hajawahi kumwambia mtu yoyote kuhusu Mapenz hivyo kumcheka kijana wangu DeMostAdmired kwa sababu yeye kaamua kuidhihirisha kwa watu sio sawa
Hakika umenena ya kweli hakuna aliyeanza ujanja bila kupitia ujinga kwanza
 
Waooo....allt he best friend
Ila sikushauri kupa huyo dada ,hyo ndoa utakufa siku si zako mdogo wangu huyo anaona wewe ni dhaifu na atakupelekesha mnooo
Subiri ujibiwe yale majibu ya kutafuta gunia za mkaaa ukimuoa she never Loved you na kama alikupenda but she took your lover for granted that's why she did hurt you badly!!!
Pole sana kwa hilo nakuombea upate mke sahihi mwenye mapenzi ya kweli na wewe na kam vipi mblok huyo Mercy kabisa usipate kuwasiliana nae kwa namna yoyote ile
Utafute mtu mwingine,yeye alichagua pesa baasi apendwe na pesa maana maumivu alokusababishia ukimuoa jiandae kufa mapema
Km kwao wanapesa baasi wamtafutie mwanaume mwenye pesa mwenziwe amuoe huyo ni kichomi brooo atakuumiza mbaya kabisa
Delete,remove,futa kabisaa mawasiliano nayee...
Nimeuchukua ushaur
 
Mkimaliza kumpa ushauri juu ya Mercy na Doctor naomba mje uku kwa Jane mtoto wa Singida

Khaaa nimemaliza kusoma ila umenikera sana kwa jinsi unavyopenda kupitiliza.. huyu Mercy mwambie tu ukweli kwamba huwezi kumuoa maana nakuona tu unavyomuoa mercy. Pia Mercy akipata bwana mwenye pesa ndefu atapita naye.
Tungeweza kuwashauri watoto wetu huko vyuoni wangefanya mapenzi kuwa ya ziada sana na sio kuishia kupata uginjwa wa moyo kisa demu uliyekutana naye ukubwani.
 
Tuendeleee.......

Hapa nikaona kabisa Mercy hakuwa na mapenz na Dokta ila shida ni tamaa za pesa na Dokta alikuwa hana mpango wa kumuoa Mercy ila alihitaji kunikomoa tu. Nilihisi vile baadae baada ya siku moja Dokta kunitumia ujumbe "dogo wanaume tushafanya yetu ole wake hiyo mimba mkaitoe".

Hii text alinitumia siku moja kabla ya Mercy kufanya jaribio la kuitoa ile mimba. Hii text sikumuonesha Mercy niliona kama ntamchanganya tu na Haina maana.

DOKTA ALIMTIA MERCY MIMBA KWA MAKUSUDI NA ALIMLAGHAI KWA PESA ZAKE, HII KITU MERCY MWENYEWE NDO ALINAMBIA.

Niliwaza kama Mercy alikuwa hampendi Dokta ni kwanini alikubali kufanya nae tena kavu siku zake za hatari. Sikupata majibu sahihi nikaamua kuipotezea tu japo niliishia kuamini kuwa pesa ndo ilimshawishi Mercy mpka kubeba mimba.

Swala la Mercy kwenda namimi kwao akanitambulishe sikulikubali niliona Mercy hajafikiria kwa kutuliza akili na pia binafsi sikuwa tayar kuoa mwanamke mwenye mtoto.

SIKU YA KUAGANA NA MERCY ILIKUWA NI MAJONZI SANA.

Nilimsindikiza stand akapanda bus kuelekea kwao. Mimi naye nilibaki kwanza pale town kuna mambo yangu nilikuwa nayafatilia.

Nilikaa kama mwezi hivi ukizingatia hata kodi yangu bado ilikuwa inasoma. Kipindi kile nipo bado pale town niliamua nimtafute Merry, Merry alikuwa tayar kashaondoka kwenda Field alienda mkoa wa dodoma. Nilipomaliza mishe zangu nikapak vitu vyangu nikaondoka nyumbani namimi.

Mawasiliano na Mercy yaliendelea ila upande wangu nilianza kuona Haina tena haja ya kumtafuta mara kwa mara ila yeye alikuwa ananitafuta sana ananisihi nimuoe hata kama bado sijajipanga yeye kwao pesa so shida sana. Aliahidi ataomba pesa ya mtaji tuanze kuzichanga mdogo mdogo ila mimi nikaona kabisa Mercy nikimuoa na tayari kazaa na Dokta nitakua nimejitia kitanzi na kujibuturia kistuli mwenyewe.

Matokeo ya semester ya mwsho yalitoka na mimi na Mercy sote tulifaulu vizur hakukuwa na mtu mwenye kimeo.
Japo nilikuwa bado naumia kumkosa Mercy lawama zangu zote nilizielekezea kwa Dokta na niliahidi kutokuja kumsamehe yule jamaa.

Ilikuwa mwez wa1 mwaka jana Mercy alijifungua mtoto wa kiume na anamuita Johnson, still Mercy ananisisitizia nimuoe lakini bado sioni kama kumuoa Mercy nitakuwa nimefanya jambo la msingi.

Mimi naye hali yangu ya kiafya ilichange ghafla nakumbuka ilikuwa mwez wa 12, 2022 hata graduation sikufanya, nilipatwa na kama kistroke flan yani upande wa kushoto haukuwa sawa. Nilishindwa kutembea, nilipoteza uwezo wa kuongea kwa takriban wiki Moja yani mdomo ulikuwa mzito sana ila nilikuwa natumia maandishi nilipokuwa nahitaji kuongea na mtu.

Nilipelekwa hospital nashukuru Mungu pamoja na madaktari walifanikisha kunipa huduma nikarudi katika hali yangu ya kawaida.
Nilitumia madawa tofaut tofaut ila kuna hiyo moja siwez isahau. Najua kuna wataalam wa afya humu wanaijua vizuri inaitwa "Aten" sijajua kama ndo jina linaishia hapo au linakirefu chake. Hii dawa bhna nakumbuka siku hiyo nilikuwa bado siwez kuongea mtaalam akaagiza ikachukuliwe hii dawa, ni tu vidonge tudogo sana kiumbo, niliambiwa nimeze kamoja tu kwa siku ila mziki wake hii dawa sio wa kitoto.

Hii dawa ukiitumia inakufanya upate ham ya kuongea, inakufanya ujihisi raha yani sinywi na sijawahi kutumia pombe lakini nature ya hii dawa inataka ifanane na tabia ya pombe. Nilikuwa naambiwa nimeze kimoja kwa siku lakini nilikuwa nataman nipige hata tutatu kwasababu yani vilikuwa vinanichangamsha kwanzia kichwani mpka sehem zingine za mwili.

Nilipona kabisa na mpka sasa niko poa.
Mercy naye anaendelea vizuri na mtoto wake na kila siku ananitafuta (hata asubuhi hii kashanitumia text) tunaongea na kuchat saana. Kila siku ananikumbusha kuhusu swala la ndoa na anasisitiza sana nimuoe kwani ananipenda lakini mimi bado sipo tayar kwasababu Mercy tayar anamtoto na sio mtoto tu ila mtoto ni wa Dokta mtu mwenye ROHO mbaya.

NIKIONA KUNA HAJA YA KULETA MREJESHO JUU YA MIMI NA MERCY BASI NITARUDI KUWAPA MREJESHO JUU YA NINI KINAENDELEA LAKINI MIMI BADO SIONI KAMA NINAWEZA KUMUOA MERCY.

Naomba kufunga Uzi wangu kwa kuwashukuru nyote na nawatakia kila lakheri katika safari yenu hapa duniani hasa katika ulimwengu wa mapenzi.

AHSANTENI 🫶🫶🫶.
BOra hukuoa

Sasa wewe tafuta hela
Namba ya demu wa dokta tunayo😂
 
Mapenzi ni ujinga,mapenzi ni upuuzi,mapenzi ni upumbavu,

Ila

Mapenzi ni faraja,mapenzi ni amani,mapenzi ni kuwa na furaha

Yanii mapenzi ni indescribable

Mwamba umepitia yote big up sana imekukomaza na hutafanya maamuzi ya kijinga tena "kama wale wa redioni"kwako maana wanaopitia upande mmoja huishia kuumia au kufurahia sanaa!!!
 
Hakika
 
sikufurahishwa na kitendo cha moyo wako kutokupasuka na afya ya akili kuimarika!
Kwa namna huna akili hata unapopata maono ilibid ukufe ili wengi wajifunze kutotilia maanani vitu vya holela kama mapenzi!
Kanuni ya mapenzi ni simple, tuko pamoja kwa sababu tunaongea lugha moja
Tofauti na hapo mambo mengine yaendelee.
kuna story ya ...umalaya na ukahaba napenda namna inachukulia ngono kitu cha kawaida mno!
Wivu usio na gavana ni ulemavu na adui wa furaha!
Ile story ya uongo, i left alipoanza kuleta story za usalama kuhusika na yule katibu mkuu. Totally a lie
 
Shida nyingi inayowapata wanaoshindwa ku-move on ni zile hisia za kuwa huyo uliye naye ni wa kipekee sana, hauwezi kupata mwingine kama yeye.

Mambo ni tofauti kwa ground; kuna watu wengi tu ambao ni wema na bora kumzidi huyo. Epuka ukosefu wa exposure, jichanganye, ufungue moyo uangalie na wengine.

Ulikuwa unaishi vizuri kabla hajaja kwenye maisha yako, unaweza ukaishi vizuri zaidi hata akitoka kwenye maisha yako. Although it's hard; life has to, and MUST, go on.
Ushauri mzuri ila nyie inaonekana kabisa bado hamkuwahi kupenda. Expectations ukishakaa na mtu muda mrefu kidogo ndo zinazoumiza. Ukichanganya na mazoea, unakufa kabisa kihisia. Ukiona mtu ka move on kirahisi rahisi ujue huyo hakupenda basi kiukweli ukweli.
 
Back
Top Bottom