Daktari anasoma miaka 5-7 na mhandisi anasoma miaka kati ya 3-4 lakini ona tofauti ya mishahara kati yao hapa chini

Daktari anasoma miaka 5-7 na mhandisi anasoma miaka kati ya 3-4 lakini ona tofauti ya mishahara kati yao hapa chini

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Udaktari tiba ni fani nyeti na ngumu sana lakini cha kushangaza daktari anapata salary ya Tsh.1,500,000 gloss hukuhandisi wa Civil pale TANROADS(case study) anapata 2,000,000
Clinical officer/tabibu =950,000 huku Civil Technician=1,118,000 per month

Kwa staili hii case za rushwa zitaisha huko hospitali na vituo vya afya?

Tafadhali serikali wapeni madaktari uzito unaostahili kwenye malipo,wanatumia kusoma na wanaumia kazini.

Hata kwenye stahiki za posho na benefits zingine daktari hamfikii mhandisi lakini pia mhandisi hasa wa civil wako kwenye industry ambayo possibility ya yeye kupata pesa ni kubwa kuliko watu wa afya hadi semina zije.

Chonde chonde serikali mnapopanga viwango mliangalie hili na ule mpango wa kuwianisha malipo ya wafanyakazi walio na elimu moja limeishia wapi?
 
Udaktari tiba ni fani nyeti na ngumu sana lakini cha kushangaza daktari anapata salary ya tsh.1,500,000 gloss huku mhandisi wa civil pale Tanroads(case study) anapata 2,000,000
Clinical officer/tabibu =950,000 huku Civil Technician=1,118,000 per month
Kwa staili hii case za rushwa zitaisha huko hospitali na vituo vya afya? Tafadhali serikali wapeni madaktari uzito unaostahili kwenye malipo,wanatumia kusoma na wanaumia kazini.
Hata kwenye stahiki za posho na benefits zingine daktari hamfikii mhandisi lakini pia mhandisi hasa wa civil wako kwenye industry ambayo possibility ya yeye kupata pesa ni kubwa kuliko watu wa afya hadi semina zije.
Chonde chonde serikali mnapopanga viwango mliangalie hili na ule mpango wa kuwianisha malipo ya wafanyakazi walio na elimu moja limeishia wapi?
Mlinganisho wako sio sahihi kwa upande mmoja.

Umeongelea TANROADS ambayo ni Taasisi, zungumzia mshahara wa daktari katika Taasisi kama vile MUHIMBILI ndio utapata usawa.

Je,unafahamu mshahara wa Civil katika ngazi ya serikali ya mtaa ni kiasi gani na MD nae ni kiasi gani?!

Halafu kwenye Case ya CO umepotosha kidogo kwa kumzidishia kiasi fulani, yeye anapata 680,000 kwa mwezi na sio 980,000/.

Nawasilisha..!
 
Kwa hiyo wewe kigezo chako ni kukaa darasani tu? Huyo Mwalimu aliyekuwezesha wewe kujua kuishika kalamu analipwa sh ngapi!?
Kigezo ni muda wa darasani na ugumu wa kozi husika, mwalimu kozi yake sio ngumu na hakai darasani muda mrefu , kingine mtu kujua kitu au kusoma kuna mchango mkubwa WA mhusika mwenyewe
 
Walimu kwa sasa wanalipwa vizuri kuliko awali,na ukiangalia ugumu na risks za kazi ualimu sio mgumu wala sio risk Kama daktari
Hoja yako ulipoianza nimeipenda, ni kweli kumlipa Civil Engineer zaidi ya Daktari wa binadamu haiingii akilini. Labda aliyepanga ngazi za mishahara alikuwa Civil Engineer. Majukumu na uwajibikaji wao ni mbalimbàli lakini risk pia ni kubwa kwa Dokta kuliko Injinia. Hili ni tatizo lililoanzishwa na ukurupukaji na sasa waneshindwa kulitafutia dawa hata walipounda tume ya mishahara ambayo nayo imeshindwa kurekebisha tatizo zaidi ya kelele za "Tumefikia hatua nzuri".
Hata hivyo udhaifu huo hauwezi kuhalalisha uonezi wanaofanyiwa walimu. Ifike mahali tujue chanzo cha maarifa yote ni Mwalimu. Hata hiyo miaka 5 ya Daktari hawi peke yake, anakuwa na Mwalimu kwa muda huo wote. Daktari ni mwanafunzi kwa miaka 5-7 kama ulivyosema, lakini Mwalimu ni mwanafunzi muda wote wa maisha yake. Kazi yake ni kutotoa Madaktari, Mainjinia, Wachumi, na kuabort mbumbumbu ambao wengine wanageuka kupanga mshahara wake wakitokea kwenye siasa ambako ni Kokoro la waliomo na wasiokuwamo.
Mwalimu ni Kila kitu ingawaje anaonekana si kitu.
 
Back
Top Bottom