Daktari anasoma miaka 5-7 na mhandisi anasoma miaka kati ya 3-4 lakini ona tofauti ya mishahara kati yao hapa chini

Wangapi mmewafanyia operation na bado wakakumbwa na mauti kwenye mikono yenu ndugu yangu?? Mbona hatujawahi kuwalaumu
 
Okay, na wewe bomoa hiyo nyumba yako alafu tuone leo utalala wapi kama siyo kuwatafuta wahandisi hawa hawa unaowakashifu wakujengee nyingine
 
Unachekesha kweli rafiki yangu........but I think n ngumu kumielewa...nikiwa na muda I will come to make u understand
Inawezekana nikawa mgumu kuelewa na panaponipa ugumu ni hapa, daktari kasomea miaka kadhaa kwenye fani yake, na amefundishwa kutibu watu. So anapohitimu anakuwa amebobea katika kutibu watu, sasa ninashangaa hapa nyie madaktari mnaposema kazi yenu ni ngumu? Au unasema kazi yako inatumia akili nyingi?
 
Basi na wewe katibu chini ya mti bila sindano, umeme, x- ray machine na mchine zingine mnazotumia maabara
 
Kaka ukiona hivyo kuna matatu.
1)ugonjwa umefikia chronic labda mtu ana ufimbe tumboni kauacha umekuwa chronic ndio anakuja kutibiwa na kaka angu chronic stage kupona labda Mungu apende.
2)Siku za mtu zimefika kiimani
Maana mm niliwahi letewa mtu aliyekuwa na abnormal ECG yani mapigo ya moyo yanakuwa hayaeleweki.
Either kuna muda yanadunda kwanguvu na most of time yanadunda kila baada ya sekunde kadhaa.watu kam hawa hawatakiw kunywa pombe.
Yule jamaa alifakamia pombe.
Licha ya ku neutralize mapigo ya moyo wake!
Alikaa sawa then baada ya masaa kadhaa akasebenza.
Hapo utasema mm chanzo?Yesu kampenda zaid.
3)makosa ya kibinadam ambayo mara nyingi hufanywa na watu wa intern
Wangapi mmewafanyia operation na bado wakakumbwa na mauti kwenye mikono yenu ndugu yangu?? Mbona hatujawahi kuwalaumu
 
Sijamkashifu mtu mkuu nimeeleza ugumu wa kazi tunayoifanya mkuu
Okay, na wewe bomoa hiyo nyumba yako alafu tuone leo utalala wapi kama siyo kuwatafuta wahandisi hawa hawa unaowakashifu wakujengee nyingine
 
Me mwenyewe ni engineer ila doctors ni sahihi walipwe zaidi ya wanavyolipwa sasa napendekeza wazidishiwe mara mbili ya wanavyolipwa sasa hasa neurosurgeon ni viumbe adimu duniani hao watu shule zao ni ngumu sana, sasa hawa madaktari wanafunzi wana module inaitwa pathology sijui ni mwaka 2 au 3 aisee ni ngumu hatare then mazingira yao ya kazi si mazuri.naona hamuwaelewi kabisa wanachopigania na wao pia ndo maengineer wa mwili wa binadamu
 
Wewe ndo unatetea vitu ambavyo hujui hivi bila mwalimu hao madaktari wangekuwepo??

Hivi kwa akili zako hizi unaamini kitendo cha kumtoa mtu kwenye upumbavu na kumleta kwenye werevu ni kazi ndogo siyo??

Kumbuka walimu hao hao unaowachukulia poa ndio walikuwezesha wewe kupata ufahamu wa kujua kusoma na kuandika mpaka leo unapata jeuri ya kuandika uharo wako hapa
 
Kaka kuna kumtibia mtu kwa kumfanyia prescription.
Yani kwa maelezo ya mgonjwa ushajua nn anaumwa unaanza kumpatia dawa anaondoka.
Hapo nishaviua vifaa vya maabara vya diagnosis.
Mfano ww ukija na miupere sina haja ya kuchukua tissue nikikwangue uende ukapimwe aina gani ya fungal infection unayo.
Directly nitaangalia na kujua ww una opportunistic skin disease iliyosababishwa na candida albicans.
Nakupatia dawa unasepa.
Ukija ktk masuala ya x,ray na ultra sound hapo kidogo kaz ipo.
Lakin ktk masuala ya sindano na madawa kaz ya mafamasia hiyo
Basi na wewe katibu chini ya mti bila sindano, umeme, x- ray machine na mchine zingine mnazotumia maabara
 
Kaka ulishawahi kuletewa mgonjwa anatapatapa?!
Ukimwangalia body temperature imezidi mpk 48 degree celsius kwa mfano.
Hapo hapo ana difficulty in breathing
Hujui uanze kukitatua kipi akifia mikonon kwako una credit umejipunguzia ukifanya mara tatu km hvyo unaachishwa kaz.
Ase we acha tyuu
Kazi yako ngumu kivip?
 
Mkuu hapo kwa Clinical officer 950,000/= mbona kama sio kweli?

C.O anachukua 680,000/= kama take home na kabla huwa haizidi au haifiki 850k..ninaye ndugu yangu C.O
 
Sijamkashifu mtu mkuu nimeeleza ugumu wa kazi tunayoifanya mkuu
Ugumu upo kila sehemu usifikiri upo kwenu tu kikubwa ni kila mmoja kutambua na kuthamini profession ya mwenzake na siyo kujikweza muonekane too special kuliko wengine huo ni ushamba.
 
Mkuu ulijuaje hiyo module ni ngumu wakati wewe umesomea uhandisi?kumbuka kitu kigumu kwako kwa mwenzako anakiona rahisi.Ugumu wa kitu upo kwa mtu
 
Hizo ni changamoto tu za kazi sio kwa udaktar tu hata wahandisi wanakutana nazo ,
 
Mkuu ulijuaje hiyo module ni ngumu wakati wewe umesomea uhandisi?kumbuka kitu kigumu kwako kwa mwenzako anakiona rahisi.Ugumu wa kitu upo kwa mtu
Swali muhimu hili.
Lakin pia atuambie kana course yake ni nyepesi, kwanini ukienda pale coet watu wanadisco sana? lakin pia hata ukienda kwa watu wanaosoma kiswahili bado watu wanadisco tu?
 
Taasisi zinatofautia mishahara
Ndo Maana Mh President aliunda tume ya kurekebisha hiyo kitu. Mfano Accountant II wa Halimashauri anatofautiana tena sana na Accountant II NSSF
au wa NHIF
 
Kawaida Mhandisi anatumia akili kubwa kwenye kazi kuliko Daktari.

Daktari anakuuliza dalili za tatizo na kujua ugonjwa lakini Mhandisi anatumia akili nyingi kuvumbua tatizo
Wewe hakuna kazi ngumu kama ku deal na miili ya watu acha kabisa we jamaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…