TANZIA Daktari Bingwa wa Upandikizaji Sir Terence wa Moyo Afariki Dunia Akiwa na Miaka 93

TANZIA Daktari Bingwa wa Upandikizaji Sir Terence wa Moyo Afariki Dunia Akiwa na Miaka 93

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
557
Reaction score
1,039
Daktari bingwa aliyefanikisha upandikizaji wa kwanza wa moyo uliodumu nchini Uingereza, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 93.

Sir Terence English, alimfanyia upasuaji huo Keith Castle (52), aliyekuwa na uraibu wa uvutaji sigara, Agosti 1979.

Castle, shabiki wa timu ya soka ya Fulham, ambaye pia alipenda bia, aliendelea kuishi kwa takribani miaka sita zaidi. Shughuli zake za kuchangisha fedha zilipata umaarufu zaidi kwenye vyombo vya habari.

Kabla ya mafanikio ya upasuaji huo, hakuna mgonjwa wa moyo aliyeishi Uingereza kwa miezi kadhaa baada ya kupandikizwa moyo.

Sasa, zaidi ya miaka 45 baadaye, takribani wagonjwa 9,000 wamepandikizwa moyo nchini humo.

Sir Terence, aliyefariki dunia Jumapili Novemba 23, 2025 alijulikana pia kwa mapenzi yake ya magari. Katika maisha ya kustaafu alimiliki Rolls-Royces tatu na Mercedes 250S ya mwaka 1965.

Screenshot 2025-11-26 174629.png
 
Ungetushtua mapema, tungempelekea mgonjwa wetu, hivi huyu wa KWETU angebadilishiwa moyo si angeweza angalau kuwa na huruma kidogo, hilo lingeweza kuokoa maisha ya wale vijana wetu wengi, Rest easy.dr.
 
Apumzike kwa amani mtaalamu wetu wa Moyo.
 
Back
Top Bottom