Daktari jela kwa kumpa sumu mkewe kusudi ili mimba itoke

Daktari jela kwa kumpa sumu mkewe kusudi ili mimba itoke

Misheli baada ya kuona Kama dokta anajishauri sana, misheli akaenda benk kakopa pesa na kanunua nyumba ya familia iliyokamilika. Akamwambia mpenz wake dokta wahamie kwenye nyumba aliyonunua.

Dokta kamsifu ila kasema atahamia pale rasmi baada ya kufunga ndoa, waanze na mipango ya ndoa kwanza maana mimba inaendelea kukua. Sio vizur unavaa shela na tumbo limevimba linaonekana. Misheli kakubali.

Mipango ya ndoa imeenda vizur, baadae dokta kabadilika eti Hataki. Showoff's anapendekeza watafunga ndoa ya kiserikali kwa sherehe fupi Sana, jamaa na marafiki wa karibu watataarifiwa kuhudhuria . Misheli kasema haina shida.

Baadae Tena dokta akabadilika,akamwambia misheli kwamba wanatakiwa kusitisha kwanza mipango yao ya ndoa. Kuna vitu anahisi haviko sawa.Misheli anastaajabu, Ni vitu gani haviko sawa!

Dokta akasema hajawahi kufikiria kufunga ndoa bila uwepo wa wazazi wake na kwao wote ufunga ndoa za kidini sio za kiserikali. Kwaiyo havutiwi kabisa kufunga ndoa ya kiserikali bila uwepo wa ndugu zake.

Misheli akauliza Sasa itakuaje, dokta akasema wahairishe kwanza mpaka ajifungue, Kisha watafunga ndoa ya kidini maana kwa dini Yao Ni mwiko mjamzito kufungishwa ndoa. Misheli anaona haina budi kukubaliana na mpenz wake.

Ila moyoni misheli anahisi mpenz wake kabadilika sn,Kuna kitu hakiko sawa...

****************
Boss DeepPond nipo nje ya mada,naomba unipe uzoefu wako,Kuna surface ceiling fan nataka kununua,najiuliza kati ya Africab au Dolphin ipi ni brand nzuri bro? Hawa Africab vitu vyao ni imara kweli?
IMG-20240614-WA0006.jpg
 
Ilitokea Ohio, marekani, 2000

KWA KIFUPI Ni kwamba,
Binti mmoja baada ya kula sana ujana, miaka 33 anaamua kuseto kwa kutafuta mume wa ndoto zake afanye maisha.

Vigezo vyake Ni awe mrefu, handsome na professional na anabahatika kupata mchumba daktari na penz lao Moto Moto penzi linaingia changamoto baada ya binti kupata ujauzito wake wa kwanza kabla ya kufunga ndoa yao rasmi.

Ujauzito ule unahatarisha maisha ya binti baada ya mwanaume kurudiana na ex wake wanaodhamiria Mimba ile itoke kwa mume kumpatia binti, sumu ya taratibu itakayotoa ujauzito ule bila mtu yoyote yule kushtukia kama Kuna faulo play imefanyika.

WALITOKA HAPA JF au?
 
Maaskali Wamemtoa pale kumbe alkua bado mzima, kesho Yake wakamuwaisha haraka sana mahakamani. Kule lilisikilizwa wiki 2 kisha akahukumiwa

-miaka 10 jela kwa jaribio la kuua kwa sumu kwa kukusudia bila parole

-Miaka 5 kwa jaribio la kutoa mimba. Kwa kukusudia bila hiari ya mhusika
(marekani utoaji mimba unaruhusiwa, ila kwa hiari ya mhusika)

- Akafungiwa leseni yake ya udaktari miaka 20

NESI MAPEPE yeye akahukumiwa
-miaka 2 jela kwa kushiriki jaribio la kuua na kutoa mimba, ila amesamehewa mwaka 1 atautumikia kifungo Cha nje kwa makubaliano ya ushirikiano ktk kesi pamoja na kua shahidi dhidi ya dokta kwa plea bargain.

-akafungiwa leseni yake ya uuguzi kwa miaka 5

Court ikafungwa, wafungwa wakenda kutumikia jela.

Misheli ameendelea kulea mimba yake chini ya uangalizi maalum na kwa bahati mbaya, ilivofika miez 7 ile mimba ikatoka. Na kwenye hati ikaandikwa "mimba imetoka sababu ya wingi wa sumu ya cytotec kwenye kizazi"

Ikabidi Tena waendesha mashtaka Wa serikali wawarudishe Tena mahakamani toka jela, dokta na nesi mapepe waje kusomewa mashtaka Yao mapya na wahukumiwe upya kwa Kushiriki na kuitoa mimba ya misheli.

Wakasomewa tena mashtaka Yao na hawakua na lakujitetea zaidi ya kukiri, hakimu akagonga nyundo na wakaongezewa miaka 5 kila mmoja kwenye vifungo vyao vya awali.

THE END*
Credit:
-court Casefiles: Michelle Baker vs doctor mainad
- Documentary ya Forensic file "bitter pill to swallow"
Ile ya mjeda na nesi imeishia wapi mkuu
 
Back
Top Bottom