Daktari: Kajala hawezi kuzaa tena

Daktari: Kajala hawezi kuzaa tena

Lugano5

R I P
Joined
Jul 15, 2010
Posts
4,520
Reaction score
757
MAJANGA juu ya majanga! Siku chache kufuatia kufanyiwa kipimo na kubainika kuna tatizo kwenye ubongo baada ya kupigwa chupa kichwani kwenye Klabu ya New Maisha, Masaki jijini Dar, mkali wa sinema za Bongo, Kajala Masanja ‘Kay' amepata pigo lingine la daktari kumwambia hawezi kuzaa tena!

Kwa mujibu wa chanzo makini, Kajala alipewa maelezo hayo mapema wiki hii baada ya kufanyiwa kipimo na daktari bingwa wa hospitali moja iliyopo maeneo ya Morocco jijini Dar.

HISTORIA YA TATIZO
Kwa mujibu wa chanzo hicho, awali staa huyo alikuwa akisumbuliwa na tatizo la maumivu makali ya tumbo kwa kipindi kirefu na mara kwa mara hali iliyomlazimu kwenda kwenye hospitali mbalimbali za jijini Dar na kutibiwa lakini bila mafanikio.

"Unajua awali, aliamini amepata vidonda vya vitumbo (Ulcers).
"Pamoja na kupewa dawa mbalimbali kama ‘antibiotic' kama Amoxicillin, Tetracycline, Clarithromycin na Metronidazole, dawa zenye uwezo wa kupunguza uzalishaji wa tindikali tumboni lakini wapi.

HALI YAZIDI KUWA MBAYA
"Kutokana na hali yake kuzidi kuwa mbaya ndipo mwanzoni mwa wiki hii alipojisikia maumivu ya kupindukia hivyo alikwenda kwenye hospitali ile iliyopo Morocco na majibu ya vipimo yakaonesha kuwa ana uvimbe mkubwa kwenye kizazi!" Kilisema chanzo hicho.

Mnyetishaji wetu alidai kuwa, daktari huyo alimshauri kufanyiwa upasuaji wa haraka ili kuondoa uvimbe huo kwa sababu anaweza pia kunyemelewa na tatizo la kansa achilia mbali ishu ya kutozaa tena.

KAJALA AISHIWA NGUVU
"Yaani Kajala aliishiwa nguvu kabisa alipoambiwa maneno hayo na kujikuta akimwaga machozi," kilisema chanzo hicho.

KAJALA ASAKWA KUTHIBITISHA
Baada ya gazeti hili kupata habari hiyo, lilimtafuta Kajala ambapo alikiri kukutwa na tatizo hilo na ni kitu ambacho kimemchanganya sana hasa akimwangalia binti yake Paula (aliyezaa na Prodyuza wa Bongo Records, Paul Matthyasse ‘P Funk'), bado mdogo hivyo kujikuta akidondosha chozi.

"Yaani mtu akikuambia una ugonjwa kama huo, lazima uumie kwa kweli na mara nyingi namfikiria mtoto wangu bado mdogo. Kwa sasa najitahidi kufanya matibabu ya haraka ili kuondoa tatizo hilo," alisema Kajala.


KITAALAM
Kwa mujibu wa daktari mmoja wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambaye aliomba jina kusitiriwa, mwanamke akiwa na uvimbe mkubwa kwenye mfuko wa uzazi na kwa muda mrefu, matibabu yake salama ni kukiondoa kizazi.

"Lakini kuna wanawake wanapatwa na vimbe mbalimbali kwenye mfuko wa kizazi lakini si kubwa, ni rahisi kuondoa kwa kuchubua kitaalam na kizazi kikabaki salama," alisema daktari huyo.

WEMA BILA KUJALI
Wakati huohuo, Kajala amekumbwa na janga baada ya aliyekuwa shosti wake wa kufichiana siri kama siyo kutunziana mambo yao ya ndani, Wema Sepetu kumpaka runingani!

Baada ya Kajala kujishusha akisema yupo tayari kupatana na mwenzake, Wema, mwanadada huyo amemshukia Kajala akimwita ‘bogasi' yaani mjinga na kwamba ni mtu mzima lakini hana akili.

Akizungumza kupitia Clouds TV Jumanne iliyopita, Wema alifunguka kwamba hivi karibuni alishangazwa na kitendo cha Kajala kuandika vitu vya ajabu kwenye ukurasa wake wa Mtandao wa Instagram akisema amejishusha kumuomba msamaha ili aonewe huruma kwa watu na yeye (Wema) aonekane kuwa hafai.

"Kabla ya kuandika vile nilikuwa nipo tayari hata akija kwangu nimkaribishe nimsikilize lakini kwa sasa sitaki kuambatana na Kajala."Kajala ni mtu mzima lakini hana akili. Kuwa na Kajala ulikuwa ni upepo tu unapita. Alichokifanya mimi namuona bogus," alisema Wema.

Kwa upande wake, Kajala alimjibu kwa kifupi bila kutaka kubebanisha maneno kwa kusema: "Siku zote duniani ukikimbizana na chizi na wewe utaonekana chizi, nimejishusha, nimechoka."

Chanzo:GPL
 
wai kumbe ni shigongo ........
na hawa madaktari sikuhizi kama mabwabwa siri za wagonjwa ni baina ya doc na mgonjwa sasa kwenye magazeti inafikaje
 
wai kumbe ni shigongo ........
na hawa madaktari sikuhizi kama mabwabwa siri za wagonjwa ni baina ya doc na mgonjwa sasa kwenye magazeti inafikaje

Madaktari wa tz ni watu wa ajabu sana.
Ukiongea naye atakupa siri za wagonjwa woote unaowafahamu.
Ila kwa kuwa ni gpl habari haina mashiko
 
Hivi hakuna sheria ya kumshtaki huyu shigongo na kwa upuuzi anaoufanya? Au mpaka ile sheria ipitishwe? Anaudhi sana huyu, atuambie na matatizo waliyonayo ndugu zake.
 
Huyo daktari inabidi mumtaje ashitakiwe kama yupo kweli.

Maana amevunja sheria ya kuanika mambo ya wagonjwa.

Tunajua shingogo na kutunga ni mwaaaaaa
 
Inabidi sheria ianze sasa hii tabia ya waandishi wa haswa global na wengine imezidi sasa
 
Nikaja speeeed kumbe ni upuuzi wa shigongo na wahuni wenzake
 
umalaya unawaponza....wanatumiiiiiiiika loh adi majanga yanawavaa mscheeeeeeeew

Acha ujinga wewe hili tatizo halimaanishi unayosema wewe, nenda Ocean road au hospitali nyingine kubwa utakuta wazee ndio wengi na watoto wadogo wasio na sifa unazosema wewe. Tena uombe sana kauli yako isije ikakurudia wewe au mtu anayekuhusu, unless you dont believe in GOD.
 
wai kumbe ni shigongo ........
na hawa madaktari sikuhizi kama mabwabwa siri za wagonjwa ni baina ya doc na mgonjwa sasa kwenye magazeti inafikaje

Lakini habari ya Kajala haijaonyesha kuwa ni daktari ndie aliyetoa siri hii. Imesema tu chanzo makini sijui cha kuaminika so inawezekana K alimsimulia mtu na ndie aliyekwenda kutoa taarifa kwa Shigongo.

Huyo daktari alotajwa kutoka Muhimbili sio kwamba alikuwa anafafanua tu juu ya tatizo hili au mimi ndie nisiyeelewa?
 
Lakini habari ya Kajala haijaonyesha kuwa ni daktari ndie aliyetoa siri hii. Imesema tu chanzo makini sijui cha kuaminika so inawezekana K alimsimulia mtu na ndie aliyekwenda kutoa taarifa kwa Shigongo.

Huyo daktari alotajwa kutoka Muhimbili sio kwamba alikuwa anafafanua tu juu ya tatizo hili au mimi ndie nisiyeelewa?

Hata Mimi naona sio daktari aliyetoa siri yeye alitoa ufafanuzi wa hilo tatizo. Na ukute hizo habari za kutokuzaa ni mtu wake wa karibu katoa hizo habari zake za kutokuzaa tena
 
Tatizo waathirika tunawatetea hapa weeee, WAKIHOJIWA WENYEWE WANABWABWAJA kiulaini... ovyoooo.

Kweli kabisa CREOLE wao wenyewe hawazijuu haki zao..... ndio kwanza akifuatwa kuthibitisha badala ya kulaumu kwa kuingilia privacy yake yeye atajieleza huku akicheka.
 
Last edited by a moderator:
Lakini habari ya Kajala haijaonyesha kuwa ni daktari ndie aliyetoa siri hii. Imesema tu chanzo makini sijui cha kuaminika so inawezekana K alimsimulia mtu na ndie aliyekwenda kutoa taarifa kwa Shigongo.

Huyo daktari alotajwa kutoka Muhimbili sio kwamba alikuwa anafafanua tu juu ya tatizo hili au mimi ndie nisiyeelewa?

hawa madaktari ulioga mao viroba jogoo hosp wamaropoka tuu.....
gpl wameyapata hukohuko maaadili yahii taalim yamevurugika kabisaaaaa
 
Back
Top Bottom