Daktari mbaroni kwa kuiba dawa na vifaa vya hospitali

Daktari mbaroni kwa kuiba dawa na vifaa vya hospitali

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
75e4841408e504aca3551f4300dccd9e

Jeshi la Polisi mkoani Katavi, linamshikilia mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Inyonga wilayani mpanda, Calvin Mnaso (37) kwa tuhuma za kuiba dawa za binadamu pamoja na vifaa tiba katika kituo hicho.

Kamanda wa polisi mkoa wa Katavi, Benjamin Kuzaga ametoa taarifa jana kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa Desemba 19, baada ya polisi kupata taarifa za wizi katika kituo hicho.

Amesema baada ya taarifa hizo jeshi la polisi walianza kupekua katika nyumba za baadhi ya watu waliohisiwa kuhusika na wizi huo wakiwemo baadhi ya watumishi wa kituo hicho cha afya.

Kamanda Kuzaga amesema walipofika nyumbani kwa mtuhumiwa na kufanya upekuzi walifanikiwa kukamata mabox matano ya dawa mbalimbali za binadamu, vifaa vya kupima maradhi ya binadamu, vifaa vya kufanyia oparesheni na tohara, godoro moja pamoja na sindano ambavyo vyote ni mali ya serikali.

Hadi sasa mtuhumiwa huyo bado anashikiliwa na polisi na upelelezi ukikamilika anatarajiwa kufikishwa Mahakamani kwa mujibu wa sheria.
 
Watumishi ambao hawakutajilika enzi za kuanzia mkapa mwinyi na kikwete inabidi wajue hizo enzi zimeisha! Huko nyuma hapakuwa na mtumishi ambaye hakuwa mwizi. Hatakama hakuiba vitu lakini atakuwa ameiba muda wa mwajiri kwa kuchelewa kazini ama kutoroka ama kutoa sababu za uongo na mwisho wa mwezi unakinga mkono kudai mshahara! Who cares? Unaona hapo mali ya umma imekaa kizembe kizembe ukikataa kuiba wewe mwingine anaiba!

SASA HIVI MAMBO YAMEBADILIKA! Mtumishi kama unaona mshahara hautoshi unakaribia kukimbiwa na mke wako bora uache kazi usote mtaani kwa muda na tumia maharifa kufanya shughuri nyingine kupata kipato zaidi kuliko kwenda jela ambapo sio tu utapoteza mke (that is abvious) lakini pia utapoteza watoto na mali zote za kuhamishika! Watumishi hacha udokozi enzi hii ya JPM!
 
Back
Top Bottom