Dr. Sabaya ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi (CCM) wilaya ya Ubungo mwenye mafanikio makubwa ambapo ndani ya miaka miwili na nusu ya uongozi wake amejenga Ofisi ya kisasa ya jumuiya kwa ngazi ya wilaya, amechimba visima vya maji kata ya Mbezi, na kuja na miradi ya fumigation katika kata zote 14 za Wilaya ya Ubungo, miradi ya viti na hema kwa baadhi ya kata na Miradi ya Maegesho ya Magari.
Chanzo: Jambo Tv