John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Hivyo, zile sababu ambazo huwa zinatolewa na wataalam pindi mwanamke anapokutwa na hali hiyo huwa ni asilimia 20 tu ya sababu zote za kitaalamu ambazo zinajulikana.
Elias Kweyamba, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kina Mama amesema hayo na kuongeza kuwa utafiti wa wataalamu wa afya umeonesha asilimia kubwa ya sababu za mimba kuharibika ni vinasaba, ambapo inapotokea damu za wenza zinapishana huwa inachangia.
“Hii sababu huwa inachanganya kidogo na inatokana na group la damu, mfano mwanaume akiwa katika group la damu ambalo ni + (positive) kisha mwenza wake akiwa + pia hapo hakuna tatizo, na mtoto anaweza kuzaliwa vizuri.
“Ikitokea mwanamke akawa – (negative) kisha mwenza wake mwanaume akiwa + (chanya), mwanamke akipata ujauzito kisha mtoto tumboni akawa + (chanya), hapo atazaliwa salama, lakini wakati wa mtoto akizaliwa huwa kuna kinga maalum zinazojitengeneza kwenye mwili wa mwanamke kumlinda mtoto huyo tumboni.
“Hivyo, baada ya hapo zile kinga mwilini mwa mwanamke huwa zinabaki, baadaye wakati wa kutafuta mtoto mwingine zile kinga zinakuwa kizuizi cha mimba kukua.
"Mwanamke anaweza kushangaa anabeba ujauzito lakini kila baada ya muda unaharibika hata kabla haijakua, hiyo ni kwa kuwa zile kinga zilizojitengeneza awali zinaharibu ujauzito huo, ndipo hapo unaposikia watu wanasema 'fulani hawawezi kupata mtoto kutokana na damu kutofautiana'.
“Lakini ufafanuzi mwingine ni kuwa huyo mwanamke ambaye damu yake ipo tofauti na ya mwenza wake, atakumbana na hali hiyo kama wakati wa kujifungua damu ya mtoto ikaingiliana kwa wingi na ya mwanamke (mama mtoto).
"Lakini kama itatokea atajifungua bila damu za wawili hao kuingiliana kwa wingi, inamaana kuwa ile kinga haitakuwa imejitengeneza, hivyo anaweza kupata ujauzito kama kawaida na akajifungua vizuri.
“Hali hiyo inaweza kuendelea bila kuwa na tatizo ikiwa tu hakutakuwa na mwingiliano wa damu. Maana yake ni kuwa damu zitakuwa zinatofautiana lakini wenza wanaendelea kupata mtoto kama kawaida.
“Wenzetu katika nchi zilizoendelea, wanaweza kutegua mtego huo kutokana na teknolojia yao kuwa juu, wanachofanya mimba ikishatungwa, wanatumia vifaa maalum wanakuwa wanamuingizia damu yule mtoto hukohuko tumboni, hivyo zile kinga zilizop tumboni (zinazoharibu mimba) zinazidiwa nguvu ya kumzulu mtoto katika ukuaji tumboni,” anasema Dkt. Kweyamba.
Amesema sababu nyingine zinazochangia ujauzito kutoka ni upungufu wa kinga mwilini (siyo lazima iwe HIV, bali mwanamke anaweza kuwa na kinga dhahifu), maambukizi, mwanamke kuvuja damu nyingi wakati wa kujifungua na magonjwa mbalimbali.