Daktari Philip Isdor Mpango, kwanini unawasuta Watanzania wanaokupenda waliokuwa wanakuulizia ulipo?

Daktari Philip Isdor Mpango, kwanini unawasuta Watanzania wanaokupenda waliokuwa wanakuulizia ulipo?

Dalton elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
373
Reaction score
829
Prof Chachage Seithy Loth Chachage - alitumia neno ‘Collective Imbecilization’ kueleza uzuzu, ubwege, ufala wa pamoja unaoweza kufanywa na serikali

Hili jaribio la kuwapumbaza watu mamilioni kwa mpigo. Ni kama vile kuwakusanya watu milioni 50, ukawaweka ndani ya ukumbi mmoja kwa ukubwa huo

Ukafunga madirisha na milango, ukawanyunyizia dawa ya uzuzu, ubwege na ufala, ikawakolea, ukawaachia waende Duniani waendelee shughuli zao.

Haiwezekani, isipokuwa inawezekana watu wakapumbazwa kwa pamoja, wakafanywa mazuzu kwa pamoja, wakageuzwa mabwege kwa pamoja

Hata kama watu hao hawajioni ndani ya ukumbi huo na hawasikii harufu ya dawa ya ajabu wanayopuliziwa na kuwafanya kuwa mabwege na mazuzu.

Ipo mifumo imetumika, kutufanya sote tuwe mazuzu kama ambavyo alieleza Chachage alipokuwa akizungumzia “collective imbecilization”

Kwamba Makamu wa Rais ni special force au secret service? Kwamba Makamu wa Rais unatumwa kazi za siri za serikali? Ukajificha usijulikane ulipo?

Daktari Mpango, hivi ni kwanini unawaona watanzania wote ni mazuzu? Tunakubaliana kwamba, mazuzu yapo, lakini siyo wote ni mazuzu.

Dkt. Mpango, usilalamikie mitandao ya kijamii. Lawama peleka ofisi ya Makamu wa Rais. Watanzania wanayo haki ya kuhoji alipo Makamu wa Rais.

Dkt. Mpango, unashukuru kuombewa na watu gani? Wanakuombea wapi na vipi wakati unasema ulikuwa katika shughuli maalum na siyo ugonjwa?

Watanzania hawajui ulipokuwa ukipokea matibabu Korea Kusini. Ni wapekuzi wachache tulifahamu hadi jina la hospitali uliyofanyiwa upasuaji.

Ulikaa kimya umetumwa kazi ya kijasusi, mwezi mmoja baadae, uibukie kanisani halafu ukapokelewe Ikulu na Rais? Aah! Akili gani hii Daktari?

Ni mara ya pili hii, unazusha taharuki ukiwa katika matibabu, baadae unatoka kuzungumza na umma, unawasuta. Kuna kusema ulikuwa mgonjwa?

Na kwanini unawafokea watu waliokuwa wanauliza makamu wa Rais yupo wapi? Unasema ulikuwa unaona kila kitu ukiwa mafichoni, ukanyuti.

Sasa kwanini unawasuta leo watu wanaokupenda na walikuwa wanauliza ulipo? Kwamba hawakuwa na haki ya kuuliza Makamu wa Rais alipo?

Hii ni tabia mbaya na haitakiwi kuwa desturi kwa watawala kuwapumbaza watanzania. Tunakataa. Watanzania ndiyo mabosi wenu viongozi/watawala.

Unapotea, mwezi haujulikani ulipo. Waajiri wako tunaanza kukutafuta, umejificha sehemu (tunajua hospitali), unatuchora tu? Unaona upo sawa?

Ok! Baada ya mwezi mzima, unapatikana, unaibuka kanisani na Ikulu, kutufokea. Unatufokea watu tunakununulia kila kitu ambacho unakula na kuvaa?

Daktari Mpango, Rais ni bosi wako, sisi, watanzania ni waajiri wako, sisi ndiyo mabosi wako, pia mabosi wa Rais. Unawajibika kwa Rais, unatumikia wananchi.

Daktari, SIJAPENDA

Sources :

Brigedia Mtikila, MMM
 
Mpango anakusaidia nini hasa hadi utake kujua aliko au kujua status ya afya yake?

Awe mfu au mzima inakusaidia nini katika maisha yako kwani hakulishi wala kukuvisha.

Fuateni maisha yenu na familia zenu maisha yake muachieni yeye na familia yake.
 
Prof Chachage Seithy Loth Chachage - alitumia neno ‘Collective Imbecilization’ kueleza uzuzu, ubwege, ufala wa pamoja unaoweza kufanywa na serikali

Hili jaribio la kuwapumbaza watu mamilioni kwa mpigo. Ni kama vile kuwakusanya watu milioni 50, ukawaweka ndani ya

Brigedia Mtikila, MMM
Nakumbuka kipindi kachomoka wodini , anakohoa kwenye mic kuzuga hajaugua korona kunfurahisha jiwe aliyedai hakuna corona Tanzania
 
Sasa mada zote hizi kisa ni Makamu wa rais kwenda nje kikazi na kurudi akiwa mzima?

Kwani mlitaka nini sasa!
 
Sijui kwann wanaona kuumwa ni dhambi, kwani ni HIV mnaumwa hadi ufanye siri hivi?

Kuna ubaya gani kusema makamu wa Rais kaondoka leo kwenda nchi fulani kwa matibabu alafu baada ya wiki wakatangaza makamu kafanyiwa upasuaji baada ya wiki tena wakasema anaendelea vizuri katoka icu na baada ya wiki wakasema madokta wamesema watamruhusu wiki ijayo. Kuna ubaya gani kwani?

Au nyie viongozi mnahisi magonjwa tumeumbiwa sisi tu ila nyie hamtakiwi kuumwa?
 
Mpango anakusaidia nini hasa hadi utake kujua aliko au kujua status ya afya yake?

Awe mfu au mzima inakusaidia nini katika maisha yako kwani hakulishi wala kukuvisha.

Fuateni maisha yenu na familia zenu maisha yake muachieni yeye na familia yake.
Ukikubali kupokea uteuzi wa cheo kikubwa ktk nchi kama hicho cha Umakamu wa Rais, maana yake ni kwamba umekubali kuwa wewe umekuwa ni "Mali ya Umma" au Public Figure, kwa hiyo ni lazima pia ukubali kuyapokea matokeo yatokanayo na cheo hicho, ikiwamo na umma/wananchi kukufuatilia kila mahali uendako na kila kitu unachokifanya ktk maisha yako ya kila siku. Kila siku wananchi wanataka kujua uko wapi na unafanya nini.

Kama ktk maisha yako hutaki kufuatiliwa kwa namna hiyo, basi usikubali kupokea uteuzi au cheo cha namna hiyo ili uwe huru na uishi maisha yako privately, hakuna mtu atakayekufuatilia au kutaka kujua kama uko wapi.

Kukubali uteuzi ktk cheo kikubwa kama hiki pia ni kukubali kupoteza kiasi fulani cha uhuru wako binafsi ktk maisha yako.
 
Sasa mada zote hizi kisa ni Makamu wa rais kwenda nje kikazi na kurudi akiwa mzima?

Kwani mlitaka nini sasa!
Kama alikuwa kikazi kwann anashukuru kwa wananchi kumuombea?

We kwa akili yako makamo wa Rais anaweza kwenda kikazi nje ya nchi kwa mwezi mzima?
 
Mpango anakusaidia nini hasa hadi utake kujua aliko au kujua status ya afya yake?

Awe mfu au mzima inakusaidia nini katika maisha yako kwani hakulishi wala kukuvisha.

Fuateni maisha yenu na familia zenu maisha yake muachieni yeye na familia yake.
Maisha yake kwenye ofisi ya umma? Ni wapi umeona wanaulizia alipo mke wake, mjomba wake au kaka yake? Umakamu wa rais ni cheo Cha umma, sio jambo binafsi.
 
Kama alikuwa kikazi kwann anashukuru kwa wananchi kumuombea?

We kwa akili yako makamo wa Rais anaweza kwenda kikazi nje ya nchi kwa mwezi mzima?
Sasa hata kama hakwenda kwa kazi kwani ni sheria ipi inamzuia kwenda nje kwa masuala binafsi?
 
Nimeshangaa sana kwa statement aliyoitoa kanisani leo. U-daktari mwingine haufai kabisa.
 
Mh. Mpango tunakupenda, huwezi kutokuonekana kwa zaidi ya mwezi, watoto wako tusione taharuki hasa pale ukinya unapotawala, na pale tulipopata maafa wewe baba hata salamu za pole hazisikiki hata kama uko mbali kwa kazi maalum bado ujumbe wa pole ungetufikia, serikali mpaka inakaa kimya hivyo huku watu wakihangaika kutafuta kiongozi wetu yuko wapi haikuwa sawa.

Magazeti ya leo yameandika sana kuhusu "Mpango atoa yake ya moyoni", mimi nilidhani moja ya yale ya moyoni ni kutuomba radhi waTanzania umehangaisha mioyo yetu kwani kazi maalumu ya Makamu wa Rais ambayo watanzania hawatakiwi kuijua ni ipi?

TUNAKUPENDA Mh. Mpango ndiyo maana watu wako tumehangaika, kujua kipi kimekupata, Tumekusamehe bure.
 
Dr. Mpango kimoyomoyo anawapa big up sana watanzania sema tu hadharani akisema itakuwa tusi kwa wengine ambao hawakitimiza wajibu wa kututaarifu alipo. Sie tunamuelewa. Endelea na kazi Dr. Mpango,ukiumwa tu hata mafua,tuambie tuanze sala. Yaani mpaka utimize kusudi la Mungu. Na ujue tunajifunza kwako na kwa unayopitia,ishi.
 
Back
Top Bottom