Daktari Philip Isdor Mpango, kwanini unawasuta Watanzania wanaokupenda waliokuwa wanakuulizia ulipo?

Daktari Philip Isdor Mpango, kwanini unawasuta Watanzania wanaokupenda waliokuwa wanakuulizia ulipo?

Mh. Mpango tunakupenda, huwezi kutokuonekana kwa zaidi ya mwezi, watoto wako tusione taharuki hasa pale ukinya unapotawala, na pale tulipopata maafa wewe baba hata salamu za pole hazisikiki hata kama uko mbali kwa kazi maalum bado ujumbe wa pole ungetufikia, serikali mpaka inakaa kimya hivyo huku watu wakihangaika kutafuta kiongozi wetu yuko wapi haikuwa sawa.

Magazeti ya leo yameandika sana kuhusu "Mpango atoa yake ya moyoni", mimi nilidhani moja ya yale ya moyoni ni kutuomba radhi waTanzania umehangaisha mioyo yetu kwani kazi maalumu ya Makamu wa Rais ambayo watanzania hawatakiwi kuijua ni ipi?

TUNAKUPENDA Mh. Mpango ndiyo maana watu wako tumehangaika, kujua kipi kimekupata, Tumekusamehe bure.
Mpende baba yako na mama yako inatosha,wanafiki
 
Dr. Mpango kimoyomoyo anawapa big up sana watanzania sema tu hadharani akisema itakuwa tusi kwa wengine ambao hawakitimiza wajibu wa kututaarifu alipo. Sie tunamuelewa. Endelea na kazi Dr. Mpango,ukiumwa tu hata mafua,tuambie tuanze sala. Yaani mpaka utimize kusudi la Mungu. Na ujue tunajifunza kwako na kwa unayopitia,ishi.
anapitia yepi mabaya kiasi wewe mgalatia unajifunza? acha viongozi wapige kazi
 
anapitia yepi mabaya kiasi wewe mgalatia unajifunza? acha viongozi wapige kazi
Nionyeshe nilipotaja neno mabaya? Wewe umetoka ndotoni na mawazo yako yenye 'mabaya' ukatafuta pa kuyaweka. Mimi sio mgalatia mimi ni muislamu. Sasa upupu wako na labeling based na ubaguzi uache. Ukishanawa uso rudi hapa utajua kuwa Dr.Mpango yuko anaendelea na kazi zake sijamshika na mimi niko hapa napoteza muda kutoa maoni yangu.
 
Nionyeshe nilipotaja neno mabaya? Wewe umetoka ndotoni na mawazo yako yenye 'mabaya' ukatafuta pa kuyaweka. Mimi sio mgalatia mimi ni muislamu. Sasa upupu wako na labeling based na ubaguzi uache. Ukishanawa uso rudi hapa utajua kuwa Dr.Mpango yuko anaendelea na kazi zake sijamshika na mimi niko hapa Napoteza muda kutoa maoni yangu.
Huo muda sasa utaenda kupotezea jela,kumbe huna shuhuri ya kufanya binti
 
Huo muda sasa utaenda kupotezea jela,kumbe huna shuhuri ya kufanya binti
Binadamu asiyeweza kuandika 'shughuli' nae wakunitishia mimi. Jela ya wapi? Ni rahisi mimi kuwa Waziri Mkuu kuliko kwenda jela. Shughuli ya kufanya ya kuniingizia kipato sina ila bando ninalo,kwahiyo niko hapa full time mpaka kazi ipatikane. Utake usitake utaniona hapa. Haya njoo na kitisho kingine...... !
 
Binadamu asiyeweza kuandika 'shughuli' nae wakunitishia mimi. Jela ya wapi? Ni rahisi mimi kuwa Waziri Mkuu kuliko kwenda jela. Shughuli ya kufanya ya kuniingizia kipato sina ila bando ninalo,kwahiyo niko hapa full time mpaka kazi ipatikane. Utake usitake utaniona hapa. Haya njoo na kitisho kingine...... !
Hata vichaa milembe wana prime minister wao
 
Hata vichaa milembe wana prime minister wao
Mirembe sio Milembe. Uzuri sikusema Waziri Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi UDOM au wa JMT au wa Mirembe. Ila kwakuwa mwenzangu ni mwenyeji hapo Mirembe au uliishi hapo ukawa Prime Minister,i can only respect changamoto unazopitia na naishia hapa kwasasa. Ukishajifunza kuandika na kutoka Rehab tutaendelea.
 
Jiulizeni watz ni mamilioni kias gan ametumia yeye na timu nzima ya wapambe na security personnel kwa mwezi mzima na watz hatuambiwi ukweli,hii nchi viongozi wanatudharau sn ,hakukosea alieimba wanatuona nyani tu
 
Prof Chachage Seithy Loth Chachage - alitumia neno ‘Collective Imbecilization’ kueleza uzuzu, ubwege, ufala wa pamoja unaoweza kufanywa na serikali

Hili jaribio la kuwapumbaza watu mamilioni kwa mpigo. Ni kama vile kuwakusanya watu milioni 50, ukawaweka ndani ya ukumbi mmoja kwa ukubwa huo

Ukafunga madirisha na milango, ukawanyunyizia dawa ya uzuzu, ubwege na ufala, ikawakolea, ukawaachia waende Duniani waendelee shughuli zao.

Haiwezekani, isipokuwa inawezekana watu wakapumbazwa kwa pamoja, wakafanywa mazuzu kwa pamoja, wakageuzwa mabwege kwa pamoja

Hata kama watu hao hawajioni ndani ya ukumbi huo na hawasikii harufu ya dawa ya ajabu wanayopuliziwa na kuwafanya kuwa mabwege na mazuzu.

Ipo mifumo imetumika, kutufanya sote tuwe mazuzu kama ambavyo alieleza Chachage alipokuwa akizungumzia “collective imbecilization”

Kwamba Makamu wa Rais ni special force au secret service? Kwamba Makamu wa Rais unatumwa kazi za siri za serikali? Ukajificha usijulikane ulipo?

Daktari Mpango, hivi ni kwanini unawaona watanzania wote ni mazuzu? Tunakubaliana kwamba, mazuzu yapo, lakini siyo wote ni mazuzu.

Dkt. Mpango, usilalamikie mitandao ya kijamii. Lawama peleka ofisi ya Makamu wa Rais. Watanzania wanayo haki ya kuhoji alipo Makamu wa Rais.

Dkt. Mpango, unashukuru kuombewa na watu gani? Wanakuombea wapi na vipi wakati unasema ulikuwa katika shughuli maalum na siyo ugonjwa?

Watanzania hawajui ulipokuwa ukipokea matibabu Korea Kusini. Ni wapekuzi wachache tulifahamu hadi jina la hospitali uliyofanyiwa upasuaji.

Ulikaa kimya umetumwa kazi ya kijasusi, mwezi mmoja baadae, uibukie kanisani halafu ukapokelewe Ikulu na Rais? Aah! Akili gani hii Daktari?

Ni mara ya pili hii, unazusha taharuki ukiwa katika matibabu, baadae unatoka kuzungumza na umma, unawasuta. Kuna kusema ulikuwa mgonjwa?

Na kwanini unawafokea watu waliokuwa wanauliza makamu wa Rais yupo wapi? Unasema ulikuwa unaona kila kitu ukiwa mafichoni, ukanyuti.

Sasa kwanini unawasuta leo watu wanaokupenda na walikuwa wanauliza ulipo? Kwamba hawakuwa na haki ya kuuliza Makamu wa Rais alipo?

Hii ni tabia mbaya na haitakiwi kuwa desturi kwa watawala kuwapumbaza watanzania. Tunakataa. Watanzania ndiyo mabosi wenu viongozi/watawala.

Unapotea, mwezi haujulikani ulipo. Waajiri wako tunaanza kukutafuta, umejificha sehemu (tunajua hospitali), unatuchora tu? Unaona upo sawa?

Ok! Baada ya mwezi mzima, unapatikana, unaibuka kanisani na Ikulu, kutufokea. Unatufokea watu tunakununulia kila kitu ambacho unakula na kuvaa?

Daktari Mpango, Rais ni bosi wako, sisi, watanzania ni waajiri wako, sisi ndiyo mabosi wako, pia mabosi wa Rais. Unawajibika kwa Rais, unatumikia wananchi.

Daktari, SIJAPENDA

Sources :

Brigedia Mtikila, MMM
Alichofanyanyia watz, nafikili ni mda sasa na Watz tumtenge kuanzia sasa mbwai mbwai
 
Pamoja na majadiliano haya,niwaombe Ndugu zangu tusivuke mipaka yake ALLAH, muumba mbingu na nchi kwani adhabu zake ni kali saana na kwake ni kuwa na inakuwa.
 
Back
Top Bottom