Daktari wa ultrasound amekataa kunambia jinsia ya vitoto vyangu

Daktari wa ultrasound amekataa kunambia jinsia ya vitoto vyangu

Sikuongea chochote na Dr kabla ya kupima. Ni kweli wife anahudhuria clinic hapo hapo ila jengo la clinic ya wazaz ni mbali kabisa na X ray, maabara na US. Pia wahudumu wake ni tofauti.
1. Machine yngne zinazotumika kufanya us n 2D ambazo co nzuri sana ku tambua sex ya mtoto zaid mpimaj hutumia signs tu Ku determine sex ambayo Mara nyng sio exactly kuwa sahh so labda upate sehem ambao sana 3D -4D machine

2. Maadili hayaruhusu kwasbb us machine ni dependent operative mpmaji anariporit mile anachokiona so wkt mwengne kunakuwa na errors ambazo znaweza kusabibishwa na mpmaji au machine yenyewe so anaweza kuona signs ambozo n MTT wa kike kuikawa hakuona sahh au machine ilileta errors so anaweza kuripoti kitu sicho then maabadae ilkaleta shida. Mfno umeambiwa MTT wako ni wakiume then mkeo akajifungua MTT wakike tena labda ni operation kunaweza kukaleta mkanganyiko mama akasema amebadilishiwa mtoto.

3. Sio indication kufanya obs USS kwa sabb ya kujua sex tu labda kuwe naishu itakayohusiana na maswali ya kisheria kiulazima
 
Kuna daktari aliniambia kuna wazazi wakijua jinsia ya mtoto na ikatokea walikuwa na matamanio tofauti, hupelekea athari hasi kwa ujauzito wenyewe. Na hii ndio sababu kuna wakati wanaamua kutokuambia.
 
Mimi wife akiwa mjamzito sikutaka kabisa tujue jinsia ya mtoto, nilipende iwe surprise kwangu, na kweli mara zote mbili sikujua jinsia ya mtoto mpk wife alupojifungua na sasa nina watoto wa jinsia moja ya kiume.
 
Hongera mkuu kwa kutarajia pacha. Nilibahatika kupata pacha wote wa kiume miaka miwili iliyopita. Sisi walituambia jinsia ya mmoja wakati mimba ina miez 6. Mtoto mwingine hawajafanikiwa kumchungulia jinsia yake mpaka masaa machache kabla wife hajafanyiwa operation ndo akajigeuza tukajua nae wa kiume.
 
Hiyo operation naogopa sana. Ila mimba ya kwanza alijifungua kawaida mtoto mmoja.
 
Ninavyojua mimi kuna couple walitaka kujulishwa jinsia ya mtoto wakaambiwa ni wa kike
Hapo wazazi wakaanza kuandaa kila kitu kwa ajili ya mtoto wa kike
Kama nguo za rangi ya purple na kupaka chumba pink na mazagazaga yote
Siku ya siku akjifungua mvulana daa
Hasira ilibidi wafungue kesi na kuishtaki hospitali
Hii kesi ilikuwa ni [emoji636] sio bongo lakini

Huenda anajua madhara yake ndio maana akakataa
 
Mimi wife akiwa mjamzito sikutaka kabisa tujue jinsia ya mtoto, nilipende iwe surprise kwangu, na kweli mara zote mbili sikujua jinsia ya mtoto mpk wife alupojifungua na sasa nina watoto wa jinsia moja ya kiume.
ili mimi niongee ukweli, napenda sana watoto wa kiume
 
Ulichoandika ni ukweli mtupu LAKINI kuna tofauti kubwa kati ya kukataa na kusema kwa sasa nashindwa kudetermine kama ni KE au ME. Hii sheria inayozuia wazazi wasiambiwe jinsia ya mtoto/watoto wao ni ya nchi gani!?

Nimewahi kusikia makosa wazazi watarajiwa kuambiwa mtoto ni ME/KE na ikawa ni vice versa lakini hii sheria ya kuzuia wazazi wasijue jinsia ya kijacho sijawahi kuisikia.

MULTIPLE PREGNANCY MEANS MORE THAN ON CHILD. dr kisheria haruhusiwi kusema jinsia ya mtoto. pamoja kama akiwa single unaweza kuona au usione inategemea na mtoto amekaaje, kama amemgeukia mama sio rahisi kuona ila kama amegeuka kukuangalia ni rahisi ila taaluma hairuhusiwi. Naweza nikakuambia kimafumbo labda finger like structure au mouth like structure. hapo unaweza chambua mwenyewe.
Tuje kwenye Multiple pregnancy yani watoto zaidi ya wawili ni kuwa mara nyingi ni ngumu kwa sababu ya space yao inakua finyu haswa kuziangalia structure zao. hvyo ngumu kuweza kujua ila wengine kama ukaaji wao upo vizuri unaweza kuona. OVa.
 
Ni haki yako wewe kama mzazi kujua jinsia ya watoto wako ambao wanaogelea kwenye amniotic fluid.

Kwa haraka haraka huyo Doc kashindwa kutambua jinsia ya watoto ndio maana aliua soo kwa kuchomekea mambo ya dini.
 
Kuna case ya hospital ya Temeke US ilionyesha mama ana watoto mapacha siku ya kujifungua mama akajifungua mtoto mmoja, ilikuwa ishu kubwa sana ilifika hadi wizarani, wizara ikateuwa watu wa kwenda kufanya uchunguzi.... Kubaini kama mama alijifungua mapacha na mmoja kuibiwa au la

Sasa hapo Dr akikuambia jinsia ya watoto then mama akija kujifungua wanaume watupu na Dr kakuambia U Saund ilimuonyesha Me na Ke hapo si patachimbika??
 
Mkuu mpeleke hospital za private mfano AGA KHAN, REGENCY etc. Nakushauri hivyo kwa sababu mke wangu alikuwa anaenda clinic katika hospital fulani hapa mjini Daslam akawa anapiaga ultrasound hizo na kupewa majibu kuwa mtoto yuko vizuri yupo katika njia yake. Hivyo asiwe na wasi wasi wowote. ila siku ya kujifungua nilishangaa na kusikitika sana waliposema kuwa mtoto hajakaa sawa katika njia yake. Pia wakatoa muongozo kuwa inabidi afanyiwe upasuaji. niliwamaindi sana. Ikabidi nijikakamue kisabuni nimpeleke pale AGA KHAN kwa huduma bora Zaidi. Nilipofika walisikiitika sana kuwa angechelewa angeweza kupoteza mtoto au yeye au wote kwa pamoja.

Take care.
Uzazi una mengi shukuru Mungu Yuko hai.
 
MULTIPLE PREGNANCY MEANS MORE THAN ON CHILD. dr kisheria haruhusiwi kusema jinsia ya mtoto. pamoja kama akiwa single unaweza kuona au usione inategemea na mtoto amekaaje, kama amemgeukia mama sio rahisi kuona ila kama amegeuka kukuangalia ni rahisi ila taaluma hairuhusiwi. Naweza nikakuambia kimafumbo labda finger like structure au mouth like structure. hapo unaweza chambua mwenyewe.
Tuje kwenye Multiple pregnancy yani watoto zaidi ya wawili ni kuwa mara nyingi ni ngumu kwa sababu ya space yao inakua finyu haswa kuziangalia structure zao. hvyo ngumu kuweza kujua ila wengine kama ukaaji wao upo vizuri unaweza kuona. OVa.

Is this true

Cc Kingsmann
 
Leo nililazimika kumsindikiza mke wangu hospital kupima mimba kwa ultrasound. Alipohudhuria clinic Mara ya mwisho nurse alisema mke wangu anaongezeka kilo kwa kasi sana, na Umri wa mimba hauendani na kimo/ukubwa wa tumbo. Yaani ndo kafunga mwez wa sita lakin mimba yake sawa na ya miezi 9. Tumbo kubwa kweli kweli.

Sasa Leo tukaenda kucheki kwa US majibu yakaja wife ana mapacha. Amesifia watoto wana afya nzuri na wanacheza vizuri(watundu kama Mimi baba yao) kisha akatoa hongera kwa wazazi, na kutuambia tarehe ya kujifungua. Kilichonifanya niandike Uzi huu ni kwamba, nilipomwuliza jinsia akajibu hawezi kusema hata Mungu hapendi. Ni haki kujibiwa hivi? Anakwepa nini au ni imani zake kidini au taaluma hairuhusu?
Huenda hana utaalam wa kutosha wa kuona jinsia ya mtoto aliyetumboni. Akaamua kuingizia mambo ya Mungu kumbe kashindwa kutambua jinsia!!
 
Leo nililazimika kumsindikiza mke wangu hospital kupima mimba kwa ultrasound. Alipohudhuria clinic Mara ya mwisho nurse alisema mke wangu anaongezeka kilo kwa kasi sana, na Umri wa mimba hauendani na kimo/ukubwa wa tumbo. Yaani ndo kafunga mwez wa sita lakin mimba yake sawa na ya miezi 9. Tumbo kubwa kweli kweli.

Sasa Leo tukaenda kucheki kwa US majibu yakaja wife ana mapacha. Amesifia watoto wana afya nzuri na wanacheza vizuri(watundu kama Mimi baba yao) kisha akatoa hongera kwa wazazi, na kutuambia tarehe ya kujifungua. Kilichonifanya niandike Uzi huu ni kwamba, nilipomwuliza jinsia akajibu hawezi kusema hata Mungu hapendi. Ni haki kujibiwa hivi? Anakwepa nini au ni imani zake kidini au taaluma hairuhusu?

Maadili ya kazi yao hayaruhusu kufanya hivyo, na kama ikitokea, basi ujue ameenda kinyume na maadili ya kazi
 
Madokta kalio kama huyu wanaochanganya dini kwenye taaluma hawafai kua na leseni.
Labda aseme tu ukweli hajui jinsi ya kuangalia jinsia sio kukaa anakupiga sound.
 
Wazazi wengine hukosa utashi na uvumilivu pale wanapogundua mtoto waliekua wanatarajia sio.
Mapenzi ama matunzo kwa mama kijacho hupungua na hivyo kusababisha changamoto kadhaa kabla na baada ya kujifungua.
 
Je, wewe na mkeo kuna jinsia mnayopendelea na Dr. huyo anafahamu? Madaktari wetu wengi hawana ujuzi wa kutambua jinsia na hivyo kuona ni bora kutosema kuliko lawama baadae.
Pia, naomba ubadili kichwa cha uzi huu toka " dr-wa-ultrasound-amekataa-kunambia-jinsia-ya-vitoto-vyangu" kwenda " dr-wa-ultrasound-amekataa-kunambia-jinsia-ya-watoto-wetu"
halafu radiographer sio daktari
 
Back
Top Bottom