luck sabasaba,
Unaposema mtaji upo.. Hio ni relative term. Mtaji upo kiasi gani?
Tofatuti ya uendeshaji wa biashara ya dala dala na gari la mizigo ni hivi;-
Dala dala
Kama una mtaji wa kutosha gari zuri lenye malengo yanayoeleweka ni Coaster kuliko Hiace hasa kwa safari za mizunguko ndani ya eneo (mji) husika. Mara nyingi mwenye Hiace hufaidi vema akiwa kapata contracts kwenye maeneo kama mahoteli, shule ama hizi kampuni za simu (hasa kwa malengo ya kusafiria katika taratibu zao za promotion bila kujali kampuni gani ya simu).
Upande wa Coaster hata gari lolote ni bora ukalianza mwenyewe na usiguse kabisa 2nd hand... Kawaida bei za Coaster ni million 39-45, ukiifanya dala dala inakuingizia sio less than 80 kwa siku ambayo ukijumulisa unakuta pesa ya Coaster inarudi ndani ya miezi 20-24 tegemeana na hali ya gari. Ila kama una network nzuri ya biashara ya gari hilo kwa kupata tenda za misafa mirefu kwa kukodiwa (kama misiba, harusi, watu wa kwaya n.k); then pesa yako inarudi hata miezi 16. Mfano kukodi coaster toka Dar hadi Mbeya kwa safari ya siku 3-4 ni kiasi cha 1.4... Ukiwa na safari za mara kwa mara za hivo then u see what I mean.
Gari la mizigo
Kama hujawahi kufanya hio biashara kwa kiasi fulani mwanzoni unababaika saana. Inatakiwa uwe in contact na mtu ambae ni mzoefu wa hio biashara huyo mtu awe ndani ya mtandao wa watu wenye magari sababu if you are not in it (Uliza vijiwe vya magari ya mizigo Dar) then unaweza kuwa doomed! Gari la mizigo inategemea ni gari gani maana yametofautiana ukubwa, ukubwa wa gari yako una determine zaidi aina ya mizigo utalenga na mahala gari litaenda. Na hii inategemea pia upo wapi, je wateja ni wafanya biashara wa bidhaa? Mazao? Mifugo? n.k..
Tuchukulie Fuso kawaida inakuwa na uwezo wa kubeba Tan 7 (Ni nafasi ndogo sana kwa gari ya mizigo - unaendesha biashara kihasara/faida ndogo). Wengi waki oder magari yao makubwa (kwa upande wa Fuso) hupeleka kwa ajili ya kuyaboresha kuongeza bodi iwe na uwezo wa kubeba mzigo mara mbili yake... Mara nyingi toka tan 7 kwenda tani 14/16 kwa kubadilisha hio gari kwenda double diff.
Hapa ninalo jaribu kukuambia ni kuwa angalia ni soko gani utaweza kulimudu ndio li determine aina ya gari unataka kununua. Kama utakuwa well connected upande wa mizigo then be it... Kama dala dala then be it.
Word of Advice: Gari yako mpya kama ni Coaster ukilipiga tu mstari basi unakuwa umeliua kibiashara za masafa marefu.