Elections 2010 Daladala wajipatia pesa kupeperusha bendera za CCM Arusha

Ibrah

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2007
Posts
2,730
Reaction score
530
Nimehakikishiwa kuwa bendera za CCM sasa ni dili kwani baadhi ya madereva wa Daladala Arusha wanakunja shilingi elfu 10 kwa kukubali kupeperusha bendera za CCM kwenye Magari yao!

Mgombea wa CCM Arusha amepaniki maana daladala nyingi za hapa mjini zinapeperusha bendera za CHADEMA ambazo hutolewa bure na kwa hiyari. Hali hiyo imepelekea Wapambe wa mgombea huyo kuwashawishi madereva wa daladala kupokea bendera za CCM na kuzipeperusha kwenye magari yao.

Inaonekana Mgombea Ubunge wa CCM Arusha ana pesa nyingi sana maana kama Wapambe wanaweza kutoa shilingi elfu 10 ili kupeperusha bendera kwenye gari wao wanabaki na ngapi?

Wajinga ndio waliwao!
 
Usijali sana wenye sauti ni sisi wapigakura na wala siyo wao.

Hata hao wanaopepeprusha bendera ya CCM kwa ugali kura zao haziendi CCM. Hapo ndipo mtu atabana na masikio yake.
 
Du kweli hawa jamaa hawafai yaani wanataka uongozi kwa nguvu zote, lakini mwaka huu wataisoma!
 
Hii tabia ya kujipendekeza na vibendera vya CCM huwa inanikera sana hasa kwa watu wanaofanya shughuri zao maeneo ambayo ni illegal Dodoma mjini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…