Ibrah
JF-Expert Member
- Mar 22, 2007
- 2,730
- 530
Nimehakikishiwa kuwa bendera za CCM sasa ni dili kwani baadhi ya madereva wa Daladala Arusha wanakunja shilingi elfu 10 kwa kukubali kupeperusha bendera za CCM kwenye Magari yao!
Mgombea wa CCM Arusha amepaniki maana daladala nyingi za hapa mjini zinapeperusha bendera za CHADEMA ambazo hutolewa bure na kwa hiyari. Hali hiyo imepelekea Wapambe wa mgombea huyo kuwashawishi madereva wa daladala kupokea bendera za CCM na kuzipeperusha kwenye magari yao.
Inaonekana Mgombea Ubunge wa CCM Arusha ana pesa nyingi sana maana kama Wapambe wanaweza kutoa shilingi elfu 10 ili kupeperusha bendera kwenye gari wao wanabaki na ngapi?
Wajinga ndio waliwao!