Daladala ni biashara ya uhakika sana haina stress sana kuhusu wateja na kama ukiwa na yafuatayo utafanikiwa.
1.Huitegemei kwa asilimia kubwa kuendesha maisha yako.
2.Pesa yake haitaki itiwe mikono.
3.Fuatili chombo chako kwa 100%.
4.Hudumia gari yako inavyotakiwa service kwa wakati nk.
5.Upate dereva anayejitambua sio gegedu.
6.uwe mvumilivu maana faida huanza kuonekana miaka 2 mbele.
7.Usicheke na nyani uwe bandidu.
NB:Usinunue gari kama costa halafu ukapeleka shamba ni ngumu sana kurudisha faida kwa muda mfupi maana riski ni kubwa ziaidi. Tumewahi miliki chombo ila tukakipeleka shamba tulijuta sana maana risk ilikua kubwa zaid.
Ushauri wangu kama pesa ndogo Nunua zile Civillian Fupi huwa zinavumilia shida kwa daladala maana bodi yake haibebi mzigo mkubwa na haikatiki bodi.