Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
1 ANAHUSISHA MATUKIO YA USIKU NA MCHANA
Utasikia akisema jana tulikwenda shamba usiku na watu wengi wamevaa nguo nyeusi. Alikuja akaniamsha tukaenda tukaruka kama ndege. Ikiwa story hizi anazieleza mara kwa mara usidharau ukasema ndoto tu hapana kipo kitu.
2 ANAKUWA NDONDO KILA SIKU
Fahamu yeke na uchangamfu wake unapungua kila siku. Usoni utaona anabadilika anakuwa kama mtu ambae yupo yupo tu lakini kama hayupo vile.
3 ANA MATUKIO YA KUSHANGAZA
Anaweza kufanya vitu paka mukashangaa mfano wa vitu vya kichawi chawi na maneno ya kutisha wenzie kuwa mutaona usiku nitakachowafanya. Kama mzazi usipuuze hili mfatilie.
4 KUNYOLEWA USINGIZINI NA CHALE
Utakuta alilala vyema lakini asubuhi mara ukute kanyolewa au kachanjwa chanjwa dalili hizi sio salama kuwa makini na mtoto.
5 HOFU KIZA KIKIINGIA
Usiku ukiingia tu ana hofu sana sehemu ambayo hata hakuogopeshi. Au anaweza kukulalamikia kuwa kuna watu anawaona ikifika usiku wanamtisha. Usidharau hilo chunguza na uchukue hatua.