Dalili kuu 7 zinazoonyesha mtu ambaye atachelewa sana kufanikiwa.

Dalili kuu 7 zinazoonyesha mtu ambaye atachelewa sana kufanikiwa.

Saidimakini

New Member
Joined
Sep 22, 2018
Posts
1
Reaction score
3
Dalili kuu 7 zinazoonyesha mtu ambaye atachelewa sana kufanikiwa.
by Saidi Makini MAFANIKIO

1. Siku zote ana pesa za kununua vocha na kuweka vifurushi,ana pesa za kununua nguo lakini hana PESA za kununua kitabu kitakachomuongezea maarifa.

2. Siku Zote ana muda wa kuchart watsapp, kuangalia Movie, kusoma magazeti na Kupiga stori za mpira ama za wasanii lakini hana MUDA wa Kusoma kuhusu taaluma yake ama mambo ya kumuongezea ujuzi.

3. Siku zote akiona waliofanikiwa anawatuhumu aidha wameiba, ni freemason ama wana bahati katika maisha. Huwachukia na hataki kujifunza Kwao.

4. Siku zote hupenda kuhalalisha kufeli kwake kwa kujitetea, kulaumu uchumi, wazazi, serikali au amerogwa.

5. Siku Zote Hujiona anajua Kuliko Mtu Yeyote Yule na hapendi Kujifunza kwa wengine. Huongea sana Kuliko Kusikiliza.

6. Kila anachoingiza anatumia, ukimwambia kusave ama kuwekeza anasema ngoja nipate cha ziada nitaanza kesho.

7. Anajua mambo mengi sana, anajua stori za mafanikio, anasoma vitabu lakini hafanyii kazi ama anafanyia kazi kidogo sana katika kile anachokijua.

Je Unayo dalili mojawapo kati ya hizo? Amua kubadilika ishi au fanya ukijua kesho ipo .... NDOTO YAKO INAWEZEKANA, CHUKUA HATUA.
 
We umefanikiwa? Kipimo cha kufanikiwa au mtu mwenye mafanikio ni kipi?
Kitambi?
Gari?
Nyumba?
Kampuni?
Nk
Kuna watu wanapesa lukuki lakini wamefell kwenye mambo mengine
Pia kuna wamiliki wa nyumba hawana hata pesa ya chai
Usiwe mjinga kwa kupima mafanikio ya mtu kwa kigezo chako mwenyewe!
Kumiliki blog tayari unajiona umefanikiwa wakati umefeli kwenye kutathimini mambo
 
Vipi kama una sifa moja kati ya hizo ulizoandika, ina maana tayari umeshachelewa!?
 
Mafanikio hayapo kwenye maandishi hayo mnayoyaandika......Kuna siri na changamoto nyingi kwa waliofanikiwa...Aya umeandika na umeyafanyia kazi..!?kipi ulichofanikiwa?
 
We umefanikiwa? Kipimo cha kufanikiwa au mtu mwenye mafanikio ni kipi?
Kitambi?
Gari?
Nyumba?
Kampuni?
Nk
Kuna watu wanapesa lukuki lakini wamefell kwenye mambo mengine
Pia kuna wamiliki wa nyumba hawana hata pesa ya chai
Usiwe mjinga kwa kupima mafanikio ya mtu kwa kigezo chako mwenyewe!
Kumiliki blog tayari unajiona umefanikiwa wakati umefeli kwenye kutathimini mambo
Kwa harakaharaka tu unaonekana wewe ni negative person!
Na ni maskn wa fukra
 
ok, Kuna uhusiano wowote kati ya picha na ulichokiandika?
 
Back
Top Bottom