Dalili, tiba na madhara ya KIMEO

Dalili, tiba na madhara ya KIMEO

Barhearty

JF-Expert Member
Joined
Jun 18, 2013
Posts
319
Reaction score
29
naombeni msaada, mwanangu anaumwa umwa sana lakini kuna majirani zangu wameniambia atakua ana kimeo. Hvyo nataka kujua kwa kina kuhusu kimeo
 
naombeni msaada, mwanangu anaumwa umwa sana lakini kuna majirani zangu wameniambia atakua ana kimeo. Hvyo nataka kujua kwa kina kuhusu kimeo
Hao waliokuambia kuwa mwanano anao kimeo ungeanda kuwaona labda wanaweza kumtibia.

Acha masuala ya kimeo mtoto akiumwa Mpeleke hospitali Daktari atajuwa anaumwa na kitu gani achana na majirani zako hao watakupoteza.
 
Hao waliokuambia kuwa mwanano anao kimeo ungeanda kuwaona labda wanaweza kumtibia.Acha masuala ya kimeo mtoto akiumwa Mpeleke hospitali Daktari atajuwa anaumwa na kitu gani achana na majirani zako hao watakupoteza.

asante,ila hosp nimeenda sana nimeshalazwa zaid ya mara 2, lakini hakuna maendeleo na watu wanadai hosp hawatambui huo ugonjwa
 
asante,ila hosp nimeenda sana nimeshalazwa zaid ya mara 2, lakini hakuna maendeleo na watu wanadai hosp hawatambui huo ugonjwa
Umekwenda wewe Hospitali kulazwa au huyo mtoto wako? mbona unanichanganya? seme ukweli unaumwa wewe au mtoto ana miaka mingapi?
 
jinsi ya kukagua hicho kimeo.mchungize ulimi wake unanyanyuka juu..mm nnavyojua kimeo ni ile hali ya ulimi kutokunyanyuka juu unang'ang'ania chini....
 
mwanangu ndo anaumwa,kwahyo lazima na mie nilale nae,mwanangu ana miez 9 tu
Mtoto wako wa miezi 9 umejuaje anacho kimeo?Mpeleke tena hospitali ikiwezekana mpeleke kwenye hospitali ya watoto au mpeleke hospitali ya Muhimbili au Hospitali ya hindu mandal huko kuna wataalam wa watoto usingojee hapa ushauri mtoto mdogo sana huyo.
 
naombeni msaada, mwanangu anaumwa umwa sana lakini kuna majirani zangu wameniambia atakua ana kimeo. Hvyo nataka kujua kwa kina kuhusu kimeo

Pole, lakini ningeuliza Unamaanisha nini kusema mwanao anaumwa sana?...Ni nini hasa anaumwa? Hospitali ulikwenda kwa dalili gani? matibabu gani aliyopata?
 
Mtoto wako wa miezi 9 umejuaje anacho kimeo?Mpeleke tena hospitali ikiwezekana mpeleke kwenye hospitali ya watoto au mpeleke hospitali ya Muhimbili au Hospitali ya hindu mandal huko kuna wataalam wa watoto usingojee hapa ushauri mtoto mdogo sana huyo.

bado naangaika nae. Muhimbili nimeshakwenda, niombe tu mwanangu apone mana anaumwa marakwa mara
 
Pole, lakini ningeuliza Unamaanisha nini kusema mwanao anaumwa sana?...Ni nini hasa anaumwa? Hospitali ulikwenda kwa dalili gani? matibabu gani aliyopata?

anapata homa mara nying, anauzito mdogo ,anakua mweupe sana paka anakaribia kua wa njano pia awezi kula chaakula nikimlisha anatapika. Kwahyo nampa uji na maziwa bas. Uji pia anatapika
 
Sasa, Kimeo Kwa Jinsi Ni Juavyo Ni Ka Nyama Furani Ambako Huota Mwishoni Mwa Kinywa. Wanadamu Wote Tunacho Na Huwa Na Madhara Kinapokuwa Kirefu Na Kugusa Ulimi. Hapo Mtu Atapatwa Na Kikoozi Kisicho Isha, Atatapika Vyakula Vyote. Yaani Ni Kama Kinywa Kinakuwa Kimefungwa. Ni Hatari Kwa Maisha Ya Mtu. Wengine Wanaita Kilimi. Wazazi Wengi Iringa Huwapeleka Watoto Kwa FUNDI, Kukata Kimeo, Huwapeleka Tatizo Linapo Kuwa Kubwa Na Hata Habla Ili Kujihami. Ila Sikushauri Kufanya Hvi. Kukiondoa, Mimi Mwenyewe Kimekuwa Kikubwa Kimeanza Kunitisha, Lakini Nimesikia Tatzo Hilo Linatibiwa Vyema Kitaalamu Kwa Baadhi Ya Hospitali. Nimeandika Ili Kulaimisha Mada. Wakuu Endelea
 
Achana na issue za kimeo

Kesho watakwambia kakikate

Hakuna kitu kama hicho

Mpeleke mtoto kwa daktari wa watoto, achinguzwe na mtaalam ampaatie tiba ya kufaa
 
Sasa, Kimeo Kwa Jinsi Ni Juavyo Ni Ka Nyama Furani Ambako Huota Mwishoni Mwa Kinywa. Wanadamu Wote Tunacho Na Huwa Na Madhara Kinapokuwa Kirefu Na Kugusa Ulimi. Hapo Mtu Atapatwa Na Kikoozi Kisicho Isha, Atatapika Vyakula Vyote. Yaani Ni Kama Kinywa Kinakuwa Kimefungwa. Ni Hatari Kwa Maisha Ya Mtu. Wengine Wanaita Kilimi. Wazazi Wengi Iringa Huwapeleka Watoto Kwa FUNDI, Kukata Kimeo, Huwapeleka Tatizo Linapo Kuwa Kubwa Na Hata Habla Ili Kujihami. Ila Sikushauri Kufanya Hvi. Kukiondoa, Mimi Mwenyewe Kimekuwa Kikubwa Kimeanza Kunitisha, Lakini Nimesikia Tatzo Hilo Linatibiwa Vyema Kitaalamu Kwa Baadhi Ya Hospitali. Nimeandika Ili Kulaimisha Mada. Wakuu Endelea

hapo kwenye kutapika hiyo tabia anayo
 
Barhearty mpeleke mtoto kwa daktari wa watoto acha kuweka hizo imani zingine.
 
Last edited by a moderator:
mwanangu anaendelea vizuri. Ila bado kilo hazijakaa vizur
 
Hii imekuwa na matokeo mazuri sana kwa hali uliyoisema ya huyo mwanao 1.kata slace za Limao 2 (siyo ndimu)pamoja na maganda 2. Vitungu maji 2, 3. Vitungu saumu 2, 4. Tangawizi 2.
Saga mchanganyiko huo kwa brenda au kinu
Chemsha mchanganyiko huo na lita 2 za maji safi mpaka upate uji mzito. Acha u poe then chuja then weka kwenye chombo safi, iweke kwenye fridge. Chukua kijiko 1 cha chai cha asali changanya na vijiko 2 vya chai vya mchanganyiko huo mpe asubuhi mchana na jioni wiki moja pia ni kinga na hata watu wazima wanaweza kuitumia
 
Back
Top Bottom