Dalili za jezi za Simba na Yanga

wajibisha

Member
Joined
May 16, 2021
Posts
90
Reaction score
215
Habari za mchana wadau wa Soka. Napata pilau langu hapa nikiandika uzi huu.

Kwanza kabisa, pongezi kwa Simba kwa kuweka wazi kiasi itakachopokea kwenye mauzo ya Jezi kutoka kwa Vunja Bei Group.

Mkataba Ni wa Tsh. 2 Bilioni kwa kipindi cha miaka miwili. Kwa maana nyingine ni Tsh. 1 Bilioni kwa mwaka.

Kwa bahati mbaya sana waandishi wetu hawakuuliza maswali ya msingi kwenye ile press conference.

Ningependa kujua hiyo Tsh. 2 Bilioni Simba inaipata kwa namna gani na kwa muda gani.

Je kila Mwezi, Robo ya Mwaka, Nusu ya Mwaka ama kwa mwaka. Je Vunja Bei anapaswa kuweka wazi idadi ya JEZI atakazoingiza na kuziuza nchini?

Mwenye majibu ya maswali hayo anijuze.

Sasa tuje Yanga, hapa kuna shida kubwa kwa sababu hatujui ni mkataba wa kiasi gani na wa muda gani.

Ningependa kujua mkataba wa GSM kutengeneza jezi za Yanga ni wa kiasi gani na wa muda gani?

Kwa miaka mitatu iliyopita klabu ya Yanga imepokea kiasi gani kutoka kwa GSM kwenye mauzo ya JEZI? Idadi ya JEZI zilizoingizwa na kuuzwa?

Je Mkataba huo unaisha lini? Na mchakato wake uko vipi?

Lazima tukubale Biashara ya JEZI inalipa sana especially kwa Simba na Yanga kwa sababu na fan base kubwa.

Tufanye hesabu za haraka.

Kwa mujibu wa mtandao wa Ali Baba, kutengeneza jezi 10,000 inagharimu $2 sawa na Tsh. 5,000. Kumbuka unaponunua mzigo mkubwa una enjoy economies of scale.

Kadiria unaweka order ya JEZI 200,000

Gharama ya manunuzi - Tsh. 1 Bilioni
Gharama za kuingiza mzigo - 30% sawa na Tsh. 300 Millioni.

Jumla ya Gharama za Manunuzi - Tsh. 1.3 Bilioni

Tuje Sokoni sasa.

Wastani wa Bei ya JEZI - Tsh. 30,000
Mauzo ya JEZI Laki Mbili - Tsh. 6 Bilioni

Toa Gharama za Manunuzi itabaki Tsh. 4.7 Bilioni
Toa Gharama zingine kama Tsh. 700 Milioni.

Kwa makisio, muigizaji anabakiwa na kama Tsh. 4 Bilioni.

Sasa Swali klabu inapokea kiasi gani?

Ni vizuri tupate taarifa hizi. Na sio kwa Yanga Bali hata kwa Simba. Maana hizi na timu za wananchi.

Karibuni tujadiliane.
 
Huwezi kuuza Jezi 200,000
Sanasana jezi 50,000.
Halafu mkataba wa bilioni moja haimaanishi kuwa Simba watapata bilioni 1 automatically.
Vipengele ni lazima viwepo.
 
Simba kwa huu mkataba ameonyesha njia na wengine wazinduke sasa.
Kama ntakua sijakosea nilimsikia Haji akisema sio jezi tu pia na barakoa zenye nembo ya Simba,mataulo yenye nembo ya Simba,khanga za kinamama n,k.

Kuhusu ni shilingi ngapi klabu inapokea sijui ila mikataba yetu inausiru sana sio soka tu hata kwenye mambo ya siasa na serikali huko,hii inaonyesha jinsi sisi watanzania tulivyo.
 
Issue..iko hivi..Vunja Bei ataipa Simba Pesa angalau kila baada ya miezi mitatu toka taraehe ya kuanza rasmi kwa mkataba...so inamaana kila baada ya miezi mitatu Vunja Bei ataipa Simba milioni 250.

GSM wanaipa Yanga tsh 1,500 kwa Kila jezi wanayoiuza ..

GSM na Vunja Bei hawajawekewa kiwango cha idadi ya jezi wanazotakiwa kuuza..(kwa maana nyingine ni kwamba watakuwa wanalimiliki soko la jezi watakavyoona inafaa..wakiamua kuuza pisi 100 sawa..au wakiuza pisi 1,000,000 ni juu yao..Ila tu wazilipe hizo klabu kulingana na makubaliano .
 

GSM wanaipa Yanga tsh 1,500 kwa Kila jezi wanayoiuza ..

Sasa hapo inaelekea mkataba wa Yanga una utata. Kama GSM wanailipa Yanga sh. 1,500/= kwa kila jezi wanayoiuza, lakini idadi ya jezi zinazouzwa haijulikani, si anaweza kusema ameuza jezi 20,000 tu na hakuna atakayehoji maana hakuna takwimu? Basi heri mkataba wa Simba, maana wao hawahitaji kujua idadi ya jezi zitakazouzwa, wanachohitaji ni 2B ndani ya miaka miwili, msala wa wateja na idadi yake wamemuachia muuzaji
 

Basi mkataba wa Yanga una matatizo makubwa.

Kama Bei ya JEZI moja ni Tsh. 30,000 iweje Yanga wapewe Tsh. 1,500. Hiyo ni asilimia ni 5% tu

Kama hiyo ndio hali halisi Mkataba wa Simba Ni bora zaidi maana wana uhakika wa kupata Bilioni 1 kwa mwaka Vunja Bei auze ama asiuze.

Hata GSM wakiuza JEZI Laki Moja kwa mwaka klabu ya Yanga wataambulia Tsh. 150 Milioni Tu wakati Jumla ya Mauzo ni Tsh. 3 Bilioni kwa JEZI Hizo Laki moja.

Viongozi wa Yanga wanasimama wapi kwenye hili jambo.
 
Kwa nn huwezi kuuza JEZI 200,000 kwenye nchi yenye wananchi zaidi ya Milioni 60?
Jamaa huwa ana mawazo negative kwa kifupi unaweza kuuza hadi jezi milioni moja kutokana na fanbase ya hizi timu cha muhimu uhakikishe hizi jezi haziuzwi kiholela na ni kitu kinachowezekana
 
Hatuna takwimu za uhakika ila Simba inadai ina wanachama Milioni 10. Unahitaji watu Laki Mbili kwenye hiyo pool kutengeneza mabilioni.
Kuwa serious.
Simba haina hata wanachama 10,000
 
Huwezi kuuza Jezi 200,000
Sanasana jezi 50,000.
Halafu mkataba wa bilioni moja haimaanishi kuwa Simba watapata bilioni 1 automatically.
Vipengele ni lazima viwepo.
Jezi pisi 50,000 ni mtaji wa machinga kabisa hapo kkoo,ongelea wastani wa kuanzia 200,000 mpaka 350,000 hapo ndipo twasema faida ataipata na ana mtaji.

Kutengeneza jezi 1 quality kama za gsm inafika mpaka rmb 13, chukua hiyo rmb 13 tazama rate ya siku husika kwa mfano leo 13÷6.37 ambayo ni sawa na Usd 2 ambayo sawa na Tsh.4678/=
Gharama za uzalishaji 4678
Gharama za usafirishaji 1200
Bei ya kuuza jumla 17,000

Jumla 5878/=

5878×200000=1,175,600,000

Mtaji wa pisi 200,000 jumlisha usafiri inakua
5878×200000= 1,175,600,000

Kukokotoa faida kabla ya kodi
4678+1200-17,000 x200,000= 2,224,400,000/=

Faida ghafi kwa pisi 2000 ni Tsh.2,224,400,000/=
 
Mataulo ya kike????
 

Mkuu umeiweka vizuri sana. Viongozi wa Yanga walikubali vipi mgao wa Tsh. 1,500 kwa jersey kulingana na maelezo ya mchangiaji hapo juu?
 
Mkuu umeiweka vizuri sana. Viongozi wa Yanga walikubali vipi mgao wa Tsh. 1,500 kwa jersey kulingana na maelezo ya mchangiaji hapo juu?
Kwa kuwa hizo 1500 ndio huaminika zaenda kwa klabu bila hata auditing,ila kwa mlango wa nyuma wananufaika viongozi wanakula gawio kubwa tuu,biashara ya jezi ni ina hela balaa.

Gsm nampongeza kwa kuweza kukomesha jezi feki za yanga,kariakoo huikuti hata 1 yaani inatafutwa kama bange vile, anauza yeye na ukitaka kuuza wewe manake ukanunue kwake.

Changamoto ni viongozi wa yanga kuwa na hulka za upigaji na ktk jezi tumepigwa mnooo.

Ndio maana Mo hajakubali watu baki waingie kwenye menejimenti ya timu ili aweze kukontroo fedha yake,mswahili akiingia tuu anawaza kuongeza mke na amjengee na magari na miradi aipatie hapo hapo.
 
Yaani negativity inaua vitu vingi sana. Jamaa hawazi kwanini kwa mkapa uwanja unaingiza mashabiki kama 60k na wastani wa 75% ya mashabiki wanavaa jezi za Simba SC. Why ashindikane kuuza jezi 500k! Kumbuka,75% ya mashabiki wanaoingia BWM Stadium ni wakaazi wa DSM.
Weka makadirio kila mkoa uwe na mashabiki 6k tu wanunue jersey ya kwa 30k au 25k pesa ngapi itaingia?
Bado wale wasioingia uwanjani ila wananunua/wanavaa jersey ya Simba SC. Bado watoto, na bidhaa zingine anazo ruhusiwa kuzalisha.
Kwa ufupi, Vunja Bei ni kama ameinunua Trade Mark ya Simba upande wa bidhaa kwa miaka miwili.
Jamaa huwa ana mawazo negative kwa kifupi unaweza kuuza hadi jezi milioni moja kutokana na fanbase ya hizi timu cha muhimu uhakikishe hizi jezi haziuzwi kiholela na ni kitu kinachowezekana
 
HIZI hesabu za kwenye calculator raha sana.
mashabiki wenyewe hawa buku tu ya ada kwa mwezi hawalipi ndo wanunue jezi og 30000?
asilimia 50 ya jezi za hapa bongo ni feki
 

Kweli Kabisa kuuza JEZI mpaka Laki Mbili kwa mwaka kwa Simba & Yanga ni jambo rahisi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…