Habari za mchana wadau wa Soka. Napata pilau langu hapa nikiandika uzi huu.
Kwanza kabisa, pongezi kwa Simba kwa kuweka wazi kiasi itakachopokea kwenye mauzo ya Jezi kutoka kwa Vunja Bei Group.
Mkataba Ni wa Tsh. 2 Bilioni kwa kipindi cha miaka miwili. Kwa maana nyingine ni Tsh. 1 Bilioni kwa mwaka.
Kwa bahati mbaya sana waandishi wetu hawakuuliza maswali ya msingi kwenye ile press conference.
Ningependa kujua hiyo Tsh. 2 Bilioni Simba inaipata kwa namna gani na kwa muda gani.
Je kila Mwezi, Robo ya Mwaka, Nusu ya Mwaka ama kwa mwaka. Je Vunja Bei anapaswa kuweka wazi idadi ya JEZI atakazoingiza na kuziuza nchini?
Mwenye majibu ya maswali hayo anijuze.
Sasa tuje Yanga, hapa kuna shida kubwa kwa sababu hatujui ni mkataba wa kiasi gani na wa muda gani.
Ningependa kujua mkataba wa GSM kutengeneza jezi za Yanga ni wa kiasi gani na wa muda gani?
Kwa miaka mitatu iliyopita klabu ya Yanga imepokea kiasi gani kutoka kwa GSM kwenye mauzo ya JEZI? Idadi ya JEZI zilizoingizwa na kuuzwa?
Je Mkataba huo unaisha lini? Na mchakato wake uko vipi?
Lazima tukubale Biashara ya JEZI inalipa sana especially kwa Simba na Yanga kwa sababu na fan base kubwa.
Tufanye hesabu za haraka.
Kwa mujibu wa mtandao wa Ali Baba, kutengeneza jezi 10,000 inagharimu $2 sawa na Tsh. 5,000. Kumbuka unaponunua mzigo mkubwa una enjoy economies of scale.
Kadiria unaweka order ya JEZI 200,000
Gharama ya manunuzi - Tsh. 1 Bilioni
Gharama za kuingiza mzigo - 30% sawa na Tsh. 300 Millioni.
Jumla ya Gharama za Manunuzi - Tsh. 1.3 Bilioni
Tuje Sokoni sasa.
Wastani wa Bei ya JEZI - Tsh. 30,000
Mauzo ya JEZI Laki Mbili - Tsh. 6 Bilioni
Toa Gharama za Manunuzi itabaki Tsh. 4.7 Bilioni
Toa Gharama zingine kama Tsh. 700 Milioni.
Kwa makisio, muigizaji anabakiwa na kama Tsh. 4 Bilioni.
Sasa Swali klabu inapokea kiasi gani?
Ni vizuri tupate taarifa hizi. Na sio kwa Yanga Bali hata kwa Simba. Maana hizi na timu za wananchi.
Karibuni tujadiliane.