Dalili za jezi za Simba na Yanga

HIZI hesabu za kwenye calculator raha sana.
mashabiki wenyewe hawa buku tu ya ada kwa mwezi hawalipi ndo wanunue jezi og 30000?
asilimia 50 ya jezi za hapa bongo ni feki

Yanga waweke wazi wameuza JEZI ngapi za Yanga toka kuanza kwa mkataba na GSM. Simba wao wataingiza Bilioni Moja ama JEZI ziuzwe ama zisiuzwe
 
Wewe ni mfanya biashara kweli wewe?
Unajua kodi inayolipwa?Unadhani kuna biashara yenye faida kubwa namna hiyo?
 
Nahisi alimaanisha wapenzi ama mashabiki kwa lugha nyepesi.
Kwanza si kweli kimahesabu na pili hata tukisema ni kweli, mashabiki wa kununua mataulo ya Simba hawafiki hata 100,000.

Mashabiki wenyewe ukiwaangalia karibu 60% wanavaa jezi za mwaka Jana uwanjani.

Halafu clubs zetu huwa hazitoi mahesabu yake kwa jamii. Ni klabu feki tu na maelezo yake ni fake.
 
mkataba wa simba na vunja bei sio jezi peke yake yake.. Vunja bei kakodishwa trade mark ya simba..

so anaweza akatengeneza chochote kile akakiwekea nembo ya simba na kuuza.. na hata anaruhusiwa kuandaa matamasha kwa kutumia nembo ya simba

nje ya simbe kupata hizo 2b za jersey pia kila mauzo ya bidhaa yenye nembo ya simba kuanzia jersy hadi shanga kama ataziweka basi simba anapata % .

sijajua ni % ngapi hawajaiweka wazi ila kwenye mauzonya bidhaa zenye. nembo ya simba vubja bei anaipa simba percent.

na kwenye events pia vubja bei akiandaa tamasha kwa kutumia nembo ya simba wanakula
percent pia.


hivi unafikiri Mhindi (Mo) akubali 2b kavu bila marupurupu mengine wakat yeye mfanyabiashara anajua umuhimu wa trademark angalia


ukisoma between the line alichosema Vunja bei wakat anatangazwa mshindi wa tenda alisema kilicho mfanya Simba wampe yeye, sio hizo 2B maana hata washindani wengine walitoa kama hizo na zaid.

sema yeye alipewa sababu aliwaonyesha simba PROPOSAL YAKE JINSI ATAKAVYOIKUZA BRAND YA SIMBA.

utaona kuwa kwa maana nyingine aliwaonyesha simba kuwa watapata pesa zaidi kwa njia zingine maana simba atapata zaid ya hizo 2B. kitakachoongezeka itategemea na mauzo na matasha. Vunja bei akizembea promo asiuze sana imekula kwake kwa sababu simba minimum 2B yake iko pale pale. Vunja bei akiuza sana simba anafaidika zaid

washinda. wengine waliweka tu fixed amount basi

Yanga mkataba mpya wa jersy wawaige simba wasidiki na swala la kupewa fixes amount na 5% ya mauzo
 

Kweli Kabisa Yanga wana chakujifunza hapa maana kwa mkataba wa sasa hivi wanapata kiduchu sana.

Wapitie tena mkataba wao na GSM.
 
GSM anakula faida ya jezi za Yanga 2bn kwa mwaka, anatumia 1bn kwa njia ya ufadhili wa ops za team na bado ananyenyekewa kama Mfalme, viongozi wa Yanga ni majuha na ma chief Mangungo.
 
GSM anakula faida ya jezi za Yanga 2bn kwa mwaka, anatumia 1bn kwa njia ya ufadhili wa ops za team na bado ananyenyekewa kama Mfalme, viongozi wa Yanga ni majuha na ma chief Mangungo.

Kwa mahesabu hayo hakuna ufadhili hapo bali GSM ndio anayefadhiliwa na Yanga.

Swali. Nani atamfunga paka kengele?
 
Kwa mahesabu hayo hakuna ufadhili hapo bali GSM ndio anayefadhiliwa na Yanga.

Swali. Nani atamfunga paka kengele?
Viongozi wa Yanga na wao wanapata mgao wake kutoka GSM ndio maana wanashinda ofisi za GSM kila siku, hakuna wa kumfunga paka kengele.
 
Wanalipwa posho..pamoja na kusajiliwa wachezaji...
 
Sahihi kabisa
 
Wanalipwa posho..pamoja na kusajiliwa wachezaji...

Daaa kweli Bongo Nyosso. Ndio maana Uongozi wa Yanga hautaki kuitisha mkutano mkuu wa wanachama.

Taarifa itolewe tujue JEZI ngapi zimeuzwa ndani ya miaka mitatu iliyopita na Yanga wamepokea kiasi gani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…